Tatu bora ya wenyeviti wa vyama "wabovu" toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini.

Tatu bora ya wenyeviti wa vyama "wabovu" toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini.

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu ndugu zangu, Ama baada ya salam, leo ningependa kuwaletea list ya wenyeviti wa vyama wabovu toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe, huku nikiambatanisha na makosa yao waliofanya kupitia vyama vyao.

4) Mbatia - Huyu jamaa huwa anajifanya ni mpinzani, ila kiuhalisia sio mpinzani na hajawahi kuwa mpinzani. Kifupi yupo upinzani kwa ajili kuufaraganyisha upinzani kupitia chama chake ili kuipa nguvu na uimara zaidi CCM iendelee kutawala Tanzania.

3) Profesa Lipumba - Huyu jamaa aliwahi kuwa mpinzani wa kweli miaka ya 2000 to 2015, hadi akapelekea kuvunjwa mkono na askari police baada ya kujaribu kuandamana bila kibali. Ila pamoja na usomi wake wote Profesa huyo alikuja kushikwa masikio na vijana wasiokuwa na elimu hadi kupelekea kutoka katika upinzani wa kweli na kugeuka mpinzani wa kitengenezwa.

2) Zitto Kabwe - Huyu huwa anacheza na opportunity ya uongozi uliyopo madarakani. Akiona kiongozi alieko madarakani haendani nae kimaslahi basi lazima awe mkali zaidi ya ukali wenyewe, ila kiongozi akienda nae sawa, basi na yeye anakuwa upande wake kwa kumpa vijisifa lukuki vya kumpamba pamba ili aendelee kuneemeka nk.

1) Freeman Mbowe - Huyu ndio kiboko wa kutoa boko uongozini. Kwake yeye siasa ni biashara, na linapokuja swala la masilahi ya pesa huwa hacheki na nyani shambani. Mfano amekuwa akikikopesha chama chake mwenyewe magari chakavu kwa bei ile ile ya dukani, na kila ruzuku ilipoingia alianza kwanza kukata deni lake bila kuangalia kuwa kuna watendaji wa chama kibao huko vijijini hawana hata hela ya mlo mmoja kwa siku.

Mwenyekiti huyu ndio alitoa boko katika uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya kuvuta mpunga mrefu yeye na genge lake ili kumpitisha mgombea mungine wa CCM mh Lowasa aje kugombea katika chama chao na kuuwa kabisa ndoto zao za kuingia madarakani. Kila mtu mwenye akili huru alijua tu kwamba ule ulikuwa ni mpango wa CCM wa kuja kuuwa, kuusambaratisha na kuumaliza kabisa upinzani.

Mwenyekiti Mbowe pamoja kuuelewa ukweli huu lakini hakuona hasara kwani alichokusanya kilikuwa kikubwa na kamwe kushinda au kutokushinda uchaguzi kusingekuwa na madhara yoyote kwake as long as yeye na genge lake wameshakusanya mpunga wa kutosha kutoka upande wa pili. Matokeo yake mpango wa CCM ukatimia, chama kikaanza kukimbiwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge, madiwani nk.

Kati ya wapinzani wote niliotaja, hakuna mpinzani hata mmoja alieomba radhi kwa wananchi au wanachama wake kutokana na maboko waliyotoa katika uongozi wao. Ndio maana watanzania wengi kwa sasa wamewapuuza, japo huyu namba moja anaonekana mjanja kwa kuajiri chawa mbali mbali mitandaoni ili waje wampiganie, wamsifie na wamtetee kama tunavyoona katika thread na comments zao.

Asanten sana.

CLJbjIxXAAAHOcG.jpg


images (41).jpeg




images (44).jpeg


images (42).jpeg


images (19).jpeg
 
Back
Top Bottom