Tatizo linalotokana na kukua shughuli za Bandari: Barabara za Kurasini, Mandela, Chang'ombe, Mbagala hazipitiki

Tatizo linalotokana na kukua shughuli za Bandari: Barabara za Kurasini, Mandela, Chang'ombe, Mbagala hazipitiki

Bandari ya Dar es Salaam imebeba mzigo mkubwa wa biashara za kimataifa, jambo ambalo linaweza kusababisha msongamano, ucheleweshaji wa huduma, na gharama kubwa za uendeshaji. Kama bandari nyingine za Tanzania kama Bagamoyo, Tanga, Mtwara, na Lindi zingepangiwa majukumu kulingana na kanda au aina ya mizigo, ingeweza kupunguza mzigo huo na kuongeza ufanisi wa biashara.





Mfano wa mgawanyo wa majukumu:


1. Bandari ya Dar es Salaam – Iendelee kushughulikia mizigo ya kimataifa kwa kiasi, lakini kwa kupunguza msongamano kwa kusambaza sehemu ya mizigo bandari zingine.


2. Bandari ya Bagamoyo – Ikiwa ni bandari yenye eneo kubwa, inaweza kushughulikia makontena makubwa na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji wa mizigo mikubwa.


3. Bandari ya Tanga – Inaweza kuhudumia zaidi biashara ya Kaskazini mwa Tanzania na nchi jirani kama Kenya na Uganda.


4. Bandari ya Mtwara – Iwe kitovu cha usafirishaji wa makaa ya mawe, gesi asilia, na bidhaa za kusini mwa Tanzania.


5. Bandari ya Lindi – Inaweza kuwa maalumu kwa shughuli za uvuvi, gesi
Vyovyote vile
Kuhusu msongamano wa magari kwenye barabara zile utatuzi wake ni ujenzi wa Barabara za Mandela, Kilwa na Ubungo hadi Kibaha kwa njia 6 hadi 8. Hili liambatane na ujenzi wa commuter trains kwenye njia hizo za barabara. Pia mradi wa ujenzi wa barabara ya Maroli hadi Chalinze ufufuliwe n ijengwe.

Kwa efficiency ya Bandari na kukua kwa biashara, ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo( kwa gati si chini ya 40) unaoambatana na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya reli na barabara pana kuunganisha bandari hiyo na mkoa wa Dar na mikoa mingine ndo suluhisho la kudumu.

Bandari ya Tanga inaweza kuwa designated kwa shughuli za upakuaji na usafirishaji wa Gesi/ Mafuta tu huku Bandari ya Mtwara ikiwa designated kwa shughuli zingine.
 
Back
Top Bottom