Tazama namna Rais wetu akipitia nyaraka kwa umakini mkubwa wakati wengine wakionekana pichani wakisinzia huko Ethiopia

Tazama namna Rais wetu akipitia nyaraka kwa umakini mkubwa wakati wengine wakionekana pichani wakisinzia huko Ethiopia

Ninyi ndio wasaliti wakubwa wa Tanganyika, na vizazi vyenu vya baadaye. Mtu amegawa rasilimali zote muhimu za Tanganyika kwa waarabu, halafu mnajitoa ufahamu na kumpamba!! Mlaaniwe watu ninyi, hamna faida.

Yaani mmekosa hata akili ndogo kabisa ya kujiuliza:

Hivi mwarabu anapopewa mbuga ya wanyama kwa mgongo wa uwekezaji, anawekeza nini kwenye mbuga? Ameleta twiga toka uarabuni?

Mwarabu anapopewa hifadhi ya misitu asilia kwa mgongo wa uwekezaji, amewekeza nini? Ameleta mobanga, mininga au mitundu kutoka Oman?
Huo uzushi wenu ulishapitwa na wakati na watanzania wanaelewa ukweli ni upi. Ni Ninyi mlikuwa mnazusha uzushi kuwa bandari zote zimeuzwa kwa Mwarabu . Lakini leo kila mtanzania anafahamu kuwa ukweli ni upi.
 
Kila nikiwaza kutoka kuwa sijui office attendant mpaka kuwa rais wa Nchi. Mungu ni mkubwa hapo ulipo jipige kifuani kwamba Mungu hpo siku. Yani Professa Shivji, Dkt Bashiru wameshindwa kuwa Marais Nchi kachukua Mama. Acheni Mungu aitwe Mungu.
Rais wetu ni akili kubwa na ni Mpango wa Mungu Mwenyewe ambaye hutoa uongozi. Huoni Odinga wa Kenya kila akigombea nafasi yoyote ile ndani ya nje ya Nchi anaishia kushindwa
 
Acha uongo wako hapa wewe. Mtu anasinzia zake hapo halafu na wewe unaleta uongo wako hapa.
Mbona Wassira akisinzia mna sema hajasinzia isipokuwa anatafakari mambo mazito!!
Samia anasema hizo unataka, je anaelewa kilichoandikwa?
 
Rais wetu ni akili kubwa na ni Mpango wa Mungu Mwenyewe ambaye hutoa uongozi. Huoni Odinga wa Kenya kila akigombea nafasi yoyote ile ndani ya nje ya Nchi anaishia kushindwa
Samia aliwahi kugombea uchaguzi gani akashinda?
Hajawahi na ndio maana anaogopa kushindanishwa!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika tuna Rais Imara,kwa hakika Ikulu yetu Imepata Mtu Makini,shupavu , madhubuti,imara,hodari na Mwenye Utimamu wa Akili na Mwili. Tanzania tumepata Neema ya kuwa na Rais Anayejua nini anapaswa kufanya katika kuwakilisha Taifa letu .

Tumepata Neema na upendeleo wa kuwa na Rais Ambaye anajua wajibu wake na majukumu yake katika kutetea na kulinda Maslahi na heshima ya Taifa letu. Huyu Mama kwa hakika ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Siyo Binadamu wa kawaida . Ni mtu na Nusu. Anafanya kazi kwa umakini Utafikiri kafungiwa Mfumo wa kompyuta kichwani mwake.

Huwezi ukaona Rais wetu akizubaa zubaa awapo katika vikao muhimu na vya kimkakati.muda wote utaona Akipitia nyaraka neno kwa neno na kurasa moja baada ya nyingine. Ndio sababu hapitwi na jambo lolote lile,ndio maana Tanzania tumefaidika na mengi sana wakati huu wa uongozi wake.

Ndio maana Ushawishi wa Tanzania umeongezeka sana Duniani kwote ,ndio maana ya Mama yetu kuorodheshwa kuwa Miongoni Mwa wanawake mia moja wenye ushawishi na nguvu zaidi Duniani Kwote.

Embu Tazama kwa umakini pichani Rais wetu akiwa katika mkutano huko Addis Ababa Ethiopia akiwa makini akipitia nyaraka zake kurasa baada ya kurasa na neno baada ya neno kwa umakini wa hali ya juu sana. Lakini pia angalia mkono wa kulia wa Mama yetu kipenzi uone nini anakifanya huyo Mwingine.

Kama una macho mazuri yasiyo na upofu wa aina yoyote ile au matatizo ya aina yoyote ile utagundua kuwa huyo Mwingine pembeni ya RAIS wetu kipenzi anasinzia na wala hana habari na hizo nyaraka zilizopo mezani pake. Lakini ukitupa jicho kwa nyuma hapo unaona kuna mwingine yupo Bize na simu yake. Na wengine ni kama hata hawajui kama kuna karatasi na nyaraka wanazopaswa kuzipitia mezani pao kabla ya kuanza na kutoa michago yao.

Hapo ni lazima utegemee Rais wetu Mpendwa kuwa na mchango chanya na wenye tija na wenye kujenga kwelikweli,huku wengine wakiamka usingizini watakuja kuunga tu mkono hatuba na hoja za Mama yetu Mpendwa. Hii ndio maana Tanzania kwa kipindi hiki hatuwezi kuburuzwa na mtu yeyote yule kwa sababu tuna Rais na kiongozi makini na mwenye kuzungukwa na watu makini ambao wote wanakesha usiku na mchana kupigania maslahi ya Taifa letu na ustawi wa watanzania.

Kwa hakika CCM Imewapa kile watanzania wanahitaji katika mioyo yao . Imewapatia chaguo bora sana katika uchaguzi ujao.View attachment 3237142View attachment 3237143

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Haelewi kilichoandikwa...anatos macho kama umeingia paper hujui uanzaje....hata jina hajasndika hapo...kilaza mwa mwi....huruma teleee
 
Mbona Wassira akisinzia mna sema hajasinzia isipokuwa anatafakari mambo mazito!!
Samia anasema hizo unataka, je anaelewa kilichoandikwa?
Kwa sasa RAIS Samia ndio Nembo ya Afrika na ndiye kiongozi anayetegemewa kutoa mwelekeo katika masuala mazito.
 
Punguza sifa za kijinga

Halafu yeye atakuwa anategemea mbeleko ya vyombo vya dola.
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka Marekani bado CCM na Rais wetu Mpendwa Mama Samia atapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
 
Back
Top Bottom