Tatizo si Kikwete na uelewa wake bali chuo kikuu alichosoma!

Tatizo si Kikwete na uelewa wake bali chuo kikuu alichosoma!

wewe umesema kweli kabisa na kuonesha kuwa una uwezo mzuri wa kufikiri

quote_icon.png
Originally Posted by Limbani
Kaka you are WRONG, huwezi fananisha wanafunzi wa UDSM na Mzumbe...



Kulinganisha anaweza,lakini kosa kubwa alilolifanya ni kugeneralise the subject matter!kila chuo huo kinatoa defective products and by products,hili ni jambo la kawaida hata katika viwanda vinavyozalisha bidhaa​
 
Ukweli ni kwamba wahitimu wengi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam ni vilaza/wababaishaji [Si kikwete tu!]. Hii inatokana na jinsi wanavyofundishwa [wanakaririshwa na si kueleweshwa] watu wa aina hiyo huishia kuwa wenye nadharia nyingi kuliko utendaji. Mwisho wa safari huwa walalamishi wazuri sana. Chanzo kikuu cha kutoa vilaza ni kwamba Walimu/professors wa mlimani wamejaa wivu na husda!!!

Mwanafunzi aliyehitimu Mzumbe au DIT ni bora kuliko mhitimu wa Mlimani!! POLENI SANA WAHITIMU WA MLIMANI!!

Papa D,

Kwanza nakushukuru kwa changa moto uliyotupa kufikiri vilevile nakuomba utuombe radhi wanaUDSM kwa kudai kuwa maprofessor wetu UDSM wamejaa wivu na husda (kwani hujatuambia wala kutupa data vipi umefikia katika conclusion hiyo).

Tuje katika hoja yako hebu tuambie ufahamu wako wa nini utendaji na ubora wa ufanisi wa kazi. Kama ni kwa kuspecialize katika kitu kimoja ukawa kihiyo vyengine basi naweza kukubali lakini fahamu kuwa specialization katika Advanced Diplomas na Degree ni vitu viwili tofauti. Sasa inawezekana hao unaofanya nao kazi pengine walikuwa hawafahamu tricks zote za utendaji basi wewe ukakimbilia kugeneralize tu.

Mkuu Generalization haijengi bali inabomoa kila la kheri!!!
 
  • Kuna baadhi ya wanafunzi wanamaliza VETA ni bora kuliko wale wa mlimani,SUA DIT. IFM na hata mzumbe.
  • Kuna wanafuzi wanamaliza mlimani,SUA DIT. IFM na mzumbe wanakuwa bora kuliko wenzao wengine
  • Kuna baadhi ya wanafunzi wa vyuo wako kwenye career ambazo hawakuzipenda basi tuwanasomakama fashion.
  • Kule UK kuna aliekuwa waziri waziri wawa mambo ya ndani wa chama cha labour aliishia darasa la Nne. anaitwa andy johnson
  • Chenge kasoma havard,
Kwanza Inategema mwanafunzi na mwnafunzi. na pili na tatizo ni siasa za tanzania. mfumo wa siasa tanzania ulivyo unachochoea wanasiasa kuwa vilaza.

Ukifundishwa na kufaulu hesabu 2+2 = 4 au probalility au statistics haitakusaidia kwenye maisha kama hutajua wapi na vipi zinatumika kwenye maisha na kazi


Baadaya kumaliza chuo kinchomfanya mwanafunzi mmoja tofauti na mwingine ni

  • creativity na inovation
Kuna wanfunzi wengi wamemaliza vyuo wako makazini hawajawai kuandika paper yeyote ya ushauri maofisini kwao. paper yao ya mwisho kuandika ni project waliyofnya chuoni.

Kuna wanafunzi hawezi kuandika memo. kuandika offficial memo iwe ni kwa kiswhaili au kingereza inamchukua zaidi ya masaa.

Wahasibu ,mwanasheria, maengineer etc wenye degree ni aibu kila siku ofisini tunasubiri tu tuambiwe ufanye nini as if hakunakitu ambacho unaweza kupendekeza kifanyike vipi kuongeza ufanisi na utendaji.

Wengi tu hapawasomi kuwepo au kutokuwepo kwetu ofisni hakuna impact yeyote kubwa . sababu hatuna mawazo mapya. ni kama marobot. liko programmed

Very shame sio tu wa UDSM but vyuo vyote.
 
