Tetesi: TBC hakukaliki, muda wowote Zuhura Yunus anakuja na mkeka!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776

Tetesi zinaelekeza Salim Kikeke anaendelea kutajwa kumng'oa Ayub Rioba alijizindika pale TBC. Hii ni baada ya chombo hiki cha Wananchi kushindwa mambo mengi na kufuja fedha za umma huku Watumishi wake wengi wakijianzishia makampuni shindani na TBC. Ukichukua TIN za Watumishi utashangaa wao ndio wana maduka yanauza bidhaa kwa TBC.

1. TBC ni chombo cha umma ambacho kinapaswa kuwa na weledi wa hali ya juu. TBC inapaswa kujitofautisha na vyombo vya mchongo vilivyozagaa nchini.

2. Kuna matukio mengi ambayo TBC imeyafanya bila kuzingatia weledi. Itoshe kuyataja machache:

2.1 Mwaka 2014 wakati wa Mjadala wa Katiba, TBC ilikuwa ikitoa upendeleo na kukera wengi akiwemo Mwandishi nguli Maggid Mjengwa wa Iringa ambaye alilazimika kulalamika.

Aidha, TBC ghafla ilikatisha matangazo Aprili 14, 2014 wakati Mhe Tundu Lissu akitoa maoni kwa niaba ya Kamati yake! Dr. Slaa, aliyekuwa KM CHADEMA, akazomoka:

"TBC ni adui wa mageuzi. Serikali imesahau kuwa ilisaini Maadili ya Vyombo vya Umma vitumike kwa manufaa ya umma bila upendeleo".

2.2 Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2020, TBC ilikinaisha kwa kuonesha kampeni za CCM tu 24/7 hadi kupachikwa jina la utani TBCCM ilihali TBC ni chombo cha umma na kuna uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa vyombo vyote vya habari vya umma vinapaswa kutoa haki sawa kwa vyama vyote.

2.3 Machi 10, 2017, TBC, kwa uchawa wake, ilitulisha "Bongolanderz" matango pori kwa kudai eti Rais Donald Trump wa Marekani amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri ! Enzi zile, ungedhani kuna mashindano ya Mawizara na Taasisi za umma kumsifia Rais Magufuli! Uchawa huu ukapelekea waandishi 9 wa TBC wasimamishwe! Waliosimamishwa ni Gabriel Zakharia, E. Mramba, P. Constantino, D. Mmari, R. Mpenda, L. Mushi, A. Wawa, C. Ruza na J. Losai.

2.4 Desemba 23, 2015, TBC iliwakera "Bongolanderz" nchi nzima pale ilipokatiza ghafla Taarifa ya Habari Saa 2 usiku na kuonesha harusi ya Kibopa mmoja kwa Saa 3! Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari (Maelezo), Assa Mwambene akatiririka:

"TBC ilichofanya si sahihi. TBC ni chombo cha umma hakikupaswa kuonesha mambo ya mtu binafsi kwa zaidi ya saa tatu. Saa tatu umma unaangalia mtu anavyomsifia mke wake? Kisa amelipa milioni 17? Hii si sawa".

2.5 Baadhi ya Watangazaji wa TBC uelewa wao ni mdogo sana kiasi kwamba kwenye mahojiano mubashara kuhusu mambo muhimu ya Kitaifa wanauliza maswali ya kijinga/kitoto sana na kukera mno (wapo baadhi wanauliza maswali ya maana mf Gabriel & Elizabeth). Aidha, wengine wanashindwa kutofautisha baadhi ya herufi mf "R" na "L".

2.6 Septemba 4, 2019. Kamati ya Maudhui ya TCRA ilitoa onyo kali kwa TBC kwa kukiuka Sheria, Kanuni na Misingi ya Uandishi wa Habari kwa kuonesha picha zisizofaa.

2.7 TBC ilifuta matangazo mubashara ya Bunge kwa sababu za kimchongo 2016. Ilielezwa kuwa TBC haitakuwa ikionesha bunge mubashara kwavile eti "Bongolanderz" wengi huwa makazini hivyo wanaacha kazi na kuangalia bunge! Tuliosomea Cuba tulibaini ni fiksi. Mhe Spika Ndugai baada ya "kustaafu" akamwaga mambo hadharani:

"Leo niseme ukweli; sababu ya kuachana na kuonesha bunge "live" ni kwavile tulibaini Wabunge wa upinzani walikuwa wanapata coverage kubwa inayowapa kichwa. Tulibaini wengi hawaendi majimboni kwao, wanatumia bunge tu na wengine wanaishambulia sana Serikali ili wajulikane kwavile wanajua kuna Bunge "live"!.

