Aisee sijui Kuna Siri Gani na haya majina, juzi nilikuwa cafeteria nakula then nikamuona mdada hivi mzuri kweli, nikajisemea kuwa siwezi kumuacha huyu bint aende zake bila kumuongelesha, kweli alivyoinuka na kuondoka nikamsimamisha na kuanza kuongea nae. Baada ya kumpigisha story nikamuuliza unaitwa nani, akanijibu mariamu, basi bhana nikaomba namba ya simu, baada ya hapo tukawa tunachat Kwa simu, sometimes nampigia.
Kwenye kuchat Yuko active sana lakini nikimuuliza kama line yake inapokea pesa huwa hajibu chochote ila muda huohuo nikimuuliza mambo mengine anajibu. Sasa nikawa najiuliza uyu bint hapendi pesa au ananitega. Nimemuuliza kama mara tatu hivi kuhusu kumtumia pesa lakini hajibu kitu.