Tatizo la wasailiwa kulala nje siku za usaili Dodoma

Tatizo la wasailiwa kulala nje siku za usaili Dodoma

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Hili limekua ni tatizo kubwa sana.

Mdogo wangu ameenda kwenye usaili Dodoma mpaka muda huu saa sita usiku hana mahali pakulala, yeye na wenzake wametembea nyumba zote za wageni zimejaa.

Hivi hakuna utaratibu mwingine serikali inaweza kuufanya ili vijana wetu wasijazwe huko Dodoma.

Inaonekana nyumba za wageni hazitoshi huko.
 
Wakatoliki wapewe Ardhi kubwa hapo Dodoma mjini wajenge hostel za kutosha, hii kazi ya hostel kanisa inaiweza hasa na kwa gharama za maradhi nafuu kabisa.

YMCA zote kulala ni 20,000/= chakula bei chee, serikali wakati wa kuhamia Dodoma imekurupushwa tu na yule mwehu bila kuwashirikisha hawa wadau muhimu wa huduma za maradhi.
 
Utasikia Bodi ya Korosho Tanzania nayo ina hamishiwa Dodoma toka Mtwara, makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania THA inahama toka DSM kwenda Dodoma n.k n.k

Huku ni kujaza mji wa Dodoma na kushindwa kusambaza ajira na keki ya taifa sehemu nyingine za Tanzania.

Dodoma ibaki kuwa makao ya mhimili wa Bunge / parliament / National assembly ili mhimili huu uendelee kuwa huru.

Dar es Salaam iwe makao makuu ya serikali ya Muungano wa Tanzania ili muhimili wa dola usiote tena mizizi mpaka ndani ya mhimili wa Bunge kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano Bunge kumezwa na mhimili wa dola.

Mji wa Arusha uwe makao makuu ya mhimili wa Mahakama Kuu ili jaji mkuu na mahakama ya rufani wabaki huko mbali siyo kila siku wanahudhuria hafla za wafanyakazi wa serikali kuu na mikoa wakiapishwa na kwa namna hii ya mgawanyo wa mihimili, Mahakama iwe huru toka minyororo na jinamizi lililoundwa ktk awamu ya tano. Arusha ni makao ya korti ya Afrika Arusha | Search Results | African Court on Human and Peoples' Rights , EACJ www.eacj.org , UN Korti za masuala ya maovu dhidi ya binadamu International Residual Mechanism for Criminal Tribunals May Conclude Most Cases by May 2021, Its President Tells Security Council | Meetings Coverage and Press Releases hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania Judiciary of Tanzania | Home watakuwa wanabadilisha mawazo na wasomi wenziwe kuhusu namna bora ya Mahakama za Tanzania kujiendesha kwa uhuru na kumaliza mrundikano wa kesi kwa kuwa kila siku wanahudhuria hafla zote za mhimili wa serikali .

The Many Capitals of South Africa
South Africa's three capital cities are strategically placed throughout the country, each hosting a separate segment of the nation's government. When asked about a single capital, most people would point to Pretoria.
  • Pretoria is the administrative capital. It is home to the executive branch of the South African government, including the President of the Cabinet. The city also hosts many departments of government and foreign embassies.
  • Located in the province of Gauteng, Pretoria is in the northeast part of South Africa and near the city of Johannesburg.
  • Cape Town is the legislative capital. It is home to the country's legislative parliament, including the National Assembly and National Council of Provinces.
  • Located in the southwest corner of South Africa in the province of Western Cape, Cape Town is the second-largest city in population.
  • Bloemfontein is considered the judicial capital. It is home to the Supreme Court of Appeal, the second-highest court in South Africa. The Constitutional Court (the highest court) is located in Johannesburg.
  • Located in the province of Free State, Bloemfontein is in the center of South Africa.
 
Huu ushamba mpaka lini wakati teknolojia imekuwa? Kwanini wasifanye interview kwa simu ili wachuje kwanza watu kadhaa then baadaye wakipata wazuri ndiyo wanawaita kwa final interview!

Mtu Kama anajua,anajua tu whether muonane physically au online!
 
Wakatoliki wapewe Ardhi kubwa hapo Dodoma mjini wajenge hostel za kutosha, hii kazi ya hostel kanisa inaiweza hasa na kwa gharama za maradhi nafuu kabisa.

YMCA zote kulala ni 20,000/= chakula bei chee, serikali wakati wa kuhamia Dodoma imekurupushwa tu na yule mwehu bila kuwashirikisha hawa wadau muhimu wa huduma za maradhi.
Unakashifu hewa?,,unakashifu familia yake,?au wewe ndio mwehu badala ya way forward unadumu Kwenye kulalama kila uchao
 
Wakatoliki wapewe Ardhi kubwa hapo Dodoma mjini wajenge hostel za kutosha, hii kazi ya hostel kanisa inaiweza hasa na kwa gharama za maradhi nafuu kabisa.

YMCA zote kulala ni 20,000/= chakula bei chee, serikali wakati wa kuhamia Dodoma imekurupushwa tu na yule mwehu bila kuwashirikisha hawa wadau muhimu wa huduma za maradhi.
Maradhi=malazi

Mwehu wahed ww
 
Back
Top Bottom