TATIZO SI MFUMO WA ELIMU
Kumekuwapo na mjadala kuhusu mfumo wetu wa elimu.Tuliowengi tunasema mfumo wetu wa elimu ni mbovu na kwamba ndiyo maana vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu lakini hawawezi kujiajiri. Kelele ziko kila kona ya nchi.
Malalamishi haya hayatoki kwa wananchi wa kawaida tu bali mpaka wenye nafasi ya kufanya maamzi nao wanalalamika.Katika mjadala wa bunge hivi majuzi hoja hii pia ikaonekana kujadiliwa katika hali ya kulalamika.Waswahili husema lisemwalo lipo kama halipo laja, inawezekana lina ukweli ndani yake.
Kwa maoni yangu, naona kama tunajaribu kutafuta dawa kwa tatizo lisilo lenyewe. Ninachokiona mimi si ubovu wa mfumo wa elimu bali ni ufinyu wa fursa za ajira. Kwasababu si kila aliyejiajiri alipata elimu bora, kuna watu shule hawaijui kabisa lakini wamejiajiri.Tujiulize maswali machache hapa.
Je, tunataka kusema nchi hii haina wataalamu katika maeneo mbalimbali, madaktari na wauguzi, walimu, wahandisi, wahasibu, marubani, manaodha, wanasheria, mafundi umeme, wataalamu wa miamba nakadhalika. Kama wapo walipata elimu yao katika mfumo gani? Walisoma katika nchi gani? Walifundishwa na akina nani?
Viongozi wetu kuanzia rais wamesoma wapi? Tuna maprofesa ndo kusema nao ni matokeo ya mfumo mbovu kwahiyo nao ni wabovu?
Bila shaka jibu ni kwamba wamesoma Tanzania na mfumo wetu wa elimu haujawahi kubadilika ni uleule wa mzungu. Je ni kweli hawafai? Kama wanafaa hawa wengine kwanini waonekane wamepata elimu mbovu? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Tukikubaliana kwamba mfumo wetu wa elimu ni mbovu kiasi hicho, maana yake hata wale tunaolalamika vilevile tulipata elimu mbovu, pengine ndiyo maana tunashindwa kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wetu.Tumeshindwa kujiajiri ila tunataka vijana wajiajiri!
Tukubaliane tu kwamba, tatizo la ajira limekuwa tatizo la kidunia kwasababu ya ongezeko la watu. Jambo la msingi ni kufikiri njia sahihi ya kutengeneza ajira katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kilimo, badala ya kuwanyanyapaa vijana wetu ambao wamehitimu elimu tunayoisimamia wenyewe. Yaani ni sawasawa na wazazi kumlaumu mtoto wao kwa kuzaliwa wakati wao ndiyo walitaka azaliwe.
Vijana wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu nchini si wapangaji wa mfumo wa elimu.Tunapowalaumu kwamba hawawezi kujiajiri tunawakosea sana maana wao ni zao la mfumo huo wa elimu kama ni mbovu. Tusiwaongezee majonzi, tusiwasakame tukifanya hivyo tunaweza kujikuta tunaongeza idadi ya vijana, watakaokuwa wanatembea barabarani huku wakiongea wenyewe au hata kuwasababishia vifo vya kujinyonga kwa kukosa matumaini ya kuishi bila kazi.
Tumekazania sana kufaulisha shule za msingi na sekondari, ili waende kwenye vyuo mbalimbali lakini nafikiri hatujafikiria zaidi mahali gani watakwenda baada ya kuhitimu vyuo vya kati na vikuu. Kama tumeshagundua tatizo kwanini tuendelee kulalamika bila kuchukua hatua za kubadili mfumo wa elimu kama ni mbovu?
Tanzania hatujawa na viwanda vya kusema kila mtu anaweza kupata ajira, lakini tuna ardhi kubwa, tunayo maji ya kutosha, ziwa victoria, nyasa, Tanganyika, Lukwa, manyara, nakadhalika, pia tunayo mito ya kutosha. Juhudi gani zimechukuliwa kuhakikisha fursa hizi za ardhi na vyanzo vya maji vinakuwa ajira?
Kwa idadi yetu sasa ni wazi kwamba serikali haiwezi tena kuajiri kila mtu, kwahiyo ni busara kuweka mazingira rafiki katika sekta binafsi, ili ziweze kusaidiana na serikali kuajiri au kutengeneza fursa za vijana kujiajiri.
Uhakika nilionao ni kwamba hata kama kila mtu akaamua kusoma elimu ya ufundi au kazi za mikono, ambazo wengi tunadhani zitakuwa mkombozi, bado halitakuwa jambo rahisi kujiajiri kwasababu hakuna namna bora ya kutafuta masoko ya bidhaa zitakazotokana na kazi hizo. Ushauri wangu.Wizara ya kazi na ajira, kilimo, viwanda na biashara ni muhimu kukaa pamoja ili kutafuta majawabu ya namna ya kutengeneza fursa za ajira kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Tunaweza kuamua kama nchi, kwamba maeneo yote ya kanda ya ziwa na mito yakawa maeneo ya kuzalisha vyakula vya aina zote. Kazi hiyo ikafanywa na vijana kwa kufanya kilimo cha umwagiliaji. Wakaweza kuuza vyakula hivyo ndani na nje ya nchi kwa kutafutiwa masoko ya uhakika.
Nchi haiwezi kujiendesha kwa kodi pekee, kwasababu unawatoza fedha wasiokuwa nazo ili uwasaidie wasiokuwa nazo. Ili uwasaidie zaidi lazima uwatoze zaidi, jambo ambalo litafanya biashara zife au wengine kuamua kutofanya biashara na ikisha kuwa hivyo maana yake hali ya nchi kiuchumi itakuwa mbaya.
Kumbe inatakiwaje? Lazima kama nchi tuwe tuna malighafi tunazoziuza nje ili kupata fedha za kigeni na kuongeza thamani ya fedha yetu vilevile, lakini kutenga maeneo ya uzalishaji wa kila kitu maana yake unachochea ukuaji wa viwanda vya ndani kwasababau huwezi kuwa na viwanda bila mali ghafi hasa zinazotokana na kilimo.
Lakini tutakuwa na chakula cha kutosha ndani ya nchi, hivyo matumizi ya fedha yatapungua, yakishapungua maana yake thamani ya pesa inakuwa kubwa, yaani ukienda sokoni na pesa kidogo unanunua vitu vingi zaidi kutokana na kwamba vitu vinapatikana kwa bei rahisi kutokana na wingi wa vitu hivyo kufanya maisha ya watu kuwa rahisi na bora Kwa kila mtanzania.

Upvote
0