Tatizo letu wasomi wengi, tunataka kuyaendesha maisha kama makocha wakati bado tuko level ya uchezaji

Tatizo letu wasomi wengi, tunataka kuyaendesha maisha kama makocha wakati bado tuko level ya uchezaji

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Kwangu mimi, hii ni moja ya changamoto kubwa sana kwa wasomi wengi siku hizi.

Nimetumia mfano wa kocha na mchezaji kwa sababu ili uwe kocha mzuri, mara nyingi unatakiwa kwanza kupitia level ya uchezaji. Unahitaji kuijua game, kuipitia, kufanya mistakes, kujifunza na kupata experience kabla hujaanza kuwaambia wengine wafanye nini.

Hivi ndivyo hata maisha yalivyo.

Ili uweze kufanya kitu kwa ufanisi, mara nyingi unahitaji kwanza kuwa na experience nacho. Knowledge ya darasani ni muhimu, lakini experience ya uwanjani nayo ina nafasi yake kubwa.

Tatizo ni kwamba siku hizi tunataka kuruka stages.

Mtu anamaliza chuo leo, kesho anaomba mtaji nyumbani, anafungua kampuni yake, anaajiri watu na kuanza ku-manage biashara ambayo yeye mwenyewe hajawahi kufanya kazi ndani yake.

Ana degree, ana confidence, ana vision… lakini hana practical experience, management skills wala exposure ya kutosha.

Matokeo yake, mwanzo mambo yanaweza kwenda vizuri kwa sababu kuna mtaji. Lakini biashara inapokutana na pressure halisi–madeni, cash flow, clients, suppliers, employees, deadlines na decisions ngumu–ndipo uwezo halisi unaanza kuonekana.

Nina rafiki yangu mmoja nilimaliza naye chuo.

Kwao mambo yalikuwa safi. Baada ya kumaliza chuo, akapewa mtaji na akaanzisha kampuni yake ya construction na supply.

Mwanzo mambo yalikwenda vizuri sana. Kampuni ikaanza kupata kazi, pesa ikaingia, na maisha yakaanza kuwa mazuri.

Lakini kadri muda ulivyokwenda, mambo yakaanza kubadilika.

Sababu kubwa ilikuwa management.

Jamaa hakuwa na experience ya kutosha kwenye uendeshaji wa kampuni. Akaanza kuingia kwenye madeni, baadhi ya kazi zikawa hazimaliziki kwa wakati, commitments zikawa nyingi kuliko uwezo wa kampuni kuzimudu, na eventually mambo yakawa mazito.

Mwaka huu akanyanyua mikono juu.

Amerudi kwenye ajira rasmi, amebadilisha kabisa line ya kazi, huku akijaribu kujinasua kwenye madeni aliyoyaacha.

Kinachonichekesha zaidi ni kwamba wakati kampuni yake ilipokuwa inafanya vizuri miaka ya mwanzo, jamaa alikuwa tayari ameanza kuwashauri watu kuhusu maisha. 😂

Kumbe naye mwenyewe alikuwa bado anahitaji ushauri.

Hapo ndipo nilipoanza kuona tatizo kubwa tulilonalo kama wasomi:

Tunasoma sana, halafu tunataka kuanza maisha tukiwa makocha kabla hata hatujacheza mechi.

Degree inakupa foundation, lakini haiwezi kukupa automatically experience ya ku-manage watu, biashara, fedha, pressure na failure.

Wakati mwingine si vibaya kuanza chini.

Fanya kazi kwenye kampuni ya mtu, jifunze industry, observe management, fanya mistakes ukiwa kwenye system, jenga network, elewa numbers, halafu ukifika wakati wa kuanzisha kitu chako, unaingia ukiwa na experience ya uwanjani.

Usikimbilie kuwa kocha kwa sababu tu umehitimu chuo.

