Watu wanapambana sana ila kinachokwamisha pia ni njia ya malipo. Kuna fursa nyingi sana mtandaoni ,unakutana nazo ila njia ya kupokea ni Paypal. Kwanini iwe Paypal?
Ni njia rahisi sana, unatengeneza account paypal, anakuwekea hela, Unatoa kwa njia ya simu, maisha yanaendelea.
Mfano.
Wewe unafanya kazi ya kuedit picha mtandaoni na kila picha moja ni 5,000 za kibongo. Sasa kwahiyo, huyo mtu kule kwenye nchi yao atoke aende western union akutumie hela yenye thamani ya shiling 5,000 za kibongo? Hiyo haiwezekani hata ningekuwa mimi siwezi.
N.B
Usilaumu watu, serikali yako inakwamisha sana watu kuwa na maendeleo. Mimi mwenyewe ni mfano hai. Paypal ingekuwa inaruhusiwa kupokea pesa na kutoa. Tungekuwa tunaongea mambo mengine