Tazama harusi ya kigogo wa CHADEMA, Henry Kilewo alivyofunga ndoa na Joyce Kiria

kama ndoa ya kwanza ilikugharimu ni sawa kwa hii ukasahihisha makosa maana ni ndoa ya pili. inakuwa vigumu wa wale wanaofanya ndoa ya kwanza maana si rahisi kuwa na ya pili. sikumbuki kuona watu wanaachana na kuwa na ndoa nyingine kubwa maana ungelazimika kuchangisha watu wale wale walioshiriki ile ya awali. Je wangechanga?
 
Kwa wakirsto mnaruhusiwa kufunga ndoa mara mbili kanisani, huyu mwanamke ameishawahi kufunga ndoa kanisani na DJ wa Clouds FM Nelly, au sheria zimefanyiwa marekebisho.
 
uzinzi umebalikiwa..hamna ndoa hapo ,kwanza huyo mwanamke mtalaka! Kanisa gani hilo !?
 
Kwa wakirsto mnaruhusiwa kufunga ndoa mara mbili kanisani, huyu mwanamke ameishawahi kufunga ndoa kanisani na DJ wa Clouds FM Nelly, au sheria zimefanyiwa marekebisho.

Mbona mnajaa povu hivo na kanisa wakati kasema ndoa ya pili ni ya Bomani/serikali?
 
Nilishakuwa mwandishi wa habari kusema mume aliandaa sherehe ndogo ya watu wachache sana ni uwongo kwa wachagga. Wachaga harusi ni issue kubwa Useme hivi "ndugu na marafiki waliiisusia hiyo harusi na waligoma kuchanga hivyo zigo likamwangukia mume peke yake"!!! Usilete uwongo.

Kweli una wivu wa kike kama alivyosema mtu mmoja humu... Nani kakwambia Kilewo ni mchaga? Acha kukurupuka man. Fwata yako ya wanaume yatakushinda.
 
Katiba na sheria ya kanisa zimebadilishwa ..... Ndo mana joyce kaolewa mara mbili kanisani .....
Dini nyingine ni za kibiashara zaidi
 
Nilishakuwa mwandishi wa habari kusema mume aliandaa sherehe ndogo ya watu wachache sana ni uwongo kwa wachagga. Wachaga harusi ni issue kubwa Useme hivi "ndugu na marafiki waliiisusia hiyo harusi na waligoma kuchanga hivyo zigo likamwangukia mume peke yake"!!! Usilete uwongo.
Wachawi utawajua tu
 
Ndugu huwezi kuongea chochote bila kutaja hawa wa2!
 
Hongera sana Joyce Kiria,hope ni Mrs Kilewo.MUNGU ni mwema sana,hatazami mambo kama sisi binadamu tunavyoyatazama...yeye si mwingi wa hasira bali mwingi wa rehema,husamehe bila kuhoji na hana kisasi,uhukumu kwa haki bila upendeleo na hutoa bila kuombwa.
Makosa yameumbwa kwa ajili ya mwanadamu,ubinadamu hutimia kwa kukiri madhaifu yetu na kuanza upya,kwani wewe ni nani hata usimkosee Mungu wako?kwani wewe ni nani hata Mungu asikusamehe na kuanza upya?
Nabii Daudi ambayo kwayo ukoo wa Yesu umetokea alimkasirisha Mungu,akiwa amejazwa na tamaa za mwili,alimpenda mke wa Huria,Daudi akiwa juu ya paa akizungukazunguka alimuona mke wa Huria ktk utupu wake,akaingia tamaa na kumtamani,ili kutimiza adhma yake akamuweka Huria mstari wa mbele ktk jeshi vitani,ili afe naye azini na mke wa Huria.
Alitimiza,lkn Mungu alimsamehe na kumuweka kama mfalme wa Mataifa,na ktk yeye ukoo wa Yesu ukazaliwa,kwani wewe ni nani usiye hata ktk ukoo wa Yesu na usitende dhambi?Mungu husamehe,tena katufunza tusamehe 7x70,Mwanamke Malaya aliyekimbia mikononi mwa Yesu ili asipigwe mawe alipona,si kwa sbb ya ubaunsa wa Yesu bali sbb ya hekima ya Yesu,aliyewataka makusanyo wasio na dhambi wawe wa kwanza kumtupia,wote walitawanyika abb hakukuwa na asiye na shambi.
Mungu hatazami kama mwanadamu anavyotazama,yupo tayari kuwaacha kondoo kenda walio zizini ili kumfuata mmoja aliyepotea,alimpa mamlaka Sauli aliyewatesa na kuwaua wafuasi wake,akampa upofu na Anania akamrudisha ktk nuru ili kumpa ushuhuda,hatimaye Sauli akabatizwa na kuitwa Paulo,akizunguka Samalia na Yudea kuutangaza habari njema.
Nayasema haya sbb kuna watu wameanza kuhukumu,wasijue lililo ndani yako na lililo ktk kusudi la Mungu,na wengine si kwa lolote,bali kwa chuki za kisiasa kwa mmoja wa waliofunga ndoa.
Tusihukumu ili tusije tukahukumiwa,kipimo kile tuwajaziacho wenzetu kwa kuwahukumu,ndio tutakachojaziwa na sisi.

Mathayo 5:31-32
Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
 
.......Hata mie nashangaa, ninavyojua ukishafunga ndoa kanisani huwa hakuna talaka.
Talaka inatolewa mahakamani na sio kanisani.
Labda kama mmoja wapo afe, ndipo utafunga tena ndoa ya kanisa.

