Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Kwanza tuweke maana halisi ya Machinga, Machinga kwa asili yake ni mtu anae nadi na kuuza bidhaa zake kwa kutembeza. Ingawa hivi karibuni maana halisi ya Machinga haipo tena. Kimsingi Machinga halisi ukiachana nae dakika 20 uwezi kumpata tena. Maana ya Machinga kwa sasa ni mfanya biashara mdogo anaevamia eneo lisilo rasmi na kujenga duka la chini ya kiwango na kufanya biashara zake za kudumu.
Sasa nirudi kwenye topic, tatizo la wavamizi na kujenga maduka ovyo ovyo haliwezi jutatuliwa hata kwa miaka 30 ijayo, siku zinavyokwenda ndivyo hali inakuwa mbaya zaidi. Hali itakuwa mbaya zaidi kwa sababu kila mwaka kuna maelfu ya vijana wa darasa la saba, form four kutoka vijijini wanaingia kwenye miji mikubwa bila plan yoyote.
Kwa kuwa hawana la kufanya ndio hao wanavamia na kujenga mabanda kila kona ya mji na kujiita Wamachinga. Swala la kuwatengea wajenga mabanda maeneo yao, hata wakimaliza maeneo yote ya wazi mijini haitatosha kama kundi la vijana lisilo na ujuzi wowote litaendelea kumiminika kwenye miji mikubwa.
Suluhu ya kupunguza wajenga mabanda ovyo lipo, ni kuweka urahisi kwa wenye viwanda, kuweka urahisi kwenye kuanzisha viwanda ikiwemo kuwa ruzuku, kufungua vyuo vingi vya ufundi na kuifanya elimu ya ufundi kuwa ya ulazima kama ilivyo kwa elimu ya msingi. Kuanzisha Mashamba ya umwagiliaji vijijini na kuwakodisha vijana kwa pesa ndogo ili wasione umuhimu wa kwenda mijini.
Nchi hii ina uwezo wa kutatua hilo tatizo lakini kwa akili za viongozi wetu sioni tukifanya hivyo hata miaka 30 ijayo. Pesa tunapata lakini tunaiharibu kwa mambo ya ovyo, mfano mabilioni ya ndege yangejenga irrigation schemes ngapi, mabilioni ya uwanja wa Chato yangejenga vyuo vya VETA vingapi vijana wakapata ujuzi?