TBC, kipindi cha Bongo Kama Ulaya mnarudia maudhui yaleyale kila siku

TBC, kipindi cha Bongo Kama Ulaya mnarudia maudhui yaleyale kila siku

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,312
Reaction score
3,345
Tunajua hiki kipindi cha Bongo Kama Ulaya kipo kwa ajili ya kukusanya kura tar 28 lakini kwa sasa hiki kipindi kinaboa.

Kila siku madaraja ya juu na treni za mwendo kasi, sidhani kama mmejipanga vizuri.

Habari inanoga kama huwezi kutabiri kabla ya kuiona/kuisikia lakini hiki kipindi kikifika tu tayari unajua kama si madaraja ya juu ni mwendokasi.

Yani mnatumia nguvu kubwa sana kumsaidia kusaka kura mpaka sasa mnafanya mambo pasipo kufikiri sawasawa.

Jitafakarini upya, hii Bongo Kama Ulaya kama mmeishiwa vyakuonesha futeni hiki kipindi.
 
Wapo wanaoangalia mkuu, we jaribu kubadilisha channel, maana zipo nyingi tu

Lakini ni muhimu kufanyia kazi ushauri wako, maana washazoea kurudia vipindi hawa jamaa
 
Mtoa mada tunakutegemea nawe uende ughaibuni ili tukurushe hewani ukisifia juhudi
 
Khaaaa!!!

Kumbe watu tunakosa mambo enh?!

Yaani Televisheni ya Taifa ina kipindi kinachoitwa Bongo Kama Ulaya?!

Nini maudhui ya hicho kipindi?!

Ni matumaini yangu maudhui ya Bongo Kama Ulaya hayana uhusiano wowote na hizi Flyovers 2 zilizo Dar es salaam!!!
 
Sasa kama hakuna kingine kinachofanana na ulaya na wameambiwa waifananishe na ulaya watafanyaje ?
 
Kuna baadhi ya watu hawakuyaona hayo ya nyuma mkuu kwa maana sio kila mtu anapata fursa ya kuangalia TV kila siku.

Wewe jaribu kuangalia TV stations za wazungu kama BBC na CCN headlines ni hizohizo kwa muda wa 24 hours unless kuwe na breaking News kwa maana wanatambua fika ya kuwa kila mmoja ana ratiba yake binafsi katika uangalizi wa habari.
 
Sisi wana-diaspora tunavipenda vipindi hivyo kwani hutupa picha kamili ya kinachoendelea huko.
 
Kuna baadhi ya watu hawakuyaona hayo ya nyuma mkuu kwa maana sio kila mtu anapata fursa ya kuangalia TV kila siku.

Wewe jaribu kuangalia TV stations za wazungu kama BBC na CCN headlines ni hizohizo kwa muda wa 24 hours unless kuwe na breaking News kwa maana wanatambua fika ya kuwa kila mmoja ana ratiba yake binafsi katika uangalizi wa habari.
Unasema BBC headline ni hizohizo tu kwa masaa 24,mimi nakwambia kipindi cha bongo kama ulaya ni habari za madaraja ya juu na mambo ya mwendo kasi kwa zaidi ya mwezi sasa,rudia kusoma tena nilivyoandika halafu urudi tena!24hrs haifanani na mwezi mzima.
 
Uchumi umebana mpaka umeshindwa kulipia king'amuzi ? Pole sana mkuu, tutaiondoa CCM madarakani tu
 
Back
Top Bottom