Tatizo liko kwa chini lakini juu naona liko sawa

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,014
Reaction score
6,834
1626413045360.png
 
Mkuu mdada kapata pancha- ilete sasa kenye maisha yetu ya kila siku-FIKIRIA TU
Naona kiongozi wa juu yuko sahihi kwa kuteua na kuwapa maagizo jinsi ya kuhudumia wanachi,lakini wanamuangusha!au sivyo?!!!
 
Weye hapo ndiyo umeishavalia kibwaya na njuga kabisaaa, mamaako anapiga manyanga
Mkuu wala- picha hiyo inaonyesha tukio la kawaida katika maisha yetu- inahusu maisha yetu- FIKIRI TU MKUU UNAPATA UTAKACHOPATA
 
Naona kiongozi wa juu yuko sahihi kwa kuteua na kuwapa maagizo jinsi ya kuhudumia wanachi,lakini wanamuangusha!au sivyo?!!!
Umejiuliza kama anayepigiwa simu akimjibu mdada aendelee na safari- itawezekana?
 
Mara zote kulielewa tatizo vizuri inasaidia kupata suluhisho sahihi.

Hapa hata anaepigiwa simu inabidi ahoji maswali ya ziada kupata uhalisia wa tatizo.

Hauwezi kumlaumu mpiga simu moja kwa moja, yeye anaona tair juu iko sawa ila chini ndio imebonyea. Hapo sasa ndio utofauti unapoanzia, kufikiri sahihi na kujiuliza maswali sahihi ili kulielewa vizuri tatizo. Hapo shida ni upepo umepungua, inaweza kuwa pancha au unatoka kidogokidogo kwa valve.

Anaepigiwa simu asipoelewa shida atapendekeza suluhu isiyofaa kutatua tatizo.

Ni sawa na ukienda kwa daktrari ukamwambia unaumwa kichwa wakati jino ndio linakusumbua. Itachukua kazi ya ziada kukuuliza maswali hadi kuja kupata uhalisia au chanzo cha tatizo. Asipofanya hivyo unaweza kupewa dawa za malaria au maumivu na bado jino lisiguswe.
 
Mkuu asante kwa mchango wako- haya ndiyo maisha yetu- je tunatambua, eleza na kutoa majibu sahihi ya matatizo yetu yanayotukabili?
 
Back
Top Bottom