Tatizo siyo kutokufanya bali ni kufanya maamuzi

Tatizo siyo kutokufanya bali ni kufanya maamuzi

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Nadhani tunapotoka; Wote tumekuwa tukipigia kelele Mamlaka makubwa ya Rais (hilo ndio Tatizo), ndio maana nililaumu kipindi cha JPM kuamua yeye kama yeye na siyo wadau kuhusu miradi (eti Miradi ya JPM na sio ya Watanzania), au Taasisi ya Rais kufanya maamuzi ya Mahakama na siyo taasisi husika.

Ila cha ajabu wanaolaumu Awamu ya Tano hawaangalii kwamba system bado ni ileile ya Rais wa sasa kuweza kufanya maamuzi... (kwa kuachia mtu mmoja kuweza kufanya maamuzi kuna uwezekano wa maamuzi hayo yakawa mabaya).

Hata uchaguzi wa Mawaziri n.k. kama tunajua matokeo yanayotakiwa mfano nishati (ni umeme wa uhakika) sasa kweli Rais ndio anahitaji kuchagua ? Kwanini mtu asipofikia viwango/kiwango asiondoke kama vile kazi nyingine?

Kwahiyo binafsi Samia simlaumu kwa kutokufanya maamuzi (nendeni mkalitazame) bali ni pale anapofanya hayo maamuzi huenda yakawa siyo sahihi (tunaendelea kukopa).
 
Back
Top Bottom