Ng'azagala
JF-Expert Member
- Jun 7, 2008
- 1,288
- 222
Kwa wakirsto mnaruhusiwa kufunga ndoa mara mbili kanisani, huyu mwanamke ameishawahi kufunga ndoa kanisani na DJ wa Clouds FM Nelly, au sheria zimefanyiwa marekebisho.
Nilishakuwa mwandishi wa habari kusema mume aliandaa sherehe ndogo ya watu wachache sana ni uwongo kwa wachagga. Wachaga harusi ni issue kubwa Useme hivi "ndugu na marafiki waliiisusia hiyo harusi na waligoma kuchanga hivyo zigo likamwangukia mume peke yake"!!! Usilete uwongo.
Wachawi utawajua tuNilishakuwa mwandishi wa habari kusema mume aliandaa sherehe ndogo ya watu wachache sana ni uwongo kwa wachagga. Wachaga harusi ni issue kubwa Useme hivi "ndugu na marafiki waliiisusia hiyo harusi na waligoma kuchanga hivyo zigo likamwangukia mume peke yake"!!! Usilete uwongo.
Nilishakuwa mwandishi wa habari kusema mume aliandaa sherehe ndogo ya watu wachache sana ni uwongo kwa wachagga. Wachaga harusi ni issue kubwa Useme hivi "ndugu na marafiki waliiisusia hiyo harusi na waligoma kuchanga hivyo zigo likamwangukia mume peke yake"!!! Usilete uwongo.
Hongera sana Joyce Kiria,hope ni Mrs Kilewo.MUNGU ni mwema sana,hatazami mambo kama sisi binadamu tunavyoyatazama...yeye si mwingi wa hasira bali mwingi wa rehema,husamehe bila kuhoji na hana kisasi,uhukumu kwa haki bila upendeleo na hutoa bila kuombwa.
Makosa yameumbwa kwa ajili ya mwanadamu,ubinadamu hutimia kwa kukiri madhaifu yetu na kuanza upya,kwani wewe ni nani hata usimkosee Mungu wako?kwani wewe ni nani hata Mungu asikusamehe na kuanza upya?
Nabii Daudi ambayo kwayo ukoo wa Yesu umetokea alimkasirisha Mungu,akiwa amejazwa na tamaa za mwili,alimpenda mke wa Huria,Daudi akiwa juu ya paa akizungukazunguka alimuona mke wa Huria ktk utupu wake,akaingia tamaa na kumtamani,ili kutimiza adhma yake akamuweka Huria mstari wa mbele ktk jeshi vitani,ili afe naye azini na mke wa Huria.
Alitimiza,lkn Mungu alimsamehe na kumuweka kama mfalme wa Mataifa,na ktk yeye ukoo wa Yesu ukazaliwa,kwani wewe ni nani usiye hata ktk ukoo wa Yesu na usitende dhambi?Mungu husamehe,tena katufunza tusamehe 7x70,Mwanamke Malaya aliyekimbia mikononi mwa Yesu ili asipigwe mawe alipona,si kwa sbb ya ubaunsa wa Yesu bali sbb ya hekima ya Yesu,aliyewataka makusanyo wasio na dhambi wawe wa kwanza kumtupia,wote walitawanyika abb hakukuwa na asiye na shambi.
Mungu hatazami kama mwanadamu anavyotazama,yupo tayari kuwaacha kondoo kenda walio zizini ili kumfuata mmoja aliyepotea,alimpa mamlaka Sauli aliyewatesa na kuwaua wafuasi wake,akampa upofu na Anania akamrudisha ktk nuru ili kumpa ushuhuda,hatimaye Sauli akabatizwa na kuitwa Paulo,akizunguka Samalia na Yudea kuutangaza habari njema.
Nayasema haya sbb kuna watu wameanza kuhukumu,wasijue lililo ndani yako na lililo ktk kusudi la Mungu,na wengine si kwa lolote,bali kwa chuki za kisiasa kwa mmoja wa waliofunga ndoa.
Tusihukumu ili tusije tukahukumiwa,kipimo kile tuwajaziacho wenzetu kwa kuwahukumu,ndio tutakachojaziwa na sisi.
.......Hata mie nashangaa, ninavyojua ukishafunga ndoa kanisani huwa hakuna talaka.
Talaka inatolewa mahakamani na sio kanisani.
Labda kama mmoja wapo afe, ndipo utafunga tena ndoa ya kanisa.
Ndio maana mwanzo waliamua kufunga ndoa serikalini, sababu kanisa halikukubali.
Nashangaa tena inakuwaje wamerudi kanisani. Ila ndio makanisa ya kidoti.com.
Mathayo 5:31-32
Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Huyo mda si mrefu, atafata mwenendo wa Babu Dr. Slaa na Mwneykiti wake Freeman mbowe.
Kuna baadhi ya sababu zinalazimisha kanisa kutoa go ahead ya kuenda mahakamani kwa ajili ya talaka. Uzinzi uliokithiri, unyanyasaji kwa maana ya abuse na ugomvi usioisha. Sharti ni lazima kupitia baraza la wazee wa kanisa kabla ya kwenda mahakamani.
Hebu tuwe serious. Kwa mfano binti kama huyo, mumewe alikuwa labda mzinzi ama anampiga, na wakaachana. Hivi kiimani tunategemea hatokaa aolewe tena ama hata kupata watoto kwa sababu ya dhambi ya mumewe? Tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Ndo maana nampenda Mungu wa rehema na neema
Hebu tuwe serious. Kwa mfano binti kama huyo, mumewe alikuwa labda mzinzi ama anampiga, na wakaachana. Hivi kiimani tunategemea hatokaa aolewe tena ama hata kupata watoto kwa sababu ya dhambi ya mumewe? Tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Ndo maana nampenda Mungu wa rehema na neema
Hakuna hata sababu moja ya msingi katika hizo ulizoandika inayopelekea ndoa kuvunjwa! Sababu pekee ni 1. Kama mume ni towashi kabla ya kufunga ndoa (siyo aupate akiwa kwenye ndoa). Pia kama mke au mume ana tatizo lolote litakalopelekea wasifaidi tendo la ndoa. 2. Undeclared children. Kwamba mmefunga ndoa halafu miezi michache baadaye linaletwa kundi la watoto wa mmojawapo wa wanandoa ambao hawakutajwa uwepo wao. Ama ikigundulika mmojawapo wa wanandoa alikuwa katika ndoa.
Biblia inaruhusu kutengana kwa muda kwa lengo la kurejeleana hapo baadaye, vinginevyo unless death do us apart. Ukimpenda Mungu utazishika amri zake, nothing less nothing more. Ndoa ni takatifu, ni lazima iheshimiwe na watu wote.
Kuna watu wana uelewa finyu kuhusu Biblia, ukiisoma vizuri utagundua kuwa inaruhusu Talaka ila kwa mashariti magumu. Maana maandiko yanasema; Mtu asimuache Mkewe/Mmewe isipokuwa kwa Uzinzi, kwa kosa la uzinzi mwanandoa aweza kumuacha mwenza wake, lakini mchakato huu utafanya na kanisa pamoja na wanandoa wenyewe kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Katika Ukristo ndoa ni kitu kinacho heshimika sana tofati na dini nyingine ambazo unaoa leo baada ya mwezi 1 ukijisikia kutoa talaka unatoa.