Tazama jinsi Mungu alivyowaaibisha Wahandisi hawa wa Ujenzi!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Tukio hili linashangaza sana na linaendelea kugonga vichwa vya habari duniani. Wahandisi wa ujenzi waliobobea katika kubuni, kupanga na kusimamia ujenzi na matengenezo ya miundo ya majengo, walikumbwa na aibu ya karne baada ya Mungu kuwaaibisha hadharani. Wahandisi hao kama sio level ya Ph.D. in Civil Engineering (Structural focus) basi wanakaribia level hiyo!

Kwa lengo la kujimwambafy na kujijengea brand ya kudumu, waliamua kuanzisha project ya kujenga mji mkubwa wenye mnara mrefu unaozidi Burj Khalifa Tower. Kwa kutumia teknolojia ya kipekee wahandisi hao pamoja na wasaidizi wao walianza ujenzi kwa moyo mmoja na lugha moja ya mawasiliano.

Mara paap, mambo yakageuka. Bila onyo wala dalili zozote, hali ya sintofahamu ilitanda. Kila mmoja alianza kuzungumza kwa lugha tofauti, kana kwamba wana tatizo la afya ya akili. Mafundi walianza "kushikana mashati" baada ya kushindwa kuelewana, maana kila mmoja aliongea lugha nyingine tofauti kabisa na lugha ya asili. Ghafla ujenzi huo ulisimama papo hapo. Wahandisi waliokuwa wamejaa majigambo walibaki wameduwaa na kufedheheka, kisha wakatawanyika!

Jaribu kuvuta picha: Ungekuwa wewe ndio Mhandisi mkuu wa Project hiyo, umefika site, unawauliza Wahandisi: "Mbona hamuendelei na Ujenzi?" Wanakujibu kwa lugha usizozielewa:

Wer den Sohn hat, der hat das Leben; wer den Sohn Gottes nicht hat, der hat das Leben nicht.
Cristo murió por nuestros pecados, conforme a las Escrituras.
凡劳苦担重担的人,可以到我这里来,我就使你们得安息。
Ἡ γὰρ χάρις τοῦ Θεοῦ ἐπεφάνη σωτήριος πᾶσιν ἀνθρώποις.
الله محبة، ومن يثبت في المحبة يثبت في الله والله فيه.
Jésus est le chemin, la vérité et la vie; nul ne vient au Père que par lui.
Yesu ūlanizūkwe nane ū mu būtemi wako ūlū washoka!

UNGEJISIKIAJE ????
==================
Hiyo habari ya uchafuzi wa lugha, ni ya kweli kabisa. Kwa undani wa habari hiyo soma kitabu cha Mwanzo 11:1–9. Mungu ndiye aliyechafua lugha ya wajenzi hao ili wasielewane! Tukio hilo ndio chanzo cha lugha nyingi tunazozisikia duniani leo.

Ndugu zangu, Mungu ni Mkuu sana. Akiamua kukufanyia lolote, anaweza, na huwezi kumzuia. Wahandisi hao walianza ujenzi kwa fahari na kiburi na kutamba kwamba mnara wao utafika mbinguni. Hawakujua kuwa mbinguni kuna Mungu anayeweza kuwapiga stop na kuwashusha chini wanaojikweza.

Leo hii mtu akijua tu kutamka: "Ad hominem" na "logical fallacy" basi anajiona msoomii na mwenye hekima kweli kweli kiasi cha kusema eti Mungu hayupo. Siku inakuja, kila anayejiona dume, goti lake litakunjwa na atalazimika kukiri kuwa Yesu Kristo ni BWANA.
 
Umejifunza nini katika tukio au habari hiyo? Mimi nimejifunza madhara ya kiburi cha wanadamu na nguvu ya Mungu ya kuzuia mipango ya waasi, na pia asili ya lugha mbalimbali duniani.
 
Tukio hili linashangaza sana na linaendelea kugonga vichwa vya habari duniani. Wahandisi wa ujenzi waliobobea katika kubuni, kupanga na kusimamia ujenzi na matengenezo ya miundo ya majengo, walikumbwa na aibu ya karne baada ya Mungu kuwaaibisha hadharani. Wahandisi hao kama sio level ya Ph.D. in Civil Engineering (Structural focus) basi wanakaribia level hiyo!

Kwa moyo mmoja, kwa lengo la kujimwambafy na kujijengea brand ya kudumu, waliamua kuanzisha project ya kujenga mji mkubwa wenye mnara mrefu unaozidi Burj Khalifa Tower. Kwa kutumia teknolojia ya kipekee wahandisi hao pamoja na wasaidizi wao walianza ujenzi kwa moyo mmoja na lugha moja ya mawasiliano.

