Huo ni ushahidi kuwa kilichotangazwa juzi na tume ya uchaguzi, sio kilichokuwa kwenye box la kura. Hivyo wanajua fika wananchi wanawasikiliza waliowachagua, na sio waliotangazwa washindi.
Mtaani kwetu kuna mtendaji alipita kwenye ule uchaguzi wa kihuni wa SM, ameitisha mikutano mara 2, anapata watu wachache sana mpaka anaahirisha vikao!
Hiyo yote ni kwasababu hana uhalali wa umma bali yuko kisheria. Ukiona ccm wanalazimisha viongozi wachache wa upinzani washiriki kwenye vikao vya madiwani na ubunge, ni kutaka kulazimisha uhalali kwa umma, baada ya kunajisi uchaguzi.