Tax on Salary goes down from 15% to 14%. Is it Significant enough?

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2010
Posts
375
Reaction score
195
Ndugu wanajamii hapa jamvini, serikali imepunguza kodi kwenye mishahara kutoka 15% kwenda 14% ( very insiginificant change) ila nina wasiwasi na matokeo yake kwa ujumla.
Hivi ndivyo ninavyoona;

1) Punguzo hilo litasababisha mshtuko katika uchumi na matokeo yake, bidhaa zinaweza kupanda bei maradufu na hata hiyo afueni ya 1% tusiione, na infact analysis ya mshahara mmoja mmoja ikajaonyesha kuwa kitendo hicho kimesababisha madhara kuliko manufaa. (Elastic Change)

2)Thamani ya shilingi inaendelea kushuka zaidi na zaidi. Hatuambiwi kwa sasa iko kiasi gani ila kuna tetesi zinazoonyesha kuwa mfumuko wa bei kwa sasa ni tarakimu mbili (double digit). Je kupanda kwa kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa hivi karibuni, mfumuko wa bei tulio nao, je kutakuwa na manufaa ama kwenye makaratasi zitaonekana tarakimu nyiiiingi ilhali kwenye maisha ya halisi mambo ni mbinyo kama mwanzo na zaidi?

Ninaona kama vile haka kanyongeza kanakozungumziwa, ka unafuu ka kodi kalikotajwa, sio kakubwa kiasi cha kuwapa wananchi manufaa, bali kama kaajenda ka kisiasa hivi ili kujibu yale madai ya TUCTA katika maeneo haya mawili (mishahara na kodi)

Wakati wa kampeni waanze:."...Oh..walidai nyongeza na unafuu wa kodi yote tumeyatimiza..."

Jamani wataalamu mlio bobea, hebu tuambieni ujumla wa haya yote, unafuu unapatikana ama danganya toto, tujikute tupo pale pale ama tumerudi nyuma hatua moja?

Wantaaluma tusaidieni wananchi wa kawaida ambao si wataalamu sana wa Uchumi
 
To me this is a joke. Quite unattractive and cannot be used to entice votes of workers under the umbrella of TUCTA.
 
Hivi ningependa kufahamu:

Salary = Wage?

is it Taxi on Salary or Taxi on Minimum Wage?

:A S-eek:
 
It is nothing and non sense to all workers,
 
Do not forget, this is ONLY for the minimum WAGE..
 
Hivi mkubwa wa nji hii haoni soni juu ya tamko hili!
Tuhurumieni walala hoi sie hatuna ma-vx, sitting allowances, marupurupu kama nyie.... Eeeh mwenyezi mungu tutupie jicho lako ukatuokoe na kejeli hizi tunazofanyiwa.......amen
 

ukiambiwa bwabwa utaanza kutaka tupewe ban...
 
Tayari malaria imeshafika kwenye ubongo,tuandaeni kamba kwani mwenzetu huyu anaumwa,tena anaumwa sana. Au nawe una ule ugonjwa wa kuanguka kama best wako?
 

Hujapona tu hiyo malaria!!
 
Badala ya kuongezea watu mishahara, wao wanapunguza kodi kwa asilimia moja huku kodi kweny emambo mengine itaongezeka na gharam aza maisha kuongezeka! Talk about deception!
 
Kupunguza kodi ndio njia ambayo haina ubaguzi tofauti na kupandisha mshahara ambao kunagusa tu watumishi wa umma.... mara nyingi... in any case bado wenye kipato cha juu wananyongwa kwa 30%.

Serikali yetu imeishiwa maarifa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…