Maendeleo yoyote husukumwa na ubunifu! (Creativity)
Ili mwanasayansi agundue lazima asukumwe kufanya ubunifu!
Ili mfanya biashara atambulishe fursa lazime atangulize ubunifu!
Ubunifu ni Imani ya kutarajia suruhisho!
Endapo watu wakiongozwa kwa vitisho na sheria mbovu Imani hiyo ya ubunifu Hufa katika mioyo yao!
Nitatoa mfano!
Huko marekani wabunifu waliobuni gari ambalo likiwa kwenye foleni linachomoza matairi yake kunyanyuka zaidi halafu linatembea kwenye korridor ya foleni bila kuathiri magari mengine yaliyopo kwenye foleni.
Ukitazama chimbuko ya ubunifu huo unatokana na weledi Na sheria za kipolisi kuwa rafiki inchini kwao!
Ingekuwa hapa Tanzania bongo ufanye hayo kwenye foleni, Polisi watakuandama hata ikiwezekana utafuatiliwa na difenda kama zote na kuhojiwa kibabe.....Arooh inamaana unaharaka sana kuliko wenzako!....paki pembeni...Toa leseni yako...ruka kichurachura na hata gari lenyewe wataling'oa na plate number kabisa!
Hapo utaona kabisa! Hata kama wabunifu wakiwepo, hawawezi kuwekeza project kama hii kwasababu ya kuhisi haitapokelewa sokoni na hao polisi
Mfano wa pili ni biashara!
Leo hii mhitimu wa chuo akitaka kufungua kampuni, Brela watamchaji pesa kibao ili kumsajili wakati hata biashara yenyewe wakati huo hajaanza!
Akitoka hapo atakwenda TRA, huko nako kabla ya kupata TIN watampa fomu kibao ajaze, na wanayohoji ni yaleyale ambayo yalijazwa brela! na watampa makadirio ambayo atatakiwa kulipa kabla hata biashara yenyewe hajaanza!
Sasa mtu anayekuja kujisajili unamwambia Alipe makadirio yepi wakati hajaanza hata hiyo biashara yenyewe?
Wakati kwanza ilitakiwa TRA wawe Automatically link na BRELA, Ili kampuni ikishasajiliwa brela na kupewa certificate, moja kwa moja huko TRA nao waione na kuipa TIN ya msamaha wa mda (Online and automatic process)! ili baadae ndipo TRA wakachukue chao baada ya mteja wao kuanza biashara!
Mtu huyo tena akitoka TRA akiwa tax clearance aende kwenye mamlaka za leseni nako atozwe pesa wakati biashara bado!
Akitoka hapo aende kwenye taasisi husika kujisajili nako wamkamue pesa na mambo kedekede ya kuambatanisha!
Hapo ndipo utagundua ubunifu upo sana afrika lakini Tunauwana wenyewe kwa sheria za kikoloni kutoka kwenye mamlaka! Na haya ndiyo huchangia rushwa na udanganyifu!