Mara paap, mambo yakageuka. Bila onyo wala dalili zozote, hali ya sintofahamu ilitanda. Kila mmoja alianza kuzungumza kwa lugha tofauti, kana kwamba wana tatizo la afya ya akili. Mafundi walianza "kushikana mashati" baada ya kushindwa kuelewana, maana kila mmoja aliongea lugha nyingine tofauti kabisa na lugha ya asili. Ghafla ujenzi huo ulisimama papo hapo. Wahandisi waliokuwa wamejaa majigambo walibaki wameduwaa na kufedheheka, kisha wakatawanyika!

Jaribu kuvuta picha: Ungekuwa wewe ndio Mhandisi mkuu wa Project hiyo, umefika site, unawauliza Wahandisi: "Mbona hamuendelei na Ujenzi?" Wanakujibu kwa lugha usizozielewa:

Wer den Sohn hat, der hat das Leben; wer den Sohn Gottes nicht hat, der hat das Leben nicht.
Cristo murió por nuestros pecados, conforme a las Escrituras.
凡劳苦担重担的人,可以到我这里来,我就使你们得安息。
Ἡ γὰρ χάρις τοῦ Θεοῦ ἐπεφάνη σωτήριος πᾶσιν ἀνθρώποις.
الله محبة، ومن يثبت في المحبة يثبت في الله والله فيه.
Jésus est le chemin, la vérité et la vie; nul ne vient au Père que par lui.
Yesu ūlanizūkwe nane ū mu būtemi wako ūlū washoka!

UNGEJISIKIAJE ????
==================
Hiyo habari ya uchafuzi wa lugha, ni ya kweli kabisa. Kwa undani wa habari hiyo soma kitabu cha Mwanzo 11:1–9. Mungu ndiye aliyechafua lugha ya wajenzi hao ili wasielewane! Tukio hilo ndio chanzo cha lugha nyingi tunazozisikia duniani leo.

Ndugu zangu, Mungu ni Mkuu sana. Akiamua kukufanyia lolote, anaweza, na huwezi kumzuia. Wahandisi hao walianza ujenzi kwa fahari na kiburi na kutamba kwamba mnara wao utafika mbinguni. Hawakujua kuwa mbinguni kuna Mungu anayeweza kuwapiga stop na kuwashusha chini wanaojikweza.

Leo hii mtu akijua tu kutamka: "Ad hominem" na "logical fallacy" basi anajiona msoomii na mwenye hekima kweli kweli kiasi cha kusema eti Mungu hayupo. Siku inakuja, kila anayejiona dume, goti lake litakunjwa na atalazimika kukiri kuwa Yesu Kristo ni BWANA.
Sawa mkuu!
 
Siku inakuja, kila anayejiona dume, goti lake litakunjwa na atalazimika kukiri kuwa Yesu Kristo ni BWANA.
Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana, na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.(Flp 2:9-11)
 
Karibu ujiunge na Freemason
KING MIDAS
Hebu niambie: Freemason ni nini hasa? Na je, nikijiunga, watanipa nini ambacho hakipo kwa Yesu. Yesu amenipa uzima wa milele bure na amani ya kweli. Sio hivyo tu, Yesu amenifanya mtoto wa Mungu. Nikiomba lolote kwake napata: mapesa, magari, nyumba... Freemason ina ofa zaidi ya hizo?
 
Umejifunza nini katika tukio au habari hiyo? Mimi nimejifunza madhara ya kiburi cha wanadamu na nguvu ya Mungu ya kuzuia mipango ya waasi, na pia asili ya lugha mbalimbali duniani.
Picha ipo Wapi? Unasema umepiga selfie na Mungu?
 
KING MIDAS
Hebu niambie: Freemason ni nini hasa? Na je, nikijiunga, watanipa nini ambacho hakipo kwa Yesu. Yesu amenipa uzima wa milele bure na amani ya kweli. Sio hivyo tu, Yesu amenifanya mtoto wa Mungu. Nikiomba lolote kwake napata: mapesa, magari, nyumba... Freemason ina ofa zaidi ya hizo?
Freemason Hawatakupa Uzima wa Milele, ila watakufanya uwe huo Uzima wa Milele. Hapo vipi?
 
Umejifunza nini katika tukio au habari hiyo? Mimi nimejifunza madhara ya kiburi cha wanadamu na nguvu ya Mungu ya kuzuia mipango ya waasi, na pia asili ya lugha mbalimbali duniani.
Linatufundisha kuwa, Tusimtegemee Mungu maana yeye mwenyewe anawaogopa binadamu.
 
Back
Top Bottom