Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. TAUHIDA GALLOS Aitaka Serikali Kuwa na Mkakati Maalum Kunusuru Watoto Dhidi ya Migogoro ya Ndoa Nchini
"Wizara imeandaa muongozo wa Taifa wa uendeshaji, usimamizi na uratibu wa Mabaraza ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa wa mwaka 2023, Mei ambao umebainisha afua ya kuwajengea wajumbe wa Mabaraza juu ya namna bora ya kufanya usuluhishi wa migogoro kwa lengo la kuepusha athari zinazoweza kuwapata watoto ambao ni pamoja na kutokana na vitendo vya ukatili au unyanyasaji" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Migogoro ya ndoa hushughulikiwa pia na taasisi za dini zilizosajiliwa kisheria pamoja na maafisa wa ustawi wa jamii walio katika Halmashauri zote hapa Nchini" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Matatizo makubwa yanayosababishwa na migogoro ya ndoa inapelekea watoto wengi watanzania kubakwa na kupata mimba. Je, ni upi mkakati wa Serikali kunusuru watoto kwenye matatizo haya yanayosababishwa na ndoa?" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum.
"Takwimu zinaonyesha watoto wengi wanafanya vibaya shuleni matatizo yao makubwa yanasababishwa na migogoro ya ndoa. Serikali ina mikakati gani ya kuweza kuwasaidia watoto ili kuwanusuru na matatizo yanayotokana na migogoro ya ndoa?" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum
"Serikali imechukua hatua ya kuandaa muongozo Maalum uliohusisha taasisi za dini (Kiislamu na Kikristo) unaojulikana kama Wazazi Wangu Kesho Yangu unaolenga kuwahamasisha wazazi waweze kuwalea watoto wao kwa kuzingatia maadili mema na kuwa karibu na watoto wasiweze kuharibikiwa" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu 102 kinampa mamlaka Waziri wa Katiba na Sheria kuandaa Mabaraza katika ngazi ya Kata yaweze kufanya kazi ya usuluhishi" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu