5 bila mkuu, sio mbili bila.
Heaven Sent ameelezea vizuri sana. Kuna jamaa tulikua tunafanya nae kazi, tukatumiwa email amefiwa na Mama yake, kwenda asubuhi kazini, namkuta yupo na anaendelea na kazi. Tukashtuka, kumbe wao mazishi sio ghafla kama kwetu, wanaweza kukaa hata miezi miwili au mitatu.
Na wakati huo hapo katikati ni full ubwabwa na finyango za kutosha kutegemea na hadhi ya aliyefariki na uwezo wa familia.
Huo utamaduni nikasema sasa hapo unakuta mtu kafiwa na jamaa wa mbali hafiki ofisini anatuma sms tu, ukikuta boss kama huyo si anakushangaa?
Ndio nikaona umuhimu wa kujifunza na kuelewa tamaduni za wengine.