Tazama namna Rais wetu akipitia nyaraka kwa umakini mkubwa wakati wengine wakionekana pichani wakisinzia huko Ethiopia

Tazama namna Rais wetu akipitia nyaraka kwa umakini mkubwa wakati wengine wakionekana pichani wakisinzia huko Ethiopia

Hizo nyaraka hakupewa kabla na kuziangalia ili kwenye mkutano a concentrate na kinachoendelea ? Huenda nimekosea ila mara nyingine kufanya kitu pekee ni jambo moja ila kufanya kitu kwa wakati muafaka ni more beneficial (huenda huyo aliyefumba macho na full concentration bila distraction ndio akawa anafuatilia zaidi)

Looks can be deceiving especially kama zikichukuliwa out of context....
Nani kakuambia kufumba macho? Kwani wewe huoni kuwa kasinzia?
 
Nani kakuambia kufumba macho? Kwani wewe huoni kuwa kasinzia?
Kwa watu ambao huwa tuna meditate hio pose inaweza kuonyesha umakini yaani unaondoa all disruptions zinazokusunguka yanabakia masikio ndio yanafanya kazi...; Nachotaka kukuonyesha ni kwamba picha kama hio inaweza ikatafsiriwa vyovyote vile hata unayesema ndio yupo tentative huenda ndio akaonekana anafanya yake badala ya kusikiliza
 
Hapo siyo Gest wala chumbani. Hapo ni mkutanoni
 
Hii nchi nina mashaka sana imevamiwa na wageni wengi, kuna mambo wanabisha kumpamba huyo maza enu mpaka unajiuliza hivi mtanzania anaweza fanya haya? Nadhani ile operation kimbunga ni muhimu CDF asisubiri maelekezo ya maza kunusuru hii nchi
 
Wivu tu ndio unakutesa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika tuna Rais Imara,kwa hakika Ikulu yetu Imepata Mtu Makini,shupavu , madhubuti,imara,hodari na Mwenye Utimamu wa Akili na Mwili. Tanzania tumepata Neema ya kuwa na Rais Anayejua nini anapaswa kufanya katika kuwakilisha Taifa letu .

Tumepata Neema na upendeleo wa kuwa na Rais Ambaye anajua wajibu wake na majukumu yake katika kutetea na kulinda Maslahi na heshima ya Taifa letu. Huyu Mama kwa hakika ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Siyo Binadamu wa kawaida . Ni mtu na Nusu. Anafanya kazi kwa umakini Utafikiri kafungiwa Mfumo wa kompyuta kichwani mwake.

Huwezi ukaona Rais wetu akizubaa zubaa awapo katika vikao muhimu na vya kimkakati.muda wote utaona Akipitia nyaraka neno kwa neno na kurasa moja baada ya nyingine. Ndio sababu hapitwi na jambo lolote lile,ndio maana Tanzania tumefaidika na mengi sana wakati huu wa uongozi wake.

Ndio maana Ushawishi wa Tanzania umeongezeka sana Duniani kwote ,ndio maana ya Mama yetu kuorodheshwa kuwa Miongoni Mwa wanawake mia moja wenye ushawishi na nguvu zaidi Duniani Kwote.

Embu Tazama kwa umakini pichani Rais wetu akiwa katika mkutano huko Addis Ababa Ethiopia akiwa makini akipitia nyaraka zake kurasa baada ya kurasa na neno baada ya neno kwa umakini wa hali ya juu sana. Lakini pia angalia mkono wa kulia wa Mama yetu kipenzi uone nini anakifanya huyo Mwingine.

Kama una macho mazuri yasiyo na upofu wa aina yoyote ile au matatizo ya aina yoyote ile utagundua kuwa huyo Mwingine pembeni ya RAIS wetu kipenzi anasinzia na wala hana habari na hizo nyaraka zilizopo mezani pake. Lakini ukitupa jicho kwa nyuma hapo unaona kuna mwingine yupo Bize na simu yake. Na wengine ni kama hata hawajui kama kuna karatasi na nyaraka wanazopaswa kuzipitia mezani pao kabla ya kuanza na kutoa michago yao.

Hapo ni lazima utegemee Rais wetu Mpendwa kuwa na mchango chanya na wenye tija na wenye kujenga kwelikweli,huku wengine wakiamka usingizini watakuja kuunga tu mkono hatuba na hoja za Mama yetu Mpendwa. Hii ndio maana Tanzania kwa kipindi hiki hatuwezi kuburuzwa na mtu yeyote yule kwa sababu tuna Rais na kiongozi makini na mwenye kuzungukwa na watu makini ambao wote wanakesha usiku na mchana kupigania maslahi ya Taifa letu na ustawi wa watanzania.

Kwa hakika CCM Imewapa kile watanzania wanahitaji katika mioyo yao . Imewapatia chaguo bora sana katika uchaguzi ujao.View attachment 3237142View attachment 3237143

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Yaani Mwashambwa unatabirika.
 
Back
Top Bottom