Ni kweli kabisa watu waliosoma mlimani ni vilaza wa kutupwa na ndo viongozi wetu wengi sana wamepita hapo na angalia nchi walipoifikisha.

Your observation leaves alot to be desired; je mawaziri wakina Nchimbi, Mkullo nao wamesoma UDSM?
 
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?

hiyo ndo inayowaponza kujiona wao ni cream then wanaishia GPA za mbili....... chuo kikuu hakuna cha kusema ulikwa cream wala mtindi wote mnaanza upya....
 
bring it on, bring it on! heri siye tulioishia darasa la kanumba!
 
tatizo si mtu ila ni itikadi zilizomweka hapo alipo imean madarakani
 
Ningeweza kuongezea hapo kwamba matatizo ya jk ni pamoja na hilo la chuo pili kabila na mazingira aliyolelewa kiuongozi ni mwimba taarabu tu
Natambua mvutano utakuwa mkali ila ukweli unabaki palepale tu kwa udsm ni pango la vilaza si watu makini hata kidogo they lack sense of leadership
 
cjakubaliana na wewe, na sitaki kukubaliana na wewe, ukweli uko wazi hata wewe unajua, mzumbe na kweingineko wanapelekwa watu wa lio na alama ndogo kwa lugha nyingine, wamefeli.kuhusiana na ukilaza wa jk, nakushauri urejelee Class aliyotoka nayo ambayo prof moja aliwahi kucoment kuwa ' he passed here'' kwa maana kwamba alipita hapa na hakuwahi kusoma. kwa hiyo hizo ni weakness zake mwenyewe na hazina uhusiano na chuo hiki kikuu.
 
mwanzisha thread hii, sijasoma UD lakini hujawatendea fair wasomi wa pale...

vilaza wapo, na wazuri wapo pia kila sehemu...

ishu ni kwamba mkwere was a weak student since then...

alipasi kwa gentlemans pass. hivyo hata walimu wake walikuwa fair!
 
Kwa weakness yake ishaonekana, its better tusibishane nae... Tumuacheni aendelee na mtizamo wake wa uongo kuwa magraduates wa UDSM ni vilaza.... Hajui kwa kufanya hivyo anapingana na dunia yenye utaalamu mkubwa kwa utafiti wa mtindo huo... Dunia inatambua kuwa UDSM ni chuo bora Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika pia.... Acha kuleta topic zisizo na maana yoyote, tuna mambo mengi sana ya kujadili na sio hilo unalolitaka wewe.... Udhaifu wa JK ni wake yeye na sio udhaifu wa wanafunzi wote wa UDSM... Inavyosemekana JK hakuwa na lolote darasani, ni kati ya watu waliopata maksi za chini sana kwenye mitihani yao!? JARIBU KUFIKIRI KABLA HUJAPOST
 
mmemshambulia mwanzisha thread kishabiki zaidi (wana UDSM vs vyuo vingine) labda kwasababu mwanzisha thread alimalizia kwa kusema Mzumbe/DIT ni bora ..hapa ndipo alipokosea lakini changamoto aliyoitoa hapa ni ya kweli kabisa. Elimu yetu hapa Tanzania inatengeneza marobot tuu na watu wa ku copy and paste. Angalia majengo yetu, barabara zetu, utendaji wetu wa kazi, marketing, customer care, biashara, etc etc ubunifu zero ni copy & paste. Tumeshindwa kuendesha mashirika yetu mpaka watu kutoka nje waje kutusaidia kuyaendesha...tumebaki kuwa taifa la wachuuzi tuu tusioweza kutengeneza hata toothpick wakati miti imejaa.

hapa tumebaki kutupiana maneno oo chuo nilichosoma mimi ni bora kuliko ulichosoma wewe what a waste of time and server space!
 
