Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Timu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), ikiongozwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Vicky Kamata, imefika katika Kata za Katangara Mrere na Kirongo Samanga, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, kwa lengo la kusikiliza changamoto na kutafuta suluhisho la pamoja kuhusu kero ya nyani wanaoharibu mazao ya wananchi.
Katika mkutano huo shirikishi, TAWA ilikutana na viongozi wa kata, akiwemo Mhe. Diwani Malaki Yananse na Mhe. Diwani Priscilla Shayo, pamoja na wananchi wa Kitongoji cha Msale. Wananchi walipata fursa ya kueleza kwa kina athari wanazokumbana nazo kutokana na wanyamapori hao, ikiwemo uharibifu wa mazao ya mahindi, maharage na ndizi, pamoja na hofu kuhusu usalama wao, hususan watoto wadogo.
Kwa upande wake, TAWA iliwashukuru wananchi kwa kuendelea kutumia njia rafiki za uhifadhi na kuepuka kuchukua sheria mkononi katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Aidha, TAWA imeahidi kuimarisha doria za pamoja na wananchi, kutoa elimu endelevu kuhusu mbinu bora na salama za kujikinga na wanyamapori wakorofi, pamoja na kuendelea kufanya jitihada ya kukabiriana na ongezeko la Nyani hao.
Pia, Soma: Rombo wanaume walalamika madume ya nyani kushika shika wake zao