Kwangu mimi, hii ni moja ya changamoto kubwa sana kwa wasomi wengi siku hizi.
Nimetumia mfano wa kocha na mchezaji kwa sababu ili uwe kocha mzuri, mara nyingi unatakiwa kwanza kupitia level ya uchezaji. Unahitaji kuijua game, kuipitia, kufanya mistakes, kujifunza na kupata experience kabla hujaanza kuwaambia wengine wafanye nini.
Hivi ndivyo hata maisha yalivyo.
Ili uweze kufanya kitu kwa ufanisi, mara nyingi unahitaji kwanza kuwa na experience nacho. Knowledge ya darasani ni muhimu, lakini experience ya uwanjani nayo ina nafasi yake kubwa.
Tatizo ni kwamba siku hizi tunataka kuruka stages.
Mtu anamaliza chuo leo, kesho anaomba mtaji nyumbani, anafungua kampuni yake, anaajiri watu na kuanza ku-manage biashara ambayo yeye mwenyewe hajawahi kufanya kazi ndani yake.
Ana degree, ana confidence, ana vision… lakini hana practical experience, management skills wala exposure ya kutosha.
Matokeo yake, mwanzo mambo yanaweza kwenda vizuri kwa sababu kuna mtaji. Lakini biashara inapokutana na pressure halisi–madeni, cash flow, clients, suppliers, employees, deadlines na decisions ngumu–ndipo uwezo halisi unaanza kuonekana.
Nina rafiki yangu mmoja nilimaliza naye chuo.
Kwao mambo yalikuwa safi. Baada ya kumaliza chuo, akapewa mtaji na akaanzisha kampuni yake ya construction na supply.
Mwanzo mambo yalikwenda vizuri sana. Kampuni ikaanza kupata kazi, pesa ikaingia, na maisha yakaanza kuwa mazuri.
Lakini kadri muda ulivyokwenda, mambo yakaanza kubadilika.
Sababu kubwa ilikuwa management.
Jamaa hakuwa na experience ya kutosha kwenye uendeshaji wa kampuni. Akaanza kuingia kwenye madeni, baadhi ya kazi zikawa hazimaliziki kwa wakati, commitments zikawa nyingi kuliko uwezo wa kampuni kuzimudu, na eventually mambo yakawa mazito.
Mwaka huu akanyanyua mikono juu.
Amerudi kwenye ajira rasmi, amebadilisha kabisa line ya kazi, huku akijaribu kujinasua kwenye madeni aliyoyaacha.
Kinachonichekesha zaidi ni kwamba wakati kampuni yake ilipokuwa inafanya vizuri miaka ya mwanzo, jamaa alikuwa tayari ameanza kuwashauri watu kuhusu maisha. 😂
Kumbe naye mwenyewe alikuwa bado anahitaji ushauri.
Hapo ndipo nilipoanza kuona tatizo kubwa tulilonalo kama wasomi:
Tunasoma sana, halafu tunataka kuanza maisha tukiwa makocha kabla hata hatujacheza mechi.
Degree inakupa foundation, lakini haiwezi kukupa automatically experience ya ku-manage watu, biashara, fedha, pressure na failure.
Wakati mwingine si vibaya kuanza chini.
Fanya kazi kwenye kampuni ya mtu, jifunze industry, observe management, fanya mistakes ukiwa kwenye system, jenga network, elewa numbers, halafu ukifika wakati wa kuanzisha kitu chako, unaingia ukiwa na experience ya uwanjani.
Usikimbilie kuwa kocha kwa sababu tu umehitimu chuo.
Kwanza cheza game.
Jifunze game.
Pitia magumu ya game.
Ukishajua game vizuri, ndipo ukaanze kuwafundisha wengine. 😂