Ndio maana mwanzo waliamua kufunga ndoa serikalini, sababu kanisa halikukubali.

Nashangaa tena inakuwaje wamerudi kanisani. Ila ndio makanisa ya kidoti.com.

Kuna baadhi ya sababu zinalazimisha kanisa kutoa go ahead ya kuenda mahakamani kwa ajili ya talaka. Uzinzi uliokithiri, unyanyasaji kwa maana ya abuse na ugomvi usioisha. Sharti ni lazima kupitia baraza la wazee wa kanisa kabla ya kwenda mahakamani.
 
Mathayo 5:31-32
Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Hebu tuwe serious. Kwa mfano binti kama huyo, mumewe alikuwa labda mzinzi ama anampiga, na wakaachana. Hivi kiimani tunategemea hatokaa aolewe tena ama hata kupata watoto kwa sababu ya dhambi ya mumewe? Tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Ndo maana nampenda Mungu wa rehema na neema
 
Mbona mnajaa povu hivo na kanisa wakati kasema ndoa ya pili ni ya Bomani/serikali?

IMG_0857.JPG

IMG_0924.JPG

Namwona kabidhi wasii mkuu kwa mbaaali, akifungisha ndoa.
 
Kuna baadhi ya sababu zinalazimisha kanisa kutoa go ahead ya kuenda mahakamani kwa ajili ya talaka. Uzinzi uliokithiri, unyanyasaji kwa maana ya abuse na ugomvi usioisha. Sharti ni lazima kupitia baraza la wazee wa kanisa kabla ya kwenda mahakamani.

Hakuna hata sababu moja ya msingi katika hizo ulizoandika inayopelekea ndoa kuvunjwa! Sababu pekee ni 1. Kama mume ni towashi kabla ya kufunga ndoa (siyo aupate akiwa kwenye ndoa). Pia kama mke au mume ana tatizo lolote litakalopelekea wasifaidi tendo la ndoa. 2. Undeclared children. Kwamba mmefunga ndoa halafu miezi michache baadaye linaletwa kundi la watoto wa mmojawapo wa wanandoa ambao hawakutajwa uwepo wao. Ama ikigundulika mmojawapo wa wanandoa alikuwa katika ndoa.

Hebu tuwe serious. Kwa mfano binti kama huyo, mumewe alikuwa labda mzinzi ama anampiga, na wakaachana. Hivi kiimani tunategemea hatokaa aolewe tena ama hata kupata watoto kwa sababu ya dhambi ya mumewe? Tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Ndo maana nampenda Mungu wa rehema na neema

Biblia inaruhusu kutengana kwa muda kwa lengo la kurejeleana hapo baadaye, vinginevyo unless death do us apart. Ukimpenda Mungu utazishika amri zake, nothing less nothing more. Ndoa ni takatifu, ni lazima iheshimiwe na watu wote.
 
Kuna watu wana uelewa finyu kuhusu Biblia, ukiisoma vizuri utagundua kuwa inaruhusu Talaka ila kwa mashariti magumu. Maana maandiko yanasema; Mtu asimuache Mkewe/Mmewe isipokuwa kwa Uzinzi, kwa kosa la uzinzi mwanandoa aweza kumuacha mwenza wake, lakini mchakato huu utafanya na kanisa pamoja na wanandoa wenyewe kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Katika Ukristo ndoa ni kitu kinacho heshimika sana tofati na dini nyingine ambazo unaoa leo baada ya mwezi 1 ukijisikia kutoa talaka unatoa.
 
Hakuna hata sababu moja ya msingi katika hizo ulizoandika inayopelekea ndoa kuvunjwa! Sababu pekee ni 1. Kama mume ni towashi kabla ya kufunga ndoa (siyo aupate akiwa kwenye ndoa). Pia kama mke au mume ana tatizo lolote litakalopelekea wasifaidi tendo la ndoa. 2. Undeclared children. Kwamba mmefunga ndoa halafu miezi michache baadaye linaletwa kundi la watoto wa mmojawapo wa wanandoa ambao hawakutajwa uwepo wao. Ama ikigundulika mmojawapo wa wanandoa alikuwa katika ndoa.

Biblia inaruhusu kutengana kwa muda kwa lengo la kurejeleana hapo baadaye, vinginevyo unless death do us apart. Ukimpenda Mungu utazishika amri zake, nothing less nothing more. Ndoa ni takatifu, ni lazima iheshimiwe na watu wote.

Kutengana kwa lengo la kulejeana ina maana gani?
 
Kuna watu wana uelewa finyu kuhusu Biblia, ukiisoma vizuri utagundua kuwa inaruhusu Talaka ila kwa mashariti magumu. Maana maandiko yanasema; Mtu asimuache Mkewe/Mmewe isipokuwa kwa Uzinzi, kwa kosa la uzinzi mwanandoa aweza kumuacha mwenza wake, lakini mchakato huu utafanya na kanisa pamoja na wanandoa wenyewe kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Katika Ukristo ndoa ni kitu kinacho heshimika sana tofati na dini nyingine ambazo unaoa leo baada ya mwezi 1 ukijisikia kutoa talaka unatoa.

Mkuu pamoja na uelewa wangu finyu, hakuna andiko linaloruhusu talaka katika biblia takatifu. Onesha hicho kifungu ili nami nipanue uelewa wangu.
 
Back
Top Bottom