Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salam
Mwaka jana niliomba ushauri kwa tatizo la kukosa uzingizi. Watu wengi walinipa advice na mwishowe nikaupata. In fact nilipewa dawa ya kunywa kwa kusaidia hali yangu ya kawaida kurudi. Within 3 weeks nikaacha dawa na tatizo likawa limeisha. (Link)
Sasa since September last year tatizo limerudi. Sio ghafla, nimeanza kupoteza saa moja, then saa mbili, then saa tatu za usingizi; hadi sasa hivi nalala 3 to 4 hours kwa 24hs... Miezi tano and getting worse.
Kawaida yangu nahitaji 7-8 hours ya usingizi kwa kufunction properly.
Just like last year tatizo la kukosa usingizi limeleta irritability, na limenisababisha kuwithdraw from social life kabisa (almost 90%)
My performance is affected pia... Nikienda kwa daktari napewa dawa.
Nimejaribu dawa zimekataa, nimejaribu meditation, walking, maziwa, asali, biringanya, mchanganyiko wa hivyo vyakula vyote nil.
Nimejifungia in my room hadi usingizi upatikane haukupatikana...
Sasa sijui nifanye nini...
Naomba walio kutana na shida hii (binafsi au kwa watu wao) wanambie walicho jaribu, maybe it could work for me...
Asante sana ndugu.Go Herbal RR.
Kama unaweza kupata majani ya tunda la Passion.
1. Kata majani kiasi cha kujaa kiganja (fungo la mkono) wako. Chukua yale mateke kiasi ambayo ni ya kijani kibichi zaidi. Yaoshe vizuri
2. Yachemshe kwa muda wa dkk 10 ktk maji lita moja, utapata some sort of delicious green tea
3. Chuja kwa kitambaa safi, yapite maji tu.
4. kunywa kikombe cha chai asubuhi kimoja na jioni kimoja. Kamwe usinywe mchana wkt jua linawaka kwani utajikuta umekuwa mchovu as if umekunywa dawa za kikohozi zenye sedatives.
Hii sio kwa Insomnia tu, inatibu pia anxiety na nervousness kama itatumiwa kwa muda mrefu.
Usiweke sukari tafadhali. Sina hakika ya nini kitatokea kama utaweka. Isije ikawa mchanganyiko wake una shida, nikushauri ufanye vile nilivyotumia mimi. Naamini ndani ya wiki ya kwanza utaona mabadiliko, unless kichwa chako kiwe kimeharibiwa na pombe za muda mrefu
Usinipige ban,nakushauri kimbia baharini halafu mwambie shem anywe hata mchuzi wa pweza na matikiti maji akuchezeshe dushelele la masaa matatu hivi,then utaniambia utachelewa asubuhi mzigoni mwambie jirani akuamshe ikifika saa kumi na mbili asubuhi otherwise utakuja stuka saa nne asubuhi fanya hivyo kwa wiki nzima then acha utaendelea kupata usingizi mzito,acha kula kahawa na vinywaji vya cola mida ya usiku,jitahidi kuuchosha ub ongo b4 kulala.soma novel zenye vingereza vigumu etc
Huu ndio ukweli Nitty.Pole sana RR, kwa sasa ni kwamba akili yako umeishaijengea woga wa kukosa usingizi kwa hiyo hata unapoenda kulaa unaanza kuanza kuwaza kama leo utapata usingizi. Hii itakufanya ukose usingizi kila siku.
Jaribu kuifanya akili yako isiwe na mawazo hayo then chagua mda maalumu wa kupanda kitandani na kama una radio weka nyimbo za taratibu za kukuchombeza utajikuta mawazo yanaondoka na usingizi unakuja
Na mimi nilisoma hiyo post nikasimama kwanza na kwenda kuchekea nje kwa dakika mbili then nikarudi kumjibu. :lol:Roulette my alter.... sababu tatizo langu ni tatizo lako sitabanduka hapa... ila time being naomba ngoja nikatafakari hii post nione kama nimeelewa ikiwa mwanzo wa kutatua tatizo. Dah!
Usinywe kahawa usiku na uwe unafanya mazoezi jioni , pia kama unavuta sigara acha kabisa.
Thanks wakuu. Sivuti sigara wala sinywi kahawa...jaribu kuwa Gym class especially in late hrs kama kuanzia saa 1:30 jioni then jitazame sana NA vyakula unavokula jioni viwe vyepesi sana, zuia caffeine, asteroids na any kind of viagra. namaanisha epuka vitu vyote vinavyostimulate the unconscious brain nyakati za jioni ,
Na mimi nilisoma hiyo post nikasimama kwanza na kwenda kuchekea nje kwa dakika mbili then nikarudi kumjibu. :lol:
Thank's love kwa kukaa na mimi... :hug:
Pamoja saana dear.....:rockon: Hata hivo iko tempting, nadhani nitaanza na hio solution kwanza....lol
Asante Kakalende. hii pia inaweza kua chanzo cha shida yangu maana nilitakiwa kwenda leave in october (kumbuka shida ilianza september) but sikuweza. 3 month later ikawa december but nilichukua leave ya kwenda msibani. huko sikupumzika vizuri, si unajua tena mambo ya matanga? na sasa nachukua leave in mach. itakua ni almost 7 month bila likizo. kazi yangu kwa sasa ni ya kawaida.RR pole sana na shida hiyo.
Kukosa usingizi umepata stress na huenda inachangiwa na routine yako ya kila siku; ikiwa ni pamoja na kazi nyingi sana. Hakuna dawa zaidi ya kuchukua likizo na kupata muda kidogo nje ya kazi za kawaida; hata kama unajiajiri, panga safari nje ya mji unaoishi, tembelea marafiki na kama upo bongo, nenda kijijini kwa bibi.
Tatizo hili linatumbua wengi na hivi ndivyo tunavyofanya; hakika kama ratiba yako inahusisha kufanya kazi masaa mengi na wakati mwingi hadi weekends, unahitaji mapumziko ya angalau wiki 1 kila baada ya wiki 6. Iwapo ratiba yako ni ya kawaida, basi kila miezi 3 hakikisha unapata wiki 1 ya likizo.
Thanks wakuu. Sivuti sigara wala sinywi kahawa...
kusema ukweli kwa sasa I don't attend any gym club na wala sifanyi mazoezi. Lakini mara 2 au mara 3 kwa wiki natembea kwa mguu long distances... nitajaribu kuanza mazoezi hata hapa nyumbani (Kumbukeni sitamani kabisa kuona watu)
MasturDating... that's the word! yaani ndio mimi kabisaaaa. Spending all my time with me and enjoying it sana tu.Pole RR, hiyo sentenso ya mwisho hapo ndo yanitia wasiwasi. Nikiwa na mawazo sana napata shida kulala. Hutaki kuona watu ni dalili ya stress. Taking a walk is also avoiding people manake unajua you don't have to mingle. Push yourself to the gym, utaona watu na kutania ama kucheka nao. Go out for movie and stop MasturDating. Utaanza kunifanya nikuwazie kama a crazy scientist living with monkeys and sharing a bed with turtles! Staki banaa!