Tatizo si Kikwete na uelewa wake bali chuo kikuu alichosoma!


Ni kweli kabisa. Hata hiyo ranking haisemi chochote kuhusu ufundishaji. To my knowledge vyou vinakuwa ranked sana sana kutokana na idadi ya research wanazofanya. Na kama tujuavyo research za UD zinazowapa chart ndo hizo za Redet na bans and banner zinazotolewa monthly. Kwa SUA I have no objection with the quality of their researches.
 
Base ya ranking unaijua lakini? Ni research, na kwa UD research nyingi ni za REDET. Una la kusema hapo. Tunaongelea ufundishaji na si research za kisisasa ambazo zinakuwa published monthly.

 

Mzee,

Hata sijajua lengo lako ni nini! Hivi Hayati John Garang na Kaguta Museveni walisoma wapi vile? Na shivji je alisoma wapi? Tundu Lisu?

UDSM imetoa viongozi wazuri sana na imetoa mchango mkubwa kwa nchi. Hivi Spika Anna Makinda alisoma wapi vile?
 

Anna Makinda ni product ya Mzumbe, si unaona maamuzi yake yalivyo ya kubabaisha? Mara oo thibitisha, mara oo kwa maandishi tena lete ofisini kwangu. Nini Bana........................
 
Base ya ranking unaijua lakini? Ni research, na kwa UD research nyingi ni za REDET. Una la kusema hapo. Tunaongelea ufundishaji na si research za kisisasa ambazo zinakuwa published monthly.

Umesaidia sana! hivi vyuo anavyosema bwana Papa viko wapi kwe orodha hii?
 
Anna Makinda ni product ya Mzumbe, si unaona maamuzi yake yalivyo ya kubabaisha? Mara oo thibitisha, mara oo kwa maandishi tena lete ofisini kwangu. Nini Bana........................

Asante bwana,

Nilitaka papa D. ajue hilo
 

Papa D, Wewe ulisoma wapi?
 

Teh teh, hizi research zingine za JF noma..

Tunaomba utupe methodology uliyotumia!sample size yako.

Ukipigwa na maumivu ya maisha kwa sababu ya JK usikurupuke kufanya conclusion za ajabu.
 
Kila mwanafunzi anayemaliza Form Six hapa Tz huwa ana ndoto za kusoma UDSM (kitovu cha elimu Tanzania). Wale wanaokosa chance ya kupita kwenye yale ma-corridor (kutokana na points kutotosha) mara nyingi hujenga chuki dhidi ya wana-UDSM. Mwenendo wa thread hii unajidhihirisha wazi. Nakumbuka hata miaka ya nyuma kulikuwa na malumbano sana baina ya wana-UDSM na iliyokuwa IDM Mzumbe. Wale wa Mzumbe, enzi hizo wakisoma Advanced Diploma walikuwa wanadai ni sawa na first degree! Lakini kilichokuwa kinatokea ni kwamba hawa wa Mzumbe wakiomba kufanya masters wanaambiwa wasome kwanza first degree.
 
hivi kama Walioba alikuwa amefoji PhD yake pamoja na wengine pale Mzumbe ambao wamefutiwa. hivi athari yake ni nini kwa waliokuwa wanasimamiwa na watu hawa?
na hivi PhD nyingine feki ukizifuatilia zimetolewa Mzumbe. nisingependa kuwataja wahusika wake
 

unasemaje kwa degree ambazo zipo UDSM na hazipo MZUMBE?
degree nyingi za Mzumbe ni za usanii kama Accounting, business management, public administration nk
 
Ukweli ni kwamba kwa Tanzania UDSM ni mambo yote, lakini swali linakuja jee UDSM inamuandaa mtu kuwa critical thinker? Jee UDSM imetoa mchango kubwa kwa taifa ukilinganisha na fund inayopokea kutoka kwa taifa la Tanzania?

Those are critical questions that a Tanzanian society need to digest. Mwalim alisema kuanzishwa kwa UDSM lazima kuwe chachu ya kuzalisha independent thinkers. Jee is it still valid kwamba UDSM produce independent thinker?

The argument can go both ways, unaweza kusema yes UDSM ndio imezaa kina Dr. Shivji, Tundu Lisu and many more. Vile vile unaweza kusema UDSM imetuletea JK, Masha na wengine. All this arguments are based on Political leadership.

