Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
CCM ni chama kiongozi, ni chama kilichobeba Matumaini ya watanzania, ni chama kilichobeba hatima ya Taifa letu, ni bima ya watanzania na chama kilicho na heshima na kuheshimika ndani ya bara la Afrika na Duniani Kwote.
Embu angalia katika picha hii chini hapa yenye kupendeza ikionyesha wachina wakiongozwa na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China(CPC) ndugu Tang Dengjie wakimsikiliza kwa umakini na usikivu wa hali ya juu Sana katibu mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Nahodha imara.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar, Mwishoni kwa wiki hii katika Ziara ya siku tatu hapa Nchini.
Ni lini umewahi kuona CHADEMA ikapata nafasi ya kupokea ujumbe mzito kama huu? Kwanza ni nani ndani ya CHADEMA atafanya na kuongoza mazungumzo na watu wazito kama hawa? Kama chama kinaendeshwa na kuwategemea watu kama akina Mdude Nyagali na kuwaona mashujaa wake .sasa ni nani mwenye akili Timamu na anayejitambua ataweza kwenda kwenye chama kama hicho aina ya CHADEMA?
Kwanza watatumia ofisi zipi? Au watapelekwa nyumbani kwa Mheshimiwa Mbowe ndio kufanyike mazungumzo? Nani atakwenda CHADEMA kuitembelea chama kinachomtuhumu kiongozi wake wa juu kuwa alinyweshwa na kununuliwa Makreti ya Bia akanywa mpaka usiku wa manane? Au mmesahau mara hii vituko na vichekesho vya uchaguzi wa kanda ya Nyasa?😃😃😃.
CCM itaendelea kuongoza Taifa hili kwa kadri ya Uhai wake.huwezi ukaitengaisha CCM na Tanzania ,kwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kusema umchune mtu ngozi halafu utegemee abakie kuwa salama. Huo ndio UKWELI japo ni mchungu kwelikweli na naweza kuonekana mimi kama mwendawazimu au kichaa kwa kusema UKWELI huu.
CCM haitoki madarakani leo wala kesho wala kesho kutwa .ni CCM jana ,leo ,kesho na kwa kadri ya uhai wa Taifa letu. Hakuna Mtu wala chama chenye ubavu wala uwezo wala nguvu wala ushawishi wa kuitikisa CCM katika sanduku la kura .mtu na chama hicho hayupo na wala chama hicho hakipo na wala hakitakuwepo KAMWE.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.