Tazama vile viumbe tunavyotumia mbao kwa wingi! Lakini kuna mtu humu hajawahi hata kufikilia kupanda mti hata mmoja

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Binadam tunalalia vitanda asilimia kubwa ni mbao! Ebu waza idadi ya kaya mtaani kwako halafu uzidishe kwa taifa zima utagundua ni miti mingi imepotea kutengenezea hivyo vitanda!
Waza idadi ya majumba, kila nyumba ina milango ya mbao, kenchi za mbao, madilisha ya mbao na makabati ya mbao hakika utaona miti inavyotufaa wanadam!

Wakati unawaza utaenda kulewa wapi, ebu fikilia ni bar ngapi zinakaunta ya miti na mbao!

Wale mabaharia wenzangu tunaokula kwa mamalishe, ebu waza kuni na mkaa wa mama lishe vimetokana na miti ile ile enzi na enzi!
Ebu waza tena kwa idadi ya watu waliopo ambapo tz kama 60mil jaribu kufikilia nusu yao 30mil mathalani ni wakristo wakija kufariki watahitaji kuzikwa na jeneza la mbao!

SASA JIULIZE hivi kwa umhimu wote huu kwanini usipande hata mti mmoja na wewe hapo ulipo?

Hata kama hautakusaidia wewe jaribu kuwaza hata ndege utawasaidia pa kutua!

Unapofurahi kivuli cha mti wakati huu wa jua Kali, kumbuka kuna mtu kama wewe aliupanda mti huo, kama hakuupanda basi alizuia usikatwe!

Kwa umri huo ni aibu sana kuwa miongoni mwa watu ambao hawajawahi kupanda mti hata mmoja hapa duniani!

Ukitaka umri mrefu penda miti&misitu, miti na misitu inachangia uhai kuongezeka, miti ni chakula, dawa na ni chanzo kikuu cha oksjeni!

Ukitaka kujua umhimu wa oksjeni ilivyo na gharama kubwa muulize mtu aliyeugua covid akawekewa mitungi ya hewa!

Sasa unashindwaje kupanda mti hata mmoja!
Hata kama eneo siyo lako nakushauri panda mti hata kando ya njia;

Usiogope mti wako kuja kukatwa, wewe panda kwanza hayo mengi baadae!
 
umewaza pakubwa sana mkuu...turud kwenye vyuma na aluminium kwa muda wa miaka kumi then baadae turud tena kweny miti ikiwa imesheheni
 
Wakati huo watu wakiwa wanapikia nini? Kama ni mkaa basi pendekezo lako ni sawa na bure.
 
Kila mtu anayesoma bango lako anapaswa akupe likes nyingi sana.
Hizi ndo nyuzi sahihi za kuamsha waliolala.
 
umewaza pakubwa sana mkuu...turud kwenye vyuma na aluminium kwa muda wa miaka kumi then baadae turud tena kweny miti ikiwa imesheheni
Sawa sawa turudi kwenye aluminiam na chuma hadi kupikia na gharama yake ni nafuu sana kuliko mbao
 
Kongole kwako kwa nyuzi murua mkuu.

Ni kweli jamii inapaswa kielimishwa kuhusu uoandaji wa miti.
Lakini tatizo linalotukabili ni makazi holela, ni bora basi kama yangetengwa maeneo kwa ajili hiyo.
 
Ni sawa lakini kila mtu aanze na jukumu rahisi la kupanda mti, halafu hayo mengine ya wajibu wa serikali tuwaachie wanasiasa
 
ukiachana na mbao hata miti ya mkaa inavunwa hasa.

serikali irahisishe upatikanaji wa gas na kwa gharama nafuu.

bomba lilijengwa toka mtwara to dar wakasema hata umeme utafufuliwa kwa gas leo hii makamba anasema gas kuanza kuchimbwa 2025.

kila awamu inakuja na kauli zake, tunarudi tena kwenye kutegemea umeme wa maji wakati tuliambiwa hata gharama za unit zitashuka.
 
Andio lako ni zuri Sana...

Mababu zetu licha ya kukosa uelewa mpana lakini walithamini mazingira yao ..sisi tuna uelewa na vitu mbadala Kama gesi lakini bado tumo kuharibu na hattuna muamko wa kuhifadhi na kuendeleza mazingira..

Elimu , uhamasishaji na Sheria Kali zinahitajika.. .. ili kuhifadhi mazingira kupanda na kutokata miti hovyo..

Serikale na wananchi wote wako bize

Kiasi tunashindwa hili ambalo ni la muhimu zaidi!
 
Wewe umepanda mingapi?!!
Hapa kwangu nilipanda 5 , huko barabarani ukipita maeneo ya ununio na mbweni kando ya njia nimefanikiwa kupanda miembe minne, chuo nilichosoma nilifanikiwa kupanda mti wa kivuli kwa siri enzi hizo, nashukuru hadi Leo nikipita pale chuoni ule mti wanafunzi hukaa chini yake kujisomea!
 
Andio lako ni zuri Sana...

Mababu zetu licha ya kukosa uelewa mpana lakini walithamini mazingira yao ..sisi tuna uelewa na vitu mbadala Kama gesi lakini bado tumo kuharibu na hattuna muamko wa kuhifadhi na kuendeleza mazingira..

Elimu , uhamasishaji na Sheria Kali zinahitajika.. .. ili kuhifadhi mazingira kupanda na kutokata miti hovyo..

Serikale na wananchi wote wako bize

Kiasi tunashindwa hili ambalo ni la muhimu zaidi!
Kweli kabisa mkuu
 
Hapa kwangu nilipanda 5 , huko barabarani ukipita maeneo ya ununio na mweni kando ya njia nimefanikiwa kupanda miembe minne, chuo nilichosoma nilifanikiwa kupanda mti wa kivuli kwa siri enzi hizo, nashukuru hadi Leo nikipita pale chuoni ule mti wanafunzi hukaa chini yake kujisomea!
Hongera
 
Back
Top Bottom