However, the question stand kwamba ni kwa jinsi gani UDSM imesaidia Tanzania society kwa research and development, ujasilimali and generation of ethical leaders?
Mimi ni moja wa wale wanao support kwamba mitaala ya chuo kikuu cha Dar es salaam inabidi ibadilishwe, kutoka kwenye exam based system kwenda kwenye combination ya mitiani na kufikiria nje ya kisanduku. Instead ya wanafunzi kuamini kwamba wao ndio cream ya nchi, wanatakiwa wajue kwamba wao ndio wanatakiwa wakazalishe kazi, wao ndio wanatakiwa wakatoe opinion zao kwenye sehemu mbalimbali za jamii ya Tanzania.

Kuendelea kwao kula bia na kuponda starehe kwa pesa za walipa kodi nadhani ni uwazimu. Nimezungumzia UDSM pekee sababu nimekua ndani ya chuo, nilibahatika kuchaguliwa kwenda kusoma even though i chose something else.
 
We elimu ulosoma sijui inakusaidiaje, maana vitu unovoongea ni kama failure flan, i doubt ur sense :A S 20:
 
it's useless arguing with a fool(here is referred as papa D)..as i shall be a fool than himself..am just a passer-by...
 
Jamani ukweli ni kuwa vyuo vyote wanakariri, ila udsm kidogo ndoo wamezidi. Japo in certain demain ni wazuri. Mzumbe ndoo kabisa jugement capacity bado. Kwa ujumla E;imu tanzania bado ya kizushi sana. Tatizo ni kujisahau. Research lab ni mahali pa kutafutia miradi ya kupatia fedha. siasa zimezidi. Hawataki kujifunza. Hivyo mkwere hata angesoma Sua, Mzumbe DIT bala linge kuwa palepale kwani hakuna aliye mwema.
 
jamani, tatizo linaweza kuwa sio ubovu wa UDSM, nadhani ni suala la zima la mfumo wetu wa elimu, tusitegemee kuwa eti tofauti ya utendaji wetu itarekebishwa kwa miaka 3 uliyospend SUA, Mzumbe , UDSM etc. ukosefu wa uzalendo na ubunifu ktk mafunzo yetu ni tatizo sugu! Afu tanzania imekuwa na chuo kimoja hadi 1984, tukawa na SUA, then Open 1994 hivyo wazee wote tulio nao walio soma miaka ya 80s backwards they are bound to be UDSM graduate kama hawakwenda nje. Na je hao wa nje how different are they?

suala la vilaza ni la kitaifa, nchi ina watu milion 43 na zaidi graduate hawafiki laki, nini cha kujisifu? ni tatizo hilo tunaishia kuchagua maraisi wabovu, mawaziri hadi ma VC feki, maprofessor wasioweza kusimamia hata hoja za kitaaluma eti wanafuata matakwa ya vyama vyao! Hizo ndo cream mnazotaka kujisifia nazo?
 

Mkuu, nafikiri hiyo red kama ilisoma UDSM then ndo sababu ya kusema yote hayo.
Sema alichokosea ni kugeneralize, otherwise wapo mabogus wengi tu, mifano ipo mingi tu:A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20:
 
Alosema kuna vyuo vina wanafunzi elfu 10 (10,000) duniani ajue kuwa bado ratio ya student lecturer ni kubwa nina maana wana lecturers wengi pia na hakuna anayesahihisha essay 3000. Na ujue technolojia ahisahihishi essay leave aside the fact that we don't have softwares za ku detect vitu kama plagiarism in any university in TZ. Mwisho wa siku walimu sijuhi ndo mnawahita lecturers hawasahihishi na wanafunzi wanakuwa demoralized na ni kureproduce kazi za watu kwenda mbele. Mimi nimesoma chuo kina wanafuni 25,000 lakini darasani tulikuwa hatuzidi 20.
 
UDSM kilikuwa chuo kizuri sana kilichotoa elimu nzuri sana miaka hiyo, at least hadi mwaka 1990. Sielewi miaka ya karibuni kwa vile kumekuwa na uongozi wa kibabaishaji na siasa zimekiingilia sana. Ni muhimu kufahamu kuwa katika msafara wa mamba, hata Kenge pia wamo, kwa hiyo tukifuata standard performance ya 2-sigma, katika kila graduate 100 wa UDSM kutakuwa na vilaza (kenge) kama watano hivi (wanaitwa outliers), na hiyo natural process inatokea duniani kote. kwa hiyo basi siwezi kushangaa kuwa huenda Kikwete alikuwa ni mmoja wa wale 5% outliers!!!.

UDSM ndiyo imeinua vyuo vingine vingi sana hapo Tanzania kwa kufundisha watu ambao ndio wamekujwa kuwa maprofesa wa vyuo hivyo: SUA, MU, SAUT, UDOM na vingine vingi tu. Haiwezekani wao wawe vilaza halafu eti wakawafundishe vipanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…