Tax on Salary goes down from 15% to 14%. Is it Significant enough?

Tax on Salary goes down from 15% to 14%. Is it Significant enough?

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2010
Posts
375
Reaction score
195
Ndugu wanajamii hapa jamvini, serikali imepunguza kodi kwenye mishahara kutoka 15% kwenda 14% ( very insiginificant change) ila nina wasiwasi na matokeo yake kwa ujumla.
Hivi ndivyo ninavyoona;

1) Punguzo hilo litasababisha mshtuko katika uchumi na matokeo yake, bidhaa zinaweza kupanda bei maradufu na hata hiyo afueni ya 1% tusiione, na infact analysis ya mshahara mmoja mmoja ikajaonyesha kuwa kitendo hicho kimesababisha madhara kuliko manufaa. (Elastic Change)

2)Thamani ya shilingi inaendelea kushuka zaidi na zaidi. Hatuambiwi kwa sasa iko kiasi gani ila kuna tetesi zinazoonyesha kuwa mfumuko wa bei kwa sasa ni tarakimu mbili (double digit). Je kupanda kwa kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa hivi karibuni, mfumuko wa bei tulio nao, je kutakuwa na manufaa ama kwenye makaratasi zitaonekana tarakimu nyiiiingi ilhali kwenye maisha ya halisi mambo ni mbinyo kama mwanzo na zaidi?

Ninaona kama vile haka kanyongeza kanakozungumziwa, ka unafuu ka kodi kalikotajwa, sio kakubwa kiasi cha kuwapa wananchi manufaa, bali kama kaajenda ka kisiasa hivi ili kujibu yale madai ya TUCTA katika maeneo haya mawili (mishahara na kodi)

Wakati wa kampeni waanze:."...Oh..walidai nyongeza na unafuu wa kodi yote tumeyatimiza..."

Jamani wataalamu mlio bobea, hebu tuambieni ujumla wa haya yote, unafuu unapatikana ama danganya toto, tujikute tupo pale pale ama tumerudi nyuma hatua moja?

Wantaaluma tusaidieni wananchi wa kawaida ambao si wataalamu sana wa Uchumi
 
To me this is a joke. Quite unattractive and cannot be used to entice votes of workers under the umbrella of TUCTA.
 
Hivi ningependa kufahamu:

Salary = Wage?

is it Taxi on Salary or Taxi on Minimum Wage?

:A S-eek:
 
It is nothing and non sense to all workers,
 
Hivi mkubwa wa nji hii haoni soni juu ya tamko hili!
Tuhurumieni walala hoi sie hatuna ma-vx, sitting allowances, marupurupu kama nyie.... Eeeh mwenyezi mungu tutupie jicho lako ukatuokoe na kejeli hizi tunazofanyiwa.......amen
 
SERIKALI YA JK jana iliwasilisha bungeni bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2010 /11 huku ikiwapoza wafanyakazi kwa kutangaza ongezeko la kima cha chini cha mishahara.
Akisoma hotuba hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafaa Mkulo alitangaza punguzo la asilimia moja kwa kodi ya mishahara kutoka asilimia 15 hadi 14 hatua inayoonekana imelenga kumaliza mgogoro wa wafanyakazi hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Alifafanua kuwa hatua za kuhakiki mishahara ili kudhibiti malipo kwa wafanyakazi hewa serikalini zitaendelea huku jukumu la kutangaza kima kipya cha mishahara ambacho ndio kilio kikubwa kwa wafanyakazi, litabaki mikononi mwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
"Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya mapato sura 332 kupunguza kiwango cha chini cha kodi ya mapato kwa wafanyakazi kutoka asilimia 15 hadi 14 sambamba na nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma,"alisema Bw. Mkulo
SASA WANAONA JK HAJATIMIZA AHADI ZAKE HAWANA HOJA HASA HII YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI. N

ukiambiwa bwabwa utaanza kutaka tupewe ban...
 
Tayari malaria imeshafika kwenye ubongo,tuandaeni kamba kwani mwenzetu huyu anaumwa,tena anaumwa sana. Au nawe una ule ugonjwa wa kuanguka kama best wako?
 
SERIKALI YA JK jana iliwasilisha bungeni bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2010 /11 huku ikiwapoza wafanyakazi kwa kutangaza ongezeko la kima cha chini cha mishahara.
Akisoma hotuba hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafaa Mkulo alitangaza punguzo la asilimia moja kwa kodi ya mishahara kutoka asilimia 15 hadi 14 hatua inayoonekana imelenga kumaliza mgogoro wa wafanyakazi hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Alifafanua kuwa hatua za kuhakiki mishahara ili kudhibiti malipo kwa wafanyakazi hewa serikalini zitaendelea huku jukumu la kutangaza kima kipya cha mishahara ambacho ndio kilio kikubwa kwa wafanyakazi, litabaki mikononi mwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
"Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya mapato sura 332 kupunguza kiwango cha chini cha kodi ya mapato kwa wafanyakazi kutoka asilimia 15 hadi 14 sambamba na nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma,"alisema Bw. Mkulo
SASA WANAONA JK HAJATIMIZA AHADI ZAKE HAWANA HOJA HASA HII YA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI. N

Hujapona tu hiyo malaria!!
 
Badala ya kuongezea watu mishahara, wao wanapunguza kodi kwa asilimia moja huku kodi kweny emambo mengine itaongezeka na gharam aza maisha kuongezeka! Talk about deception!
 
Kupunguza kodi ndio njia ambayo haina ubaguzi tofauti na kupandisha mshahara ambao kunagusa tu watumishi wa umma.... mara nyingi... in any case bado wenye kipato cha juu wananyongwa kwa 30%.

Serikali yetu imeishiwa maarifa...
 
Back
Top Bottom