for life
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 3,397
- 4,436
Ok, kwa kifupi ni hivi, mbegu bora huwezi kuziangalia kwa Macho tu ukajua kuwa hixi ni mbegu bora au siyo.
Kinachotakiwa kufanywa ni kupitia katika Uchunguzi uitwao Semen Analysis ndipo watakapojua kuwa unambegu bora au la.
Kwanza tunaangalia Ujazo wa wa fluid unayoitoa ukiwa una ejaculate. Hiki ndo kitu cha kwanza, kawaida kuanzia 3.5mls mpaka 5mls ni normal.
Pili, tunaangalia rangi ya fluid uliyotoa na normal semen ina Rangi ya Umaziwa na pia Unjano kwa mbali. Ila kama fluid ni njano au kijani kuna uwezekano mkubwa wa matatizo katika uzazi hasa infection mfano magonjwa ya zinaa hasa Gonorrhea
Tatu, sasa huku ndipo kuna Technical issues ambapo tunafanya Semen Analysis kwa kuangalia Morphology au Umbo la Sperm moja moja na Jinsi gani Zinavyotembea (motility) pia na idadi (cell count)
Mbegu nzuri zinaonaekana kwa jinsi zinavyokuwa na shepu ya sperm yenyewe na pima zinavyoswim kwa uharaka na Straight forward si kuzunguka sehemu moja.
Kuna mambo mengi ya kitaalamu ni mpaka uingie darasani kidogo hapa sidhani kama tutaelewana.
Ila Cha Msingi ni nenda kapime kipimo cha Semen Analysis. Na kipimo hiki kinahitaji maandalizi ambayo daktari atakuambia.
But few ni haya
1. Unatakiwa usifanye Mapenzi kwa mda wa siku 3 mpaka tano kuupa mwili mda wa kutengeneza mbegu
2. Unapotoa Hiki kipimo hakikisha upo maeneo ya hospital ili kuwahisha kipimo hicho maabara ili kupata majibu sahihi zaidi kuliko kuchelewa Na kusababisha sperm kufa.
3. Unapotoa hiki kipimo jua unaenda kupiga punyeto kwahiyo mujiandae kisaikolojia.
N.k n.k
Mkuu kuna madhara yeyote externality yanayowez kuchelewesha au kutoundwa kabisa kwa mbegu, mfano mazingira, chakula, ufanyaji musturbation, na nk heshima kwako.