TBC haipo hewani, Mafuriko ya leo yasababishwa izimwe

TBC haipo hewani, Mafuriko ya leo yasababishwa izimwe

Nadhano kati ya taasisi ambazo hazina faida yoyote kwa umma wa watanzania, mojawapo ni hii tbc.

Ni chombo kinachotumia pesa yetu lakini kinatumika kama chombo cha watawala na CCM.

Sidhani kama kuna mtanzania mzalendo wa kweli anayeweza kusikitika kama tbc itashindwa kurusha matangazo, na huenda ikawa ni faraja kwa walio wengi.

Tunahitaji vyombo vya habari vinavyoendeshwa kwa maadli na weledi, na siyo vyombo vya hovyo kama tbc. Ukisikia chochote kupitia tbc unalazimika kufuatilia habari kutoka vyombo vingine ili kuthobitisha ukweli wa habari iliyotangazwa au kusikika kupitia tbc.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa tushauriane tufanyeje ili wajirekebishe?
Au wamebaki tu kuweka wanwake akina Mkabesah na wengine kuuza sura bila contents?
au kwasababu wana maelekezo ya kuto onyesha habari za lissu?
 
Ila TBC no utopolo...hata wasiporudi hewani ni sawa tu ..Yaani tanzania haitakuwa a kitu chochote ilicho kipoteza 😂 😂 😂
eh, sijaona positive comment kuhusu TBC, kutakuwa na shida pale, ijui ni mkurugenzi ndio tatizo?
 
Kumbe ni kweli imezima, vipi Radio yao?
Radio ipo, studio za Radio zipo TAZARA-NYERERE ROAD, studio za TV ndiyo zipo kwenye Shamba la Mpunga mikocheni.
Nahisi aliyetoa wazo la kujenga zile studio pale shamba la mpunga ndiyo huyo huyo aliyeshauri kujenga Kituo cha mwendokasi pale jangwani.
 
eh, sijaona positive comment kuhusu TBC, kutakuwa na shida pale, ijui ni mkurugenzi ndio tatizo?
Channel inaendeshwa kizee sana Content zake zimekaa kizee mnoo ubunifu 0..wakati katika taifa lolote lile generation yenye nguvu ni ya vijana ..ukifanikiwa kuwateka vijana basi umefanikiwa katika project yako ..kubwa zaidi na ambalo ndio baya kabisa TBC ni mali ya wananchi lakini imekuwa ikitumiwa vibaya na chama tawala kwaajili ya kueneza propaganda zao ambazo wakati mwingine zina kandamiza vyama pinzani
 
na habari kutoka vyanzo ambavyo bado havija dhibitishwa ni kwamba Maji yameingia ndani ya studio na tangu asubuhi imekuwa ikifanika jitihada ya kuvuta maji hayo bila mafanikio[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Radio ipo, studio za Radio zipo TAZARA-NYERERE ROAD, studio za TV ndiyo zipo kwenye Shamba la Mpunga mikocheni.
Nahisi aliyetoa wazo la kujenga zile studio pale shamba la mpunga ndiyo huyo huyo aliyeshauri kujenga Kituo cha mwendokasi pale jangwani.
Kwahiyo atakuwa ni meko!??😂
 
Safi sana,hayo maji yaendelee kuwepo na mitambo ipate kutu ili wasirudi hewani hadi novemba au disemba kabisa.Maana wamezidi bias kwenye kurusha matangazo ya kampeni,wao wapo na JIWE tu asbh hadi usiku!!
 
TBC Tanzania Broadcast Corporation ambapo zamani ilijulikana kama TvT katika hali ya kustaabisha na kushangaza ulimwengu inasemekana haipo hewani na habari kutoka vyanzo ambavyo bado havija dhibitishwa ni kwamba Maji yameingia ndani ya studio na tangu asubuhi imekuwa ikifanika jitihada ya kuvuta maji hayo bila mafanikio.

Chanzo cha maji hayo ni kile kile kujenga Studio bila kuwa na mipango mikakati wakijua kabisa pale lilikuwa shamba la mpunga, water table ipo karibu na hakuna drainage, sasa wanavuna walichopanda.


Habari zaidi zitawajia baadae baada ya kudhibitishwa.
Mbona Kama umefurahi badala ya kusikitika?
 
If not us Who?
And if not now when?

28/10/2020 Lissu is my president.[emoji111]
My president
IMG_20201004_214806.jpeg
IMG_20201004_214038.jpeg
IMG_20200926_184130.jpeg
 
Kama imefikia kipindi watanzania tunafutahia majanga basi ujue uzalendo umefika ukomo.
Mkuu. Uzalendo unaisha kutokana na serikali inavyo wa treat raia wake. Unakumbuka kipindi Cha awamu ya pili? Rais alikua anatembea na defender amekaa mbele kushoto huku amefushusha vioo anasalimia wananchi.
Msafara wake ilikua wakati mwingine magari mawili tu.
 
Back
Top Bottom