Wenzetu Magharibi wanaamini mtu akifa sio mwisho wake, kuna maisha mengine baada ya kufa. Na mazishi yao huwa ni more of a celebration, kufurahia maisha ya mpendwa wao hapa duniani na kumtakia kheri kwenye maisha yake mapya. So anapokufa wanamfanyia the so called befitting burial. Kwa hiyo lazima wachukue muda kujipanga kumfanyia hiyo sherehe, na ndiyo hapo inategema kati ya mtu na mtu (titles). Nakumbuka first time nasikia hili, kuna Nigerian Actor alikuwa anaitwa Justus Esiri alikuwa amefariki; imepita miezi miwili ndiyo nakuja kusoma eti anazikwa. Baba yake Yemi Alade na yeye alifariki January akaja kuzikwa May n.k
Hiyo befitting burial ndiyo unakuta jeneza la gharama, Aso ebi (sare, kama mnavyojua mishono ya kinigeria) + grand party. Na naonaga wanakuwa wanaimba na kucheza haswa (nawazia kilio cha wanyaki). So kwa wenzetu wakifiwa ni stress mara mbili; kwanza mmempoteza ndugu yenu, na pili ni gharama za mazishi; inakuwa kama mashindano sasa nani alizikika kifahari zaidi. Lakini kwa Northeners ambao wengi ni Muslims, mazishi yao ni chapchap kama kawaida.