#COVID19 Tatizo la UVIKO-19: Mwaka huu Moshi kutaendeka kweli?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Dah! Taarifa za msiba zimekuwa nyingi sana. Kwanza naamini Watanzania wanakufa sababu ya uzembe na kujitakia wenyewe. Mtu anakufa kwa nimonia watu mnajazana msibani kwenda kuzika bila tahadhari yoyote unategemea nini hapo? Umeenda kuzika mara 3 je Disemba utaenda tena.

Mkoa wa Kilimanjaro wilaya zinazoongoza kwa misiba mpaka sasa
Rombo
Moshi (v)
Hai
Sina watu wa kunijuzi kuhusu wilaya nyingine
Nina marafiki kadha wengi sana wameshasafiri kwa ajili ya msiba wengine wamsafiri zaidi ya mara 3( kulingana na hali yake kiuchumi) safari zote kwenda kuzika.

Kulingana na marafiki walionizunguka mikoa hii inaongoza kwa vifo

1. Kilimanjaro
2. Arusha
3. Mbeya
4. Dar es Salaam

Je, kwa mujibu wa marafiki, ndugu na jamaa zako ni mikoa mingapi unapata ripoti nyingi za misiba?

Tuchukue tahadhari, tuache mzaha
 
Mkuu hao watanzania watazodolewa bure. Waone hawa:

Hao huwa hawasikii wataenda na kufa wengi wao watakufa na wengine wataisambaza nchi nzima.

Wawekewe karantin hao wachaga watulie kwao.

Group za ukoo kwa wiki moja misiba haipungui mitatu na michango inatakiwa.
 
Swali la kujiuliza ni je, kwa nini iwe mikoa hiyo/wilaya hizo?
 
Mimi mpaka nimechoka kuchanga ukiangalia status ni mambo ya R.I.P tu,bora tulaumiane tu kwa sasa
 
Swali la kujiuliza ni je, kwa nini iwe mikoa hiyo/wilaya hizo?
Sijamaanisha ni hiyo tu ila ni kwa mujibu wa marafiki zangu,sina rafiki wa Dodoma ndio maana sijaitaja,sina mawasiliano na mtu wa Mwanza ndio maana sijui uzito wa huko. Ila huenda ikawa ni sehemu nyingi TANZANIA
 
Vile December nitajichimbia Dar bila kutoka kwenda kuhesabiwa Mchaga mimi👇
_20190906_111046.JPG
 
Mkuu hao watanzania watazodolewa bure. Waone hawa:

Bora serikali ingepiga marufuku kuzikana ili kupunguza hii kitu. Kama Rombo mochwari zilijaa karibu zote,tena maiti zimepandiana yan full vilio
 
Swali la kujiuliza ni je, kwa nini iwe mikoa hiyo/wilaya hizo?

Wewe unadhani mikoa na wilaya anazoleta mleta mada ni exhaustive? Kwani yeye ndiye mwenye kanzidata kuu?

Mwenye kanzidata kuu ana nia ovu ya kuficha takwimu ili ukae ukijiuliza maswali hayo unayojiuliza yasiyokuwa na tija yoyote.

Endelea kujiuliza.
 
Asante sana
 
Swali la kujiuliza ni je, kwa nini iwe mikoa hiyo/wilaya hizo?
Kwa sababu virus wakishaingia sehemu kutoka inachukuwa muda. Mkoa wa Kilimanajaro uko active sana na kuna wasafiri wengi wanaingia na kutoka kila siku. Hawa waliingiza virus na virus wakasambaa kwenye jamii yote wanapokutana kwenye shughuli kama misiba, ibada na burudani. Virus wakishaingia sehemu kutoka inachukuwa muda. Pia sehemu nyingine za Tanzania ni suala la muda tu watasambaa kama watu wataendelea kupuuza masharti
 
Shida pia ipo kwenye usafiri wa umma. Msiba umetokea watu wanachangana kwenda na coster wakifika wanazika wanarudi na coster wakifika Dar wanapanda daladala tena hakuna cha level siti wanawaachia wangapi? Ndio mana huku tuendako ni kugumu zaidi
 
Mkuu:

"Pia sehemu nyingine za Tanzania ni suala la muda tu watasambaa kama watu wataendelea kupuuza masharti"

Hapa labda kama ni kuwapa kesi tu wasiohusika. Ungesema kama serikali itaendelea kupuuzia ungeeleweka.

Hili ni janga la taifa. Uwajibikaji wake hauwezi kuwa kwa matakwa ya watu binafsi, wakiwamo hata wale wenye nia ya kujitoa mhanga.
 
Shida pia ipo kwenye usafiri wa umma. Msiba umetokea watu wanachangana kwenda na coster wakifika wanazika wanarudi na coster wakifika Dar wanapanda daladala tena hakuna cha level siti wanawaachia wangapi? Ndio mana huku tuendako ni kugumu zaidi
Kweli kabisa. Katika vitu ambavyo serikali imezembea ni kuweka mwongozo kuhusu mazishi. Juzi niliongea na jamaa yangu ananiambia yuko kwenye mazishi ya mama mmoja aliyefariki kwa covid. Watu wamejazana hakuna tahadhari
 
Back
Top Bottom