Tatizo linalotokana na kukua shughuli za Bandari: Barabara za Kurasini, Mandela, Chang'ombe, Mbagala hazipitiki

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Kila masika na mbu wake, lakini mbu hawa wa kukua sana shughuli za Bandarini, Serikali ijipaange kutatua.
Mizigo na shehena za bidhaa zinazoteremshwa Bandarini zimekuwa nyingi mno.
Miundombinu ya barabara za kutoa mzigo na kupeleka mzigo bandarini limezua tatizo kubwa la barabara kuelekea Bandarini kutopitika kwa kiwango kikubwa.

Barabara ya Mandela tokea Bandarini, hadi maeneo ya machinjio Chang'ombe huwa inakuwa na jam kubwa
Barabara ya Kilwa tokea Mbagala hadi Rangi Tatu napo foleni kubwa ya malori
Barabara za Chaang'ombe karibu zote zina magari mazito yanayofunga njia
Barabara ya Mandela ndio karibia yote hadi Ubungo ni malori matupu.

Kuna haja kubwa kwa serikali kupitia Wizara zake za Uchukuzi na Ujenzi kuliangalia hili tatizo kwa jicho la tofauti.
Reli iliyopo haitumiki kikamilifu kutoa mizigo Bandarini.
Pili kuna haja ya kujenga barabara mahsusi kwa ajili ya Bandari
Ni wazo tu!
 
Niliandika uzi humu miaka 3 iliyopita na kutoa mapendekezo nini kifanyike! Ni vile tu tunaongozwa na vilaza

Angalia hapa👇
 
Kumbe wewe ndo ulishauri ikaletwa DP World. Hongera sana kwa uzalendo wako.
 
Ukiwa msomaji na mfuatiliaji wa JF humu utapata mawazo mazuri sana ambayo yakifanyiwa kazi vizuri nchi yetu inaweza kuongoza kiuchumi Afrika nzima.

Ni vile tu tuna Viongozi vilaza ila unaweza kuwa Rais nchi hii na ukaongozq nchi kwa mawazo ya wana JF na ukawa the best performing President ever nchini mwetu.
 
Kuna mawazo mengi tu humu huwa yanafanyiwa kazi.
 
Fursa ya sekta binafsi kujenga bandari kavu au tupeleke mali kwenye mfuko mkubwa wa hazina
 
TRC ilibidi wawe wamechangamkia hiyo fursa zamani sana, jenga bandari kavu morogoro au dodoma malori ya mikoa ya kusini na kanda ya ziwa yaishie huko yote
Hakuna ulazima wa kujenga bandari kavu Morogoro sababu Ruvu maeneo ya Kwala (Vigwaza kwa ndani) serikali ya Tanzania awamu ya tano imejenga bandari kavu kubwa sana. Sidhani kama imejeaa, Rwanda pia kama sikosei walipewa eneo huko huko wajenge bandari kavu.
Reli ya kati na SGR zote zimefika hapo Kwala. Kilichobaki ni uendeshaji na usimamizi tu matumizi ya reli na hiyo bandari kavu.
 
It is an urgent matter that calls for an immediate and emergency solution. The queuing and congestion significantly affect our development endeavors and costly to the general wananchi. We can fast track kwala to decongest Dar and ease traffic around Kilwa for economic and social good.
 
TRC ilibidi wawe wamechangamkia hiyo fursa zamani sana, jenga bandari kavu morogoro au dodoma malori ya mikoa ya kusini na kanda ya ziwa yaishie huko yote
Iko kwenye mchakato vuta subira...
 
Kila masika na mbu wake, lakini mbu hawa wa kukua sana shughuli za Bandarini, Serikali ijipaange kutatua.
Mizigo na shehena za bidhaa zinazoteremshwa Bandarini zimekuwa nyingi mno.
Miundombinu ya barabara za kutoa mzigo na kupeleka mzigo bandarini limezua tatizo kubwa la barabara kuelekea Bandarini kutopitika kwa kiwango kikubwa.

Barabara ya Mandela tokea Bandarini, hadi maeneo ya machinjio Chang'ombe huwa inakuwa na jam kubwa
Barabara ya Kilwa tokea Mbagala hadi Rangi Tatu napo foleni kubwa ya malori
Barabara za Chaang'ombe karibu zote zina magari mazito yanayofunga njia
Barabara ya Mandela ndio karibia yote hadi Ubungo ni malori matupu.

Kuna haja kubwa kwa serikali kupitia Wizara zake za Uchukuzi na Ujenzi kuliangalia hili tatizo kwa jicho la tofauti.
Reli iliyopo haitumiki kikamilifu kutoa mizigo Bandarini.
Pili kuna haja ya kujenga barabara mahsusi kwa ajili ya Bandari
Ni wazo tu!
Waanze kutumia miundombinu ambayo imeshaandaliwa ya Bandari kavu ya Kwala huko Mkoa wa Pwani
 
Mkuu wewe mmoja wa watu msiolielewa tatizo, kama wanasiassa wetu walivyo.
Sasa hizo containers to bandarini zitaruka kama ndege kuelekea Bandari Kavu Kwala, au meli zianze kusafiri nchi kavu kuelekea huko Kwala?
 
Mkuu Bandari ya Kwala imekuwa linked na SGR, na Mwezi wa 12 walisema behewa za mizigo za awamu ya kwanza ziliwasili. Hivyo SGR ianze kubeba shehena kutoka Bandarini kwenda Kwala na malori badala ya kufika Dar yaishie vigwaza yaelekee kwala kuchukua shehena mbalimbali.

Kuna link ya habari ya leo hapa naambatanisha. (kama hii link haitaondolewa)
 
Nimekuelewa mkuu, pamoja na hiyo link juu ya mabehewa yaliyokwisha kufika by 10th March 2025.
Nimepita barabara hizo nilizoainisha majuzi(last week) na hakuna cha mabehewa mapya ya mizigo wala ubebaji wake toka Bandarini.
Kwanza kwa freight serrvices kuanza lazima pawepo na Marshalling Yard ndani ya Bandari, na hatujui kama ipo au ndo inajengwa.
A marshalling yard, also known as a classification yard, is a railway yard where rail cars are sorted by destination and assembled into trains. It is a fan-shaped network of tracks and switches where incoming freight trains or cars from local shippers are sorted and made up into trains for their respective destinations.
 
It is an urgent matter that calls for an immediate and emergency solution. The queuing and congestion significantly affect our development endeavors and costly to the general wananchi. We can fast track kwala to decongest Dar and ease traffic around Kilwa for economic and social good.
I couldn't agree more.
You have said it all.
 
Back
Top Bottom