2.8 Tukio la majuzi la MV Mwanza ndio fungakazi. Mwandishi, bila kupepesa macho wala kutikisa mustachi, ameeleza eti meli hiyo itafika hadi Malawi & Zambia! Kwani inatumia matairi ? Hivi mnatuchukuliaje lakini? Mbaya zaidi, nimeiona taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ambayo haikutaja nchi hizo hivyo mwandishi kaongea urongo mwingine! Cha ajabu, hadi leo TBC haijatuomba radhi!

NB:
Ikumbukwe kuwa Mhe Harrison Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Habari, Sanaa & Utamaduni, alieleza bungeni alipowasilisha bajeti ya Wizara yake ya 2017/18 kuwa moja ya changamoto kubwa za TBC ni kutozingatiwa kwa maadili ya uandishi wa habari.

Miaka 7 baadaye, tatizo bado linataradadi!
 
View attachment 2948917
Tetesi zinaelekeza Salim Kikeke anaendelea kutajwa kumngoa Ayub Ryoba alijizindika pale TBC. Hi ni baada ya chombo hiki cha wananchi kushindwa mambo mengi na kufuja fedha za umma huku watumishi wake wengi wakijianzishia makampuni shindani na TBC. Ukichukua TIN za watumishi utashangaa wao ndio wana maduka yaiuza bidhaa kwa TBC.

1. TBC ni chombo cha umma ambacho kinapaswa kuwa na weledi wa hali ya juu. TBC inapaswa kujitofautisha na vyombo vya mchongo vilivyozagaa nchini.

2. Kuna matukio mengi ambayo TBC imeyafanya bila kuzingatia weledi. Itoshe kuyataja machache:

2.1 Mwaka 2014 wakati wa Mjadala wa Katiba, TBC ilikuwa ikitoa upendeleo na kukera wengi akiwemo Mwandishi nguli Maggid Mjengwa wa Iringa ambaye alilazimika kulalamika. Aidha, TBC ghafla ilikatisha matangazo April 14, 2014 wakati Mhe Tundu Lissu akitoa maoni kwa niaba ya Kamati yake! Dr. Slaa, aliyekuwa KM CHADEMA, akazomoka:

"TBC ni aduinwa mageuzi. Serikali imesahau kuwa ilisaini Maadili ya vyombo vya umma vitumike kwa manufaa ya imma bila upendeleo".

2.2 Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020, TBC ilikinaisha kwa kuonesha kampeni za CCM tu 24/7 hadi kupachikwa jina la utani TBCCM il hali TBC ni chombo cha umma na il hali kuna uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa vyombo vyote vya habari vya umma vinapaswa kutoa haki sawa kwa vyama vyote.

2.3 Machi 10, 2017, TBC, kwa uchawa wake, ilitulisha "Bongolanderz" matango pori kwa kudai eti Rais Donald Trump wa Marekani amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri ! Enzi zile, ungedhani kuna mashindano ya Mawizara na Taasisi za umma kumsifia Rais Magufuli! Uchawa huu ukapelekea waandishi 9 wa TBC wasimamishwe ! Waliosimamishwa ni Gabriel Zakharia, E. Mramba, P. Constantino, D. Mmari, R. Mpenda, L. Mushi, A. Wawa, C. Ruza na J. Losai.

2.4 Desemba 23, 2015, TBC iliwakera "Bongolanderz" nchi nzima pale ilipokatiza ghafla Taarifa ya Habari saa 2 usiku na kuonesha harusi ya Kibopa mmoja kwa masaa 3! Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari (Maelezo), Assa Mwambene akatiririka:

"TBC ilichofanya si sahihi. TBC ni chombo cha umma hakikupaswa kuonesha mambo ya mtu binafsi kwa zaidi ya saa tatu. Saa tatu umma unaangalia mtu anavyomsifia mke wake? Kisa amelipa milioni 17 ? Hii si sawa".

2.5 Baadhi ya watangazaji wa TBC uelewa wao ni mdogo sana kiasi kwamba kwenye mahojiano mubashara kuhusu mambo muhimu ya Kitaifa wanauliza maswali ya kijinga/kitoto sana na kukera mno (wapo baadhi wanauliza maswali ya maana mf Gabriel & Elizabeth). Aidha, wengine wanashindwa kutofautisha baadhi ya herufi mf "R" na "L".

