Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Tukwepe mikusanyiko uku wao ndo wana changia watu wakusanyike

sijui itakuaje
 
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

Nchi hii ingekuwa ina wananchi wanaotambua haki zao hili sakata la corona na sukari yalitosha kabisa kuiondoa hii serikali madarakani kwa nguvu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi taifa lina serikali kweli bei ya jumla ya sukari ni 4200 huku niliko na sharti la kuuziwa lazima upange foleni na kilo ni 4500-5000, Nimewakuta wamama wamepanga foleni ya watu kama 200 na wanaswagwa kama mbuzi ukitoka tu kwenye mstari hata sukari upati tena hv kweli tuna serikali? kama tu hawawezi kuagiza sukari miaka 59 ya uhuru!
 
Kapicha basi mkuu tuone maana umewapitaje bila capture yoyote
 
Sikuwahi kudhani siku moja nchi itarudi kwenye utaratibu wa kupanga foleni kwa ajili ya bidhaa muhimu kama sukari. Haya ni mambo ya 1970 wakati Mwl. Nyerere alipolazimisha sera za ujamaa na uchumi ukaanza kuparanganyika.

Leo, wakazi wa Morogoro wanalazimika kupanga foleni kwa ajili ya sukari! Mkoa wenye viwanda vinne vya sukari, wakazi wake wa mjini wanasubiri sukari kwenye foleni, na ikipatikana watanunua kwa Tsh. 5,500 kwa kilo, au hata Tsh. 7000 kwa kilo.

Unajua maana ya kukosekana kwa sukari? Maana yake ni kuharibu biashara ya Mama ntilie.

Tuliambiwa awamu hii ya Magufuli Mambo yamekuwa magumu. Biashara ni ngumu, ingawa wapo wanaopinga hoja hii wakidai mambo ni magumu kwa sababu watu walizoea kuishi kifisadi'.

Sasa, Muuza Chai, Muuza Uji, Muuza Vitumbua, Maandazi na Chapati naye anafunga biashara kwa kukosa sukari, au kwa kushindwa kuhimili bei ya sukari. Je! Nao walizoea kuishi kifisadi'?

What a shame!
......
Christopher Cyrilo
FB_IMG_1589098854838.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

Wapo wengi tu hawajavaa barakoa.
 
Hii imenikumbusha mwaka 1980 baada ya vita ya Kagera!
 
Najua Bashungwa hana ufahamu wa forces of demand and supply ila hivi ni kweli wizara nzima haina mchumi?
When you impose a ceiling price without addressing supply is like kuchamba kabla ya kujisaidia. When you set a ceiling price in the absence of the commodity, you are intact allowing the sharks to take over.
 
imefikia kilo elfu 4. mtaani haipatikani.

Morogoro wanunua kwa foleni.

huko ulipo hali ikoje!?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mauaji ya Wapinzani,Mauwaji ya Wananchi kwa kutumia nyenzo ya Corona,ukosevu wa bidhaa muhimu watu kushindia mlo mmoja na kadhalika

Magufuli Nchi imeshamshinda kweni kujiuzulu ni dhambi jamani?
 
Back
Top Bottom