Tatizo la Waraka wa shehe Ponda ni zile takwimu hazina uhakika na ni kinyume na sheria

kama mtu ana uhakika wa anachosema na anayo dhamira njema kwa mujibu wa imani yake, anaogopa nini kukisema?
Kama malalamiko haya ya waislamu ni ya kweli, kwanini Mufti hayasemi mbele ya Rais na hata hadharani?
Nakumbuka enzi za Mufti akiitwa Hemed bin Jumaa bin Hemed, kuna kijana wa kiislamu alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kusema 'Yesu siyo Mungu', Mufti alitoka hadharani na kusema kuwa waislamu wote ndivyo wanavyoamini kuwa Yesu siyo Mungu, kwahiyo kumshikilia kijana huyo ni kama kumdhulumu haki yake ya kukiri anachoamini. Kama nakumbuka vizuri kijana yule alishinda rufaa yake, na ushindi wake kwa mtazamo wangu hauthibitishi kuwa Yesu siyo Mungu bali unathibitisha uhuru wa mtanzania kuamini dini anayoitaka ilimradi hajavunja sheria.
Vivyohivyo kwa yanayolalamikiwa, kwanini Mufti asiyawakilishe serikalini aseme wazi kuwa hivi ndivyo waislamu wanavyotaka, pawepo mjadala na uchunguzi kuhusu haki iliyokiukwa kama ipo, muafaka upatikane.
 
Kwahiyo mkuu katika maboresho hapo UDOM ndio waondolewe waislam 11 waletwe wakristo 11? .Hakuna hata mkristo alikuwa na sifa sawa za waliondolewe achanganywe katika hao 11?

Kuna tatizo hapo nawala sibahati mbaya.
Bado kuna mambo ambayo huyu aliyeleta malalamiko hajaweka wazi. Maswali haya:
1. Jumla ya wote walioondolewa UDOM ni hao 11 tu au mwandishi amechambua hayo majina ya waislamu yakatimia 11? Hao wengine ni kina nani? Tupate ushahidi kutoka UDOM.
2. Jumla ya watu wote waliopelekwa UDOM kuziba nafasi wazi ni hao 11 tu, au mwandishi amechambua majina ya hao wakristo 11? Hili nalo lahitaji ushahidi kutoka UDOM
3. Kabla ya kuondolewa hao waislamu 11, wahadhiri wa kiislamu jumla yao ilikuwa wangapi na sasa wamebaki wangapi? Hali kadhalika kwa hao wahadhiri ambao ni wakristo walikuwa wangapi kabla ya mabadiliko na sasa ni wangapi?
4. UDOM wanasemaje kuhusu mabadilik haya, yalikusudiwa kufanikisha nini? Vigezo (criteria) vilivyotumika katika mabadiliko hayo ni vipi? Dini ni criterion mojawapo?

Tukishapata majibu ya maswali hayo ndipo tunaweza kusema kama kulikuwa na nia ovu ya ubaguzi au la.
 
Mkuu hukufatilita mjadala toka mwanzo, Yule Mama nafikiri mama Kabaka Kama sijasahau alijibu majibu ambayo hayana kichwa Wala miguu tafuta hio thread iko humu tangu mwaka Jana watu wakilalamika.
 
Apigwe tu hizi chokochoko za ponda zilikuwa zimepoa baada ya kumsweka ndani. Teuzi haIfuati dini bali watanzania wenye uwezo na sifa za kuchapa kazi
so wenye sifa na uwezo wa kuchapa kazi ni watanzania wa imani fulani pekee?
 
huku mtaani kwetu wapo wengi mno walio soma hayo maandishi yao na class walitusua kinyamaa!!!sawa na tusio soma yale maandishi na class tuka chemka mbaya!!!
 
Mkuu hukufatilita mjadala toka mwanzo, Yule Mama nafikiri mama Kabaka Kama sijasahau alijibu majibu ambayo hayana kichwa Wala miguu tafuta hio thread iko humu tangu mwaka Jana watu wakilalamika.
Samahani sikuiona hiyo thread. Kama una urahisi wa kuipata naomba uniwekee link
 
Zitto is smarter than that, anajua akisema hivyo atakosa kura za wakristo ambao anawahitaji pia. Asimame katikati kwa neno la haki sawa, hapo atafanikiwa. Haki sawa kwa maana ya kwamba anataka kuondoa dhuluma zote zilizotendewa watu wa aina zote. Nina uhakika watu wa kila kundi wana malalamiko yao mbalimbali, ajikite kwenye haki na usawa.
 
Ubaguzi sio mzuri,utatugharimu hata tusiopenda ubaguzi.
 
Pendekeza tume iwe na watu gani,maana inawezekana ni kelele tu kumbe tume huru ndiyo iliyopo
 
Ukweli hauhitaji sheria yoyote kusimama pahala pake.

Udini haufai, nchi hii ni yetu sote, tunahitaji kuwa fair kwa makundi yote ya kijamii.

80% kwa 20% ni too much, haijakaa sawasawa hata kidogo

Waislamu majority wanaunga mkono waraka
Sasa unasoma madrasa halafu upewe ukurugenzi?? Akili matope hiyo.

Waislamu wasipoishukuru serikali ya CCM hapo hata mungu ataendelea kuwapiga kofi,yaani Mzee Mkapa aliwapa chuo kikuu Morogoro pale na wanasoma waislamu tu,bado mnasema mnabaguliwa?

Taja chuo gani wakristo wamepewa zaidi ya vyuo vyao kwa kuthamini elimu dunia badala ya elimu ya tusikokujua.

Tuongee ya kweli,unajiita muislamu safi halafu unaongea uongo tu.

Kabla hujalaumu,tafuta idadi ya wasomi wakristo against waislamu watanzania. Kama umesoma utagundua hata bila kuzunguka.
 
pia tusi sahau ile MEMORANDUM OF UNDERSTANDING baina ya Serikali na Makanisa pengine ndiyo sababu ya makanisa kuwa na vyuo na mashule! ikiwa ni sababu basi niwazi kuna upendeleo wa imani fulani dhidi ya imani fulani unao fanywa na serikali.
 
Siku na sisi tusioamini katika hizo dini zenu zilizokuja na mashua tukiamua kutaka upendeleo kwenye vyeo na teuzi ndio mtajua sisi ni nani....hahahahah natania tu, miungu wetu hawana wivu kama wa kwenu; tunawaandika kwa herufi ndogo ya mwanzo hawagombi, tunaweza kuwachanganya wao na yule wa kwenu bila wao kuwa na wivu, wakati hao wa kwenu huwezi kuchanganya Allah na Yehova yaani ufahamike unasali kwenye madhehebu yote mawili uachwe hivi hivi! Huyo wa kwenu anataka dunia yote na sayari zingine wawe ni waumini wake tu....wa kwetu hana kiu na idadi ya waumini, hata watatu tu wanatosha, hata majina ya "ubatizo'' mungu wetu hana habari nayo hata uitwe Masoud au Yohana hawezi kukubagua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…