KERO Tatizo sugu la kukatika kwa umeme Wilaya ya Mvomero huku mamlaka zikiwa kimya

KERO Tatizo sugu la kukatika kwa umeme Wilaya ya Mvomero huku mamlaka zikiwa kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wakaazi wa Wilaya ya Mvomero tunaopata huduma ya umeme kuanzia Kituo cha msamvu kuja Turiani, laini ambayo inasambaza umeme maeneo mengi zaidi ya Wilaya ya Mvomero kuanzia mkundi, halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Dakawa, Dumila, Gairo, Mvomero, Turiani, Madizini, Kibati mpaka Pemba, kuna shida kubwa sana ya umeme ambayo haijawahi kupata ufumbuzi.

Umeme unakatika zaidi ya mara 20 kwa siku, unaweza ukakatika hata mara 10 ndani ya dakika tano pekee, kinchosikitisha zaidi na kukera ni mamlaka zinazohusika kuwa kimya licha ya wananchi kupiga kelele na kupaza sauti zao bila mafanikio.

Shughuli za kiuchumi ndani ya halmashauri hii ni kama haziwezekani kabisa, ukitaka kufilisika kiuchumi weka pesa zako ndani ya halmashauri hii utajuta.

Shida haijawahi kujulikana, TANESCO wanaweza kuomba radhi hata mara kumi kwa siku kutokana na kelele za wananchi lakini hawajawahi kuja na suluhisho la kudumu la tatizo hili,

Tupo njia panda, hatujui shida ni wataalam kua na uwezo mdogo??
Au miundombinu chakavu???
Au vitendea kazi duni???
Au uwajibikaji mbovu???

Bahati mbaya meneja tanesco Wilaya ya Mvomero hajawahi hata kutoka hadharani kusema chochote licha ya wateja kupaza sauti zao usiku na mchana.

Chakushangaza zaidi mheshimiwa mkuu wa Wilaya pia anaona adha hii lakini hatujawahi kuona hatua zikichukuliwa,

Tunawaza ni nani anawalinda hawa watendaji mpaka wanakua na utendaji mbovu kiasi hiki na bado hakuna chochote kinachofanyika?

TUNAOMBA kilio chetu hiki kiwafikie wenye mamlaka (mh. Waziri wa Nishati) watusaidie utatuzi wa kadhia hii ambayo mimi binafsi nimeishi ndani ya halmashauri hii kwa miaka zaidi ya kumi lakini shida hii haijawahi kuisha.

Tulipata nafuu kipindi cha raisi magufuli baada ya kuwaambia atashughulika nao Kwasababu anajua wanachokifanya hali ikawa safi ndani ya miaka mitano tu kasahau shida hii,

Kwahiyo wananchi tunaamini shida hii sio ya kimfumo ni shida ya kiutendaji kwakua tuna uzoefu wa kupata huduma ya uhakika kwa kipindi kifupi baada ya mamlaka Kusimamia watendaji kikamilifu tena kwa miundombinu hii hii, na ofisi hizi hizi, na Vitendea kazi hivi hivi,

Tunaomba msaada wa dharura watu wanapata hasara ktk biashara zao na shughuli mbali mbali za kiuchumi

Ikiwezekana kama watendaji hawatakua na sababu geniune ifanyike reshuffle ya uhakika tupunguze mazoea.

Nitaambatisha screen shots za jumbe mbali mbali kutoka ktk group la TANESCO Mvomero kuonyesha hali ilivyo.

Screenshot_2026-02-26-13-23-29-987_com.whatsapp.w4b.jpg
Screenshot_2026-02-26-13-22-56-903_com.whatsapp.w4b.jpg
Screenshot_2026-02-26-13-22-27-917_com.whatsapp.w4b.jpg
 
Back
Top Bottom