2.6 Septemba 4, 2019. Kamati ya Maudhui ya TCRA ilitoa onyo kali kwa TBC kwa kukiuka Sheria, Kanuni na Misingi ya Uandishi wa Habari kwa kuonesha picha zisizofaa.

2.7 TBC ilifuta matangazo mubashara ya Bunge kwa sababu za kimchongo 2016. Ilielezwa kuwa TBC haitakuwa ikionesha bunge mubashara kwavile eti "Bongolanderz" wengi huwa makazini hivyo wanaacha kazi na kuangalia bunge! Tuliosomea Cuba tulibaini ni fiksi. Mhe Spika Ndugai baada ya "kustaafu" akamwaga mambo hadharani:

"Leo niseme ukweli; sababu ya kuachana na kuonesha bunge "live" ni kwavile tulibaini wabunge wa upinzani walikuwa wanapata coverage kubwa inayowapa kichwa. Tulibaini wengi hawaendi majimboni kwao, wanatumia bunge tu na wengine wanaishambulia sana serikali ili wajulikane kwavile wanajua kuna bunge "live"!.

2.8 Tukio la majuzi la Mv Mwanza ndio fungakazi. Mwandishi, bila kupepesa macho wala kutikisa mustachi, ameeleza eti meli hiyo itafika hadi Malawi & Zambia! Kwani inatumia matairi ? Hivi mnatuchukuliaje lakini? Mbaya zaidi, nimeiona taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ambayo haikutaja nchi hizo hivyo mwandishi kaongea urongo mwingine! Cha ajabu, hadi leo TBC haijatuomba radhi!

NB:

Ikumbukwe kuwa Mhe Harrison Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Habari, Sanaa & Utamaduni, alieleza bungeni alipowasilisha bajeti ya Wizara yake ya 2017/18 kuwa moja ya changamoto kubwa za TBC ni kutozingatiwa kwa maadili ya uandishi wa habari.

Miaka 7 baadaye, tatizo bado linataradadi!
Mtajuana na kazi zenu za serikali
 
Afanye kama tido muhando enzi hizo kwa kuwapa coverage kubwa wapinzani. Midahalo wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu iwepo kwa wagombea wote bila ubaguzi. Kikekeke aje na ubunifu mpya wa vipindi na muonekano mzuri wa tv. Urushaji wa matangazo mubashara toka kwa watangazaji wake walioko mikoani. Usikivu imara wa redio maeneo yote nchini na kuwepo na watangazaji wenye weledi na ufahamu wa mambo mbalimbali kuhabarisha umma
 
View attachment 2948917
Tetesi zinaelekeza Salim Kikeke anaendelea kutajwa kumngoa Ayub Ryoba alijizindika pale TBC. Hi ni baada ya chombo hiki cha wananchi kushindwa mambo mengi na kufuja fedha za umma huku watumishi wake wengi wakijianzishia makampuni shindani na TBC. Ukichukua TIN za watumishi utashangaa wao ndio wana maduka yaiuza bidhaa kwa TBC.​

1. TBC ni chombo cha umma ambacho kinapaswa kuwa na weledi wa hali ya juu. TBC inapaswa kujitofautisha na vyombo vya mchongo vilivyozagaa nchini.

2. Kuna matukio mengi ambayo TBC imeyafanya bila kuzingatia weledi. Itoshe kuyataja machache:

2.1 Mwaka 2014 wakati wa Mjadala wa Katiba, TBC ilikuwa ikitoa upendeleo na kukera wengi akiwemo Mwandishi nguli Maggid Mjengwa wa Iringa ambaye alilazimika kulalamika. Aidha, TBC ghafla ilikatisha matangazo April 14, 2014 wakati Mhe Tundu Lissu akitoa maoni kwa niaba ya Kamati yake! Dr. Slaa, aliyekuwa KM CHADEMA, akazomoka:

"TBC ni aduinwa mageuzi. Serikali imesahau kuwa ilisaini Maadili ya vyombo vya umma vitumike kwa manufaa ya imma bila upendeleo".

2.2 Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020, TBC ilikinaisha kwa kuonesha kampeni za CCM tu 24/7 hadi kupachikwa jina la utani TBCCM il hali TBC ni chombo cha umma na il hali kuna uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa vyombo vyote vya habari vya umma vinapaswa kutoa haki sawa kwa vyama vyote.

