TBC kudhamini ligi ya NBC hatupati value for money

Tatizo linaanzia kwako wewe mtazamaji kuchukua uamuzi wa kuangalia TBC
Mimi Niko huku kijijini, naambiwa TBC ndiyo mwenye haki ya matangazo ya radio, lakini mpira inaanza wao wanasema mambo mengine kabisaaa. Baada ya dk tano mpira kuanza wao ndio wanaanza kutangaza mpira na katikati ya mpira unaendelea wao wanatangaza mambo mengine kabisaaa. Wakati mwingine bao linafungwa wakiwa wanatangaza mambo mengine kabisaaa.
 
Sio kweli, Kuna wakati goli linafungwa wakati wao wakiwa kwenye matangazo yao mengine. Kuna wakati timu inafanya sub wakati wao wakiwa kwenye matangazo yao mengine. Kuna wakati wanaja lineups baada ya dk 5 mpira kuanza
 
TBC inaendeshwa na Kodi zetu, hakuna mfanyakazi wa TBC analipwa kwa fedha za matangazo hayo ya viwembe butu. Wenye radio yao wanataka kupata huduma ya kusikiliza kandanda kupia Kodi zao. Hizo biashara waachwe wafanye Radio One, Clouds, abood FM, RFA, UFM, etc badala ya TBC kuhodhi ukiritimba wa matangazo.
 
Tulitarajia Radio itufanyie uchambuzi wa kuhusu mechi, timu, wachezaji, makocha na matukio yooote muhimu ya uwanjani kwakuwa sisi hatujui, hatuoni na hatuko uwanjani. Lakini kwa TBC loooo!! siyo hivyo.

Huwa wakati mwingine nasikiliza matangazo ya mpira BBC ligi ya england, hakuna matangazo ya good good kunyoa nywele zote katikati ya mpira. Abood FM ilikuwa hakuna matangazo katikati ya mpira, UFM hakuna hilo, iweje TBC yetu wenyewe iwe hivi?
 
Usilalamike kwani umechaguliwa au kulazimishwa kuangalia hiyo channel?
 
Ni kweli ni miaka mingi sijakaa kusikiliza mpira kwenye redio na nashangaa kuna watu bado wanafanya hivyo. Nilivyomuelewa mleta mada anasema matangazo ya mpira yanakatwa kwa ajili ya matangazo ya biashara wakati mpira unaendelea.
Exactly!! Ladha ya mpira kupitia radio siku hizi hakuna. Tofauti na zama zile za akina Chilambo, Hillary, Nkamia, mbonde, mikidadi, TIDO. Siku hizi ni vuluvulu TU. Goli linafungwa watu wanatangaza rungu.
 
Tatizo linaanzia kwako wewe mtazamaji kuchukua uamuzi wa kuangalia TBC
Kaka hatuangalii TBC bali tunasikiliza TBC Radio yetu tukufu inayoendeshwa kwa Kodi ya wananchi.
 
Kule YouTube kuna redio nyingi hutangaza Mpira, Kumbuka TBC hawalazimishi mtu kuwasikiliza
Sisi wanyonge tusio na Azam tv Wala simu janja tunaitegemea sana TBC Radio kwenye starehe ya mpira ndiyo maana tunayasema haya yanayotukera
 
Nakiliza sana mpira kupitia radio TBC hasa radio ya kwenye gari pale ambapo muda wa kuingalia mechi kwenye luninga sina. Matangazo yanakatwa sana. Hebu fikiria mtu anakutajia list ya wachezaji wakati mpira unaendelea kuchezwa na baada ya dk 5 za mchezo kupita.
 
Mara ya mwisho kusikiliza mpira katika radio ni mwaka jana niligonganga na hayo matangazo ya TBC mjini Youtube. Nikasikia mtangazaji anasema "vijana wanasema amefinyia kwa ndani". Hapo hapo nikaamua kusave bando langu.

Unaposema matangazo hukatwa mwanzoni mwa kipindi cha kwanza na mwishoni mwa kipindi cha pili, hapo mpira unakuwa umeanza/umeisha?

Pia kwa maelezo ya mleta mada amesisitiza kuwa matukio mengi wanayamiss ikiwemo ya magoli kwa kuwa radio inakuwa kwenye matangazo. Sasa nani mkweli kati yenu nyie wawili?
 
Hao watoto wa juzi hawawezi kukuelewa, tulioanza fatilia mpira kabla ya tv hatushangazwi na anachofanya TBC leo
 
Tatizo kuna Watu mna tabia ya kuchangia hoja kabla