Wakuu nimefatilia michango mingi lakini kwa uzoefu wangu tatizo sio udsm ni mfumo wa elimu ya tz ambayo ni ya kukariri na tena udsm wanajitahidi mara nyingi sababu wengi wanahistoria nzuri ya shule toka awali na hivyo ubora wao ni sababu walishazoea kupiga msuri bila kutegemea sana lecturer na sio kwamba chuo ndio kinatoa elimu bora na hata vilaza waliopo ukifatilia historia zao za awali si nzuri sana kitaaluma.ndio maana kama kuna mtu ameshafanya kazi na watu waliomaliza tu form six na kufanya professional examinations mpaka ku graduate CPA (kwa uhasibu) huwa wana uwezo mkubwa sana sababu mitihani yao ilivyo huwa force kusoma sana vitu vingi.nafikiri hasa sababu ni mfumo mbovu wa elimu yetu kutomfanya mtu kuweza kufanyia kazi aliyosoma.pia tunapotoa michango yetu tusi generalize sababu kila course inatofauti kimalengo,namna ya ulunganifu wa graduates hivyo si sahihi kusema kwa ujumla tu kuwa graduates wa udsm ni vilaza.Udsm ni chuo kikongwe,chenye mchango mkubwa sana hapa tz na ndio chemchem ya fikra ila tukizungumzia changamoto za elimu ya tz hatuwezi kukikwepa
kwani tutakuwa hatuwatendei haki wanaosoma na watakaosoma pale.tusibeze wanataaluma bali mfumo wa taaluma yetu inahitaji marekebisho makubwa.
 
Kauli yako ina mapungufu ya aina mbili; kwanza ina mtizamo mgando. Ubora wa wahitimu katika miaka zaidi ya arobaini ya uhai wa chuo hicho, umekuwa ukihitirafiana siyo tu kwa fani moja na fani nyingine, lakini pia kwa mwaka hadi mwaka. Pili, kimsingi inalinganisha vitu viwili vilivyo tofauti. Katika hali halisi, wahitimu wa vyuo vya DIT na Mzumbe tangu mwanzo ilikusudiwa wawe watendaji (technitians), wakati wale wa mlimani walitegemewa wawe waratibu (coordinators). Ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana baada ya kuhitimu DIT na Mzumbe walikuwa wanapewa diploma na mlimani digree. Tofauti kati ya diploma na digree, ni kwamba mtu wa diploma anazama zaidi katika eneo dogo, wakati mtu wa digree anafundishwa kwa lengo la kuwa na uelewa kwa maeneo mengi, ili aweze kuratibu kazi za wengine. Watu wengi huwa wanapotosha ukweli kwamba mtu anaweza akawa mwana taaluma tu kwa kujifunza darasani. Hii si kweli, ndiyo maana si sahihi hata kidogo kumwita JK mchumi au Pinda mwanasheria, kwasababu waheshimiwa hawa tangu wahitimu wamekuwa wakifanya mambo tofauti na fani zao.

Huyu nae amesoma UD....maneno meeeengiiii.....eti technitians.....jamani!!!!
 
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?

Hapo mwenyewe unaona umeleta booonge la Logic.....ndio mnavyofundishwa UD hivi?
 
Hii topic naona haina mashiko kabisa,..naona kama ina agenda ya siri,inataka kututoa kwenye mijadala ya maana ya kitaifa na kutupeleka kwenye mambo ya cjui ulisoma chuo gani!!,n.k.ebu tuongeleee yanayohusu muskabali wa nchi yetu kama vile mambo ya ufisadi,katiba mpya, serikali mbovu,uwajibikaji kwa viongozi, waathirika wa mabomu na majanga mengine,n.k,..lakini siyo mambo ya vyuo,vyuo ni majengo(taasisi) tu ambazo hupokea watu wa aina na uwezo mbali mbali,
 
Kwa wenye busara kutokukujibu ndio jambo sahihi. Lakini bado utakuwa haujasaidika. Unachotaka ni kuanzisha ligi ambayo itaifurahisha nafsi yako.

Hao wengi hujasema ni kina nani hivyo nikiwa uzao wa mlimani lazima nikujibu. Mimi tusi hujibiwa kwa tusi busara na hekima vinasubiri kwa muda.

Umeamua kuonyesha ujinga wako hadharani. Umeanika upuuzi wako. Umethibitisha vilaza wengi wanatokea wapi. Nina uhakika JK angekushinda darasani. Makamba mngekuwa mnapishana, term hii anakuwa wa 42 kati ya 43 term inayofuata unakuwa wa 42 kati ya 43!

najua ukweli unauma.....ila kama kweli una busara, basi either ungekaa kimya tu, au ungejaribu kujibu kwa hekina na unyenyekevu na kwa kujaribu kumuelewesha huyu jamaa kwa vipi hayupo sahihi.

ila jinsi ulivyojibu hata kama usingesema umesoma mlimani, ningehisi hivyo.

sijui umejifunza kitu kwenye hii reply yangu??....sijatukana wala kumuita mtu mpuuzi.
 
Back
Top Bottom