jaxonwaziri
JF-Expert Member
- Feb 17, 2010
- 375
- 195
Ndugu wanajamii hapa jamvini, serikali imepunguza kodi kwenye mishahara kutoka 15% kwenda 14% ( very insiginificant change) ila nina wasiwasi na matokeo yake kwa ujumla.
Hivi ndivyo ninavyoona;
1) Punguzo hilo litasababisha mshtuko katika uchumi na matokeo yake, bidhaa zinaweza kupanda bei maradufu na hata hiyo afueni ya 1% tusiione, na infact analysis ya mshahara mmoja mmoja ikajaonyesha kuwa kitendo hicho kimesababisha madhara kuliko manufaa. (Elastic Change)
2)Thamani ya shilingi inaendelea kushuka zaidi na zaidi. Hatuambiwi kwa sasa iko kiasi gani ila kuna tetesi zinazoonyesha kuwa mfumuko wa bei kwa sasa ni tarakimu mbili (double digit). Je kupanda kwa kima cha chini cha mshahara kitakachotangazwa hivi karibuni, mfumuko wa bei tulio nao, je kutakuwa na manufaa ama kwenye makaratasi zitaonekana tarakimu nyiiiingi ilhali kwenye maisha ya halisi mambo ni mbinyo kama mwanzo na zaidi?
Ninaona kama vile haka kanyongeza kanakozungumziwa, ka unafuu ka kodi kalikotajwa, sio kakubwa kiasi cha kuwapa wananchi manufaa, bali kama kaajenda ka kisiasa hivi ili kujibu yale madai ya TUCTA katika maeneo haya mawili (mishahara na kodi)
Wakati wa kampeni waanze:."...Oh..walidai nyongeza na unafuu wa kodi yote tumeyatimiza..."
Jamani wataalamu mlio bobea, hebu tuambieni ujumla wa haya yote, unafuu unapatikana ama danganya toto, tujikute tupo pale pale ama tumerudi nyuma hatua moja?
Wantaaluma tusaidieni wananchi wa kawaida ambao si wataalamu sana wa Uchumi