DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepanga kuwaondoa watumishi wa umma na wapangaji wote wanaodaiwa na wakala huo, iwapo hawatalipa madeni yao ifikapo Septemba 30, 2025.
Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro, amesema kuwa zoezi la kuwaondoa wadaiwa hao litazingatia mikataba iliyowekwa na wateja wao.
Amesema wadaiwa wote watakaoshindwa kulipa madeni yao wataondolewa, na nyumba hizo zitatolewa kwa watumishi wengine.
Arch. Kondoro ameongeza kuwa zoezi hilo litawahusisha pia watumishi ambao wamehamishwa vituo vya kazi kutoka mji mmoja kwenda mwingine, watumishi wa umma waliostaafu, watumishi wa umma waliofariki dunia, na watumishi wa umma walioacha utumishi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Milki wa TBA, Said Mndeme, amesema wakala huo unadai wapangaji wake zaidi ya shilingi bilioni 4.5, ambapo mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma ndiyo inaongoza kwa madeni hayo.