Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

Pole sana,ili kuondokana na tatizo hilo la kuota vipele,epuka kuweka maji kabla na baada ya kunyoa ktk sehemu husika,Kwa mfano kama unanyoa kichwani kwa kutumia wembe au mashine japo wembe ndo una madhara zaidi waweza kupaka spirit au after shave lotion,baada ya hapo usitie maji kichwan kwa muda wa kama siku mbili mfululizo.Fanya hivyo kila unaponyoa,njia hii ni rahisi sana na gharama hazitumiki.
 
Siku mbili mfukululizo maji yasiingie kichwani! Kwa hiyo kuoga ni shingoni kushuka chini bas!!
 
Mkuu umenifurahisha Sana, maana pamoja na yote umejitahidi sana kumjibu kila mmoja hapa. Tena kiungwana mno. Hongera na endeleza hii hali. Mmekuwa adimu sana watu wa namna yako.
unapokuwa na shida mkuu....huna budi kujinyenyekeza....ili kila mtu ajitoe kukupa taarifa zenye kuleta tija.....[emoji120] [emoji120]
 
Nimekuelewa mkuu, ila sio kidevuni...kwa suala la ndevu sina shida...bandiko la picha ni sehemu ya kisogoni...ndio uniletea matokeo hayo baada ya kunyoa.
 
Juma chief Hapo kichwani umeumia na nini?

Btw, unatumia nini kunyolea? wembe au? Kuna dawa naweza kukuelekeza
sijaumia mkuu, huo ni mkunjo wa nyama za shingo eneo la kisogoni. Hali hiyo unitokea punde baada ya kunyoa,baadae vinapotea. Kama kuna tiba unaifahamu mkuu nielekeze tu.
 
Usijali mkuu...hiyo ni sehemu ya kisogoni. Mkunjo huo ni nyama za shingo.
 
Hiyo ni sehemu gani ya mwili? Mbona kuna tundu?
ni sehemu ya kisogoni mkuu.....tundu kiaje hapo...[emoji1] [emoji1]..??? .....rekebisha macho yako....mkuu na tafsiri ya..bongo yako.....
 
Nashkuru kwa maelekezo mkuu..
 
Kwanza kabla ya ushauri wowote ingekupasa ueleze ni sehemu gani ambayo imeathirika mana kila sehemu hua ina kuwa na visababishi viambatanishi.
 
Hii inaitwa Sycosis Barbae. Inatokea wakati unaponyoa against plane ya nywele zako, inapelekea kutengenezwa kwa a potential space btn hair follicles ambayo pathogenic microorganisms wanaota. Kwa matibabu zaidi nitafute.
 
Kuna aina ya mashine hususani hizi za saluni zetu ni butu hivyo zinang'oa nywele badala ya kukata, kwa hiyo ukikata nywele kwa kifaa butu ikang'ooka lile tundu ilipong'oka nywele linakuwa affected na bacteria hatimae ngozi ina react kama hivyo manundu yanakutoka! SASA NINI UFANYE:

1. Tumia kifaa kikali kukata nywele zako, hata kama ni za sehemu za siri, kata kwa kifaa chenye ncha kali sana. Chagua wembe mkali
2. Inaaminika mashine za umeme huleta matokeo mazuri zaidi ya unyoaji hususani zile ambazo nyembe zake zinanolewa vizuri
3. Be selective. Wapi unanyoa je ni hair cutting salon au barber shop au chini ya mwembe kwa wazee wa zungu la unga na vitana
4. Chungua aina ya kemikali unazopaka baada ya kunyoa after shave liquids, lakini pia dawa za nywele kv blackening liquids nk unaweza kuwa allergic na moja ya hizo.

Credit: Kwa alienisimulia ilinisaidia nilisahau kitambo vipele vya ndevu na vya kwenye ncha za kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…