PreGE2025 Tazama Malori yakiwa na Baiskeli za Rais Samia kwa ajili ya kuzigawa kwa wapiga Kura

PreGE2025 Tazama Malori yakiwa na Baiskeli za Rais Samia kwa ajili ya kuzigawa kwa wapiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu!

Uchaguzi unapokaribia mbinu za kisiasa zinaongezeka, zikiwemo zawadi kwa wananchi zinazobeba sura ya rushwa. Hadi mabox yenyewe yameandikwa jina la Samia Suluhu Hassan (SSH). Tazama malori yakipakiwa sijui wanashusha baiskeli zinazojulikana kama Baiskeli za Rais Samia, tayari kwa kugawa kwa Wananchi wa maeneo mbalimbali.

Nimeona clip moja tiktok mzee mmoja ana toa shukran mpaka analia aisee ningekua karibu ningemnasa kibao na baiskali ngeichoma
 
Wafadhili wa CCM hao hapo hata shilingi moja ya CCM haijatumika
Kwahiyp hao wafadhili wakiiba mali za wananchi wataulizwa? Kwani wewe ni mgeni wa mambo ya Tanzania? Unakumbuka kipindi kile baada ya uchaguzi linawekwa zengwe treni inaanzia Dodoma badala ya kigoma ili kina Shabiby wabebe abiria?
 
Malori haya kutengenezwa au kukusudiwa kubeba abiria (Passengers), bali yametengenezwa kwa kusudi maalumu la kubeba mizigo. Kwa hiyo wale wanaosombwa na MACCM ni mizigo ya mama.

Mama anavunja sheria za Usalama barabarani mchana kweupe, alitakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kusababisha ajali ya uzembe iliyopelekea vifo vya watu wanne.
 
Baiskeli. Bila kujua kuwa tuna daiwa 107T
Dah ila kusema ukweli ccm kuja kutolewa kwa sanduku la kura n kujidanganya aisee, wananchi wenyewe ndo hao wakipelekewa baiskeli na kanga wanashangilia Aisee ccm wataendelea kuwepo sana tuu labla huku mijini ndo hawawezi kutufanyia upumbavu wao
 
Back
Top Bottom