Tatizo lolote la PC/device

Ndio mkuu. Imegoma. Yani hata nikipeleka ule mshale kwenye folder bila ku clik inajifungua yenyewe. Tena zaidi ya mara moja yani. Yani folder moja linajifungua hata zaid ya mara 10 tena kwa speed
Vip kuhusu virus, na je unaweza kufanya windows restore kutokea mwanzoni?.
 
Pc yangu kuna muda charge inaingia pia muda mwengine aingii shida nin
okay hapo kunaweza kuwa na matatizo mawili na yote yanaweza kuwa ni tatizo so ukitaka kujua tatizo hasa ni charger au battery fanya hivi

Tumia Pc bila battery yan weka charger tu uone kama PC itawaka muda wote na ufanye hivyo hata siku mbili kama ikizima na umeme upo bado basi charger ina tatizo, ila isipofanya hivyo ujue kabisa battery limefikia muda wake wa kuishi.
 
mkuu hapo wa msaada wa haraka naweza kukusaidia njia moja uifanye kabla ujaagiza maana inawezekana ikawa battery ni nzima bado'
kama unaweza jaribu kufungua alaf cheki hiyo cable ya battery maana nimeona ipo cable moja tu, toa battery alaf tumia pc kwa charger kama nusu saa hivi kisha baadae fungua pc tena toa cmos battery kama dk hivi alaf rudisha battery na CMOs alaf chomeka pc kwenye charger bila kuiwasha kama dk 10 kisha iwashe bila charger ikiwaka chomeka charger tena, inawezekana tatizo likawa limeisha.

utatupa mrejesho.
 
SAMAhani bro una roho ngapi?? je ni ke au ni me?......babu yako alikuwa chif au kawida tu?
mkuu mimi ni me, na nina roho moja tu kuhusu uchifu hatujawahi kuwa nao kwa jinsi ninavyofahamu ukoo wetu
Nahamini kama mtu una uelewa wa kitu mambo kazaa sio mbaya kusaidia wenzako, kwa sababu jamii forums humu mimi pia nimejifunza mambo mengi pia bila gharama yoyote labda bundle la internet tu, na kusaidiana sio lazima upate pesa ndio umsaidie mwenzako muda mwingine unaweza kumsaidia mtu pia nawewe mambo yako yakawa yanasonga.
 
CPU inawaka, lakini sekunde chache inazima,nini tatizo????
japo ujaelezea vizuri tatizo ila naweza kukusaidia kwa haraka, cheki vitu hiv vifuatavyo,
charger unayotumia,
vipi kuhusu umeme wa hapo unaotumia ,
na kama ni laptop cheki battery kama unatumia battery muda mwingine,
na muda mwingine inawezekana ikawa processor inachangia, au motherboard kwa ujumla.
 
maelezo ni kuwa ukiwasha, inawaka then inakaa secunde chache inazima
 
maelezo ni kuwa ukiwasha, inawaka then inakaa secunde chache inazima
Sawa umecheki vitu nilivyokwambia??
Na je hiyo laptop ni aina gani na tatizo limeanza hadi sasa lina muda gani?
 
samahni mkuu pc yangu baadhi ya app inashndwa ku run kwa usahihi mfano app ya dev c++ nkirun mda mwngine inanambia app pamission denied au ina run ila haifany kitu nnachotaka pia nkitaka kupga window mpya nkiweka flash ya window inagoma kuwaka
 
samahni mkuu pc yangu baadhi ya app inashndwa ku run kwa usahihi mfano app ya dev c++ nkirun mda mwngine inanambia app pamission denied au ina run ila haifany kitu nnachotaka pia nkitaka kupga window mpya nkiweka flash ya window inagoma kuwaka
mkuu hapo tatizo kubwa linawezekana kuwa ni hiyo dev++ na sio system yako, na kusolve fanya njia hii inawezekan ikakusaidia,

ukiona kama imekuandikia permission denied
fugua Task Manager ichek kwenye Running alaf fanya kui-kill exe yake.
 
limeanza ghafla tu, ni desktop, hp compaq
okay kama ni desktop kuna uwezekano mkubwa wa overheat kwenye CPU yako, Fanya hivi vitu vifuatavyo
Fungua Cpu yako kisha isafishe kwa dust blower alaf fungua sehemu inayokaa Cpu chip kunakuwaga na Paste kwa juu ya Cpu chip uwa inasaidia kupunguza overheating kwenye Chip ambapo pia inafanya kazi pamoja na feni kwa ujumla, kama imeganda sana inabidi uibandue kisha upake nyingine ( unaweza kwenda kununua maduka yoyote yanayouza vifaa vya computer uwa wanakuwa nazo unaulizia Heat sink Paste utapata)
baada ya hapo funga Pc tumia kama kawaida na tatizo litakuwa limekwisha.
 
inauzwa bei gani???
 
Habari kiongozi.. Pc ya sistaangu ilizima tu ghafla wakat wanachek movie tangu hapo haiwaki tena. Ukichomeka charger haionesh kama inachaj ila kanawaka kataa keupe tu kanawaka na kuzima. Naomba nisaidie kujua shida itakuwa nn Pc Ni HP Intel core i3
ProBook 4430s
 

Mkuu hapo Tatizo ni battery limeisha kabisa au limegoma kucharge kabisaaa, jaribu kufanya hivi chomoa battery kisha jaribu kuwasha bila battery uone kama itawaka, kama ikiwaka izime alaf, fanya hard reset ya HP ( chomoa charger, chomoa battery, Toa CMOS battery, kisha shikilia button ya kuwashia kwa sekunde 10 hivi, japo CMos battery sio lazima sana pia)
Kama isipowaka jaribu na charger nyingine ambayo inatoa umeme sawa kwaajili ya Pc hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…