2.3 Machi 10, 2017, TBC, kwa uchawa wake, ilitulisha "Bongolanderz" matango pori kwa kudai eti Rais Donald Trump wa Marekani amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri ! Enzi zile, ungedhani kuna mashindano ya Mawizara na Taasisi za umma kumsifia Rais Magufuli! Uchawa huu ukapelekea waandishi 9 wa TBC wasimamishwe ! Waliosimamishwa ni Gabriel Zakharia, E. Mramba, P. Constantino, D. Mmari, R. Mpenda, L. Mushi, A. Wawa, C. Ruza na J. Losai.

2.4 Desemba 23, 2015, TBC iliwakera "Bongolanderz" nchi nzima pale ilipokatiza ghafla Taarifa ya Habari saa 2 usiku na kuonesha harusi ya Kibopa mmoja kwa masaa 3! Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari (Maelezo), Assa Mwambene akatiririka:

"TBC ilichofanya si sahihi. TBC ni chombo cha umma hakikupaswa kuonesha mambo ya mtu binafsi kwa zaidi ya saa tatu. Saa tatu umma unaangalia mtu anavyomsifia mke wake? Kisa amelipa milioni 17 ? Hii si sawa".

2.5 Baadhi ya watangazaji wa TBC uelewa wao ni mdogo sana kiasi kwamba kwenye mahojiano mubashara kuhusu mambo muhimu ya Kitaifa wanauliza maswali ya kijinga/kitoto sana na kukera mno (wapo baadhi wanauliza maswali ya maana mf Gabriel & Elizabeth). Aidha, wengine wanashindwa kutofautisha baadhi ya herufi mf "R" na "L".

2.6 Septemba 4, 2019. Kamati ya Maudhui ya TCRA ilitoa onyo kali kwa TBC kwa kukiuka Sheria, Kanuni na Misingi ya Uandishi wa Habari kwa kuonesha picha zisizofaa.

2.7 TBC ilifuta matangazo mubashara ya Bunge kwa sababu za kimchongo 2016. Ilielezwa kuwa TBC haitakuwa ikionesha bunge mubashara kwavile eti "Bongolanderz" wengi huwa makazini hivyo wanaacha kazi na kuangalia bunge! Tuliosomea Cuba tulibaini ni fiksi. Mhe Spika Ndugai baada ya "kustaafu" akamwaga mambo hadharani:

"Leo niseme ukweli; sababu ya kuachana na kuonesha bunge "live" ni kwavile tulibaini wabunge wa upinzani walikuwa wanapata coverage kubwa inayowapa kichwa. Tulibaini wengi hawaendi majimboni kwao, wanatumia bunge tu na wengine wanaishambulia sana serikali ili wajulikane kwavile wanajua kuna bunge "live"!.

2.8 Tukio la majuzi la Mv Mwanza ndio fungakazi. Mwandishi, bila kupepesa macho wala kutikisa mustachi, ameeleza eti meli hiyo itafika hadi Malawi & Zambia! Kwani inatumia matairi ? Hivi mnatuchukuliaje lakini? Mbaya zaidi, nimeiona taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ambayo haikutaja nchi hizo hivyo mwandishi kaongea urongo mwingine! Cha ajabu, hadi leo TBC haijatuomba radhi!

NB:

Ikumbukwe kuwa Mhe Harrison Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Habari, Sanaa & Utamaduni, alieleza bungeni alipowasilisha bajeti ya Wizara yake ya 2017/18 kuwa moja ya changamoto kubwa za TBC ni kutozingatiwa kwa maadili ya uandishi wa habari.

Miaka 7 baadaye, tatizo bado linataradadi!
Kumbe unatuletea siasa za wale nyumbu
 
.........duuh! sijui mi ndo sielewi au ni vipi, nilidhani hapa tunaenda kuona ufujaji wa fedha katika utendaji wa tbc hasa miaka hii miwili mitatu, kumbe bado tunajadili rasimu ya katiba ya 2014 hatukui hata kama Mh Samia atakuwa makamu, tupunguze kukurupuka jamani, pia kubadili kiongozi mmoja sidhani kama ni mkeka labda ingekuwa listi viongozi kadhaa kubadilishwa, hata hivyo Kikeke au yeyote akiletwa hapo TBC haitakuwa Kwa sababu hizo sababu za miaka ya 47.......
 
Back
Top Bottom