Kwanza cheza game.
Jifunze game.
Pitia magumu ya game.
Ukishajua game vizuri, ndipo ukaanze kuwafundisha wengine. 😂
 
Shida ya graduates wengi wa sasa hivi ni kutaka overnight success bila kupitia mchujo wa experience. Unakuta mtu ana vision kubwa sana ya biashara lakini hata namna ya ku-deal na supplier msumbufu hajui, mwisho wa siku mtaji unakata na anarudi square one.
 
Kinachonichekesha zaidi ni kwamba wakati kampuni yake ilipokuwa inafanya vizuri miaka ya mwanzo, jamaa alikuwa tayari ameanza kuwashauri watu kuhusu maisha. 😂
Hicho ndio kinafanya wakianguka tuwacheke, na tutawacheka tu hata kama Sisi wenyewe ni oyaoya, mtu Kapata vihela vya kuhongwa au kupewa which is good, lakini anaanza kuwabananga wengine na kuwabagaza😂😂
 
Shida ya graduates wengi wa sasa hivi ni kutaka overnight success bila kupitia mchujo wa experience. Unakuta mtu ana vision kubwa sana ya biashara lakini hata namna ya ku-deal na supplier msumbufu hajui, mwisho wa siku mtaji unakata na anarudi square one.
Ni kweli mkuu, wakipata changamoto kidogo wanasusa 😂😂😂
 
Hicho ndio kinafanya wakianguka tuwacheke, na tutawacheka Tu hata kama Sisi wenyewe no oyanoya, mtu Kapata vihela vya kuhongwa au kupewa which is good, lakini anaanza kuwabananga wengine na kuwabagaza😂😂
Tunaridhika mapema sana mkuu
 
Wasomi na upumbavu , akishamaliza chuo anakuambia sababu ya umaskini ni elimu 😀 😀 😀 yeye mwenyewe ni maskini , wanafikiria kutatua umaskini ni fikra badala ya kufanya kazi .

Utamuona anapigania katiba mpya , sasa hiyo katiba mpya inaleta ugali , wakati bado nchi watu wanapiga kazi na kutusua ..Wasomi akili zao zimeganda , anawza kukaa na pc , kuvaa suti ila atumie hizo akili anazodanganywa kumbe real life ni struggle zote za kimwili na akili .

Mwishoe, wanapoteza muda tu mjini kwa kuwaza watkuwa matajiri siku moja .
 
Mkuu hapa uliposema kuwa maisha halisi yana hitaji struggle zote za mwili na akili, ni kweli kwa 100%
 
Wasomi na upumbavu , akishamaliza chuo anakuambia sababu ya umaskini ni elimu 😀 😀 😀 yeye mwenyewe ni maskini , wanafikiria kutatua umaskini ni fikra badala ya kufanya kazi .

Utamuona anapigania katiba mpya , sasa hiyo katiba mpya inaleta ugali , wakati bado nchi watu wanapiga kazi na kutusua ..Wasomi akili zao zimeganda , anawza kukaa na pc , kuvaa suti ila atumie hizo akili anazodanganywa kumbe real life ni struggle zote za kimwili na akili .

Mwishoe, wanapoteza muda tu mjini kwa kuwaza watkuwa matajiri siku moja .
Comment ya mafisadi utajijua Tu😂
 
Mimi nfanya kazi wewe dogo , sio wanataka madaraka kwa kuwashawishi nyie wajinga , hawana kazi mpaka wachangishe pesa za kikao chao , mil 300 za nn zaidi ya kulipana posho na kuhudumia magari ya viongozi wao . wajinga mtaendelea kuburuzwa mpaka kufa .
Mkuu wewe kula maisha mazuri ni yako wewe na familia yako, Sisi hayatuhusu
 
Mkuu wewe kula maisha mazuri ni yako wewe na familia yako, Sisi hayatuhusu
Tatizo mnatia huruma sana , badala ujikite kufanya kazi kazi kubwa kujifanya unajua , kama una elimu fanya tafiti kubwa zenye tija sio kushauri tu ni upuuzi .

Unafikiria kama wanasiasa wasingekuwa wanapata pesa wangekuwa wanapambania vyama ?
 
Back
Top Bottom