Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Muwe Mnaelewa tunapowaambia ya kuwa Rais Samia anakubalika,kupendwa na kuungwa mkono ni haijapata Kutokea. Amekaa katika mioyo ya watu mpaka watu wanabubujikwa na machozi ya furaha wamuonapo. Watu wanakuwa na hamu na kiu kubwa sana ya kumsikiliza Mama ili wapate neno.
Embu angalia kwa picha tu namna alivyopokewa kwa wingi na maelfu ya wananchi waliofurika na kumiminika kwa wingi utafikiri mchanga wa bahari ,kumlaki Rais wetu mpendwa eneo la Gailo mkoani Morogoro ambako ameingia kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
Ikumbukwe ni siku chache tu alikuwa na ziara ndefu mikoa ya nyanda za juu kusini ,ambako nako alipata mapokezi makubwa na ya kihistoria kwa kupokelewa na maelfu kwa maelfu ya wananchi kwa kila alipopita na kufika.
Kwa hakika nyota njema huonekana asubuhi na Rais Samia ni Nyota njema inayoendelea kung'ara, kuangaza na kuleta nuru na matumaini kwa mamilioni ya Watanzania.
Kazi iendelee Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Soma zaidi: Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku sita mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Agosti