Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Askari hao wamehitimu baada ya kukamilisha mafunzo ya miezi sita yaliyowajengea uwezo katika maeneo mbalimbali, ikiwemo matumizi sahihi ya silaha, mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS), utimamu wa mwili, nidhamu, haki za binadamu, udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na maadili ya kijeshi.
“Nendeni mkafanye kazi kwa nidhamu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo, bidii, weledi na ubunifu sawa na viapo vyenu bila upendeleo wala rushwa ili muweze kuwa misingi muhimu ya Jeshi la Uhifadhi lenye ufanisi.“
Naye, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Yussuf Kabange amesema kuwa uwezeshaji unaotolewa na Serikali umeendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii. TAWA inajukumu la kuhakikisha rasilimali za wanyamapori na maliasili zinalindwa kikamilifu ili ziendelee kuwa msingi wa shughuli za utalii, uwekezaji na maendeleo ya wananchi.
Kamishna Kabange amewataka askari hao wapya kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti ujangili, kulinda mazingira na rasilimali za Taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na jamii kwa kutoa elimu ya uhifadhi na kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori ili kuendelea kulinda rasilimali za Taifa."