Pole sana mama!
Nitakushauri kwa namna 2, moja kimwili na ya pili kiroho.
1. Ungeweka data za mzunguko wapo hapa ili tukuambie siku sahihi za wewe kushika mimba.
-Siku ya wewe kushika mimba baada ya sex kuna vinywaji hupaswi kunywa kama Pepsi, Coca Cola, Energy drinks, Azam Cola n.k
-Wakati wa Sex kuna mikao ambayo mwenzi wako anapaswa kukuweka, usikae juu yake au mambo sijui ya kushika ukuta n.k
Pia, nenda hospitali wewe kama wewe kwanza kama mmeo hujamwambia kuwa ulitoaga mimba. Yawezekana kizazi ni kichafu. Baada ya nenda na mmeo hospitali mkapime, huenda shida ipo kwake.
2. Inawezekana kwenu kuna mtu alishawahi kumwaga damu, yaani kuua. Damu isiyo na hatia ikimwagwa huwa inalia mbele za Mungu kupata haki yake, DAMU INADAI DAMU.
Kuna binti alinishuhudia kwamba kwao kulikuwa kuna tatizo la watu kufa kila mwaka, pia kulikuwa na tatizo la watu kutoa mimba. Wazee wao wakakaa kikao na kwenda mtoni kwenye miungu kutambika, wakaenda na wanyama ili kuwachinja kutoa damu. Wale wazee walitambika kwamba 'Kutokana na watu kila mwaka na utoaji mimba, kunafanya ukoo huu usikue, YEYOTE ATAKAYETOA MIMBA, KUFA NA AFE'.
Huyo binti alikujaga Dar na akapata mimba, bwana akaikataa. Mimba ya miezi 3, yule binti akaenda Dispensary kutoa mimba. Kilichotokea mle ndani ni ngumu kueleza hapa, hata mimi nikikumbuka huwa machozi yananilenga ila MUNGU ALIKUWA ANA MAKUSUDI NA YULE BINTI NDO MAANA HAKUFA. Mpaka sasa ameokoka, yupo ndani ya Yesu.
Maagano/Laana/Mikataba ina NGUVU SANA ktk ulimwengu wa roho. Yawezekana na ww upo sehemu hii.
Kubwa zaidi ni kumrudia Mungu, yupo tayari kukurehemu. Yeye mwenyewe alisema HAKUNA TASA KWA WATOTO WAKE.
Barikiwa dada yangu.