Anyisile Obheli
JF-Expert Member
- Dec 13, 2009
- 3,400
- 320
Ukweli ni kwamba wahitimu wengi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam ni vilaza/wababaishaji [Si kikwete tu!]. Hii inatokana na jinsi wanavyofundishwa [wanakaririshwa na si kueleweshwa] watu wa aina hiyo huishia kuwa wenye nadharia nyingi kuliko utendaji. Mwisho wa safari huwa walalamishi wazuri sana. Chanzo kikuu cha kutoa vilaza ni kwamba Walimu/professors wa mlimani wamejaa wivu na husda!!!
Mwanafunzi aliyehitimu Mzumbe au DIT ni bora kuliko mhitimu wa Mlimani!! POLENI SANA WAHITIMU WA MLIMANI!!
Ni kweli kabisa watu waliosoma mlimani ni vilaza wa kutupwa na ndo viongozi wetu wengi sana wamepita hapo na angalia nchi walipoifikisha.
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?
Ndugu;
Ningesema wote hapo ndo ningekuwa nime-generalize. lakini nimesema wengi [yaani majority]. therefore I still stand for my view!!
Kauli yako ina mapungufu ya aina mbili; kwanza ina mtizamo mgando. Ubora wa wahitimu katika miaka zaidi ya arobaini ya uhai wa chuo hicho, umekuwa ukihitirafiana siyo tu kwa fani moja na fani nyingine, lakini pia kwa mwaka hadi mwaka. Pili, kimsingi inalinganisha vitu viwili vilivyo tofauti. Katika hali halisi, wahitimu wa vyuo vya DIT na Mzumbe tangu mwanzo ilikusudiwa wawe watendaji (technitians), wakati wale wa mlimani walitegemewa wawe waratibu (coordinators). Ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana baada ya kuhitimu DIT na Mzumbe walikuwa wanapewa diploma na mlimani digree. Tofauti kati ya diploma na digree, ni kwamba mtu wa diploma anazama zaidi katika eneo dogo, wakati mtu wa digree anafundishwa kwa lengo la kuwa na uelewa kwa maeneo mengi, ili aweze kuratibu kazi za wengine. Watu wengi huwa wanapotosha ukweli kwamba mtu anaweza akawa mwana taaluma tu kwa kujifunza darasani. Hii si kweli, ndiyo maana si sahihi hata kidogo kumwita JK mchumi au Pinda mwanasheria, kwasababu waheshimiwa hawa tangu wahitimu wamekuwa wakifanya mambo tofauti na fani zao.
Kama ni chuo cha vilaza mbona huwa kinachukua cream yote, hafu mtu akikosa mlimani ndo anafikiria kwenda vyuo vingine, kwa nini?
Kwa wenye busara kutokukujibu ndio jambo sahihi. Lakini bado utakuwa haujasaidika. Unachotaka ni kuanzisha ligi ambayo itaifurahisha nafsi yako.
Hao wengi hujasema ni kina nani hivyo nikiwa uzao wa mlimani lazima nikujibu. Mimi tusi hujibiwa kwa tusi busara na hekima vinasubiri kwa muda.
Umeamua kuonyesha ujinga wako hadharani. Umeanika upuuzi wako. Umethibitisha vilaza wengi wanatokea wapi. Nina uhakika JK angekushinda darasani. Makamba mngekuwa mnapishana, term hii anakuwa wa 42 kati ya 43 term inayofuata unakuwa wa 42 kati ya 43!