Tatizo la Uric Acid

Tatizo la Uric Acid

Habari za jumapili wana jukwaa wote.

Naomba niende MOJA kwa MOJA kwenye mada, Nina ndugu yangu anasumbuliwa Sana na Uric Acid.

Ni mwezi sasa amekuwa wa kukaa na kulala tu uku akilalamika maumivu makali anayoyapata kwenye Maungio ya mwili wake.

Ameshakwenda hospitali na kufanyiwa vipimo NDIO akaambiwa ana Uric Acid, Amepatiwa dawa za mwezi mzima na zinaisha tarehe 6 mwezi wa pili. Lakini mpaka Leo hii ni kama hakuna afadhri toka ameanza matumizi ya dawa hizi.

Pamoja na dawa pia kuna vyakula ametakiwa kuacha kuvitumia Mara MOJA kama Samaki, Nyama, maharage n.k amefanya hvyo na sasa anatumia mboga za majani na mrenda pekee lakini bado maumivu ni pale pale.

Naleta kwenu tatizo ili niweze kupata msaada wa
Nini tufanye, Dawa na hata matibabu yoyote ambayo yataweza kumponyesha.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu

Nawasilisha
Sio kuacha nyama,samaki na maharage pekee pia wali ,ugali,chai chapati,bajia vitumbua ndizi mbivu .
Kuna jamaa alimponya mama yangu mkubwa hiyo kitu. Ngoja nijaribu kumtafuta kesho nikimpata hewani nitakutumia mawasiliano yake atamsaidia
 
Sasa alikuwa anakula nini?
 
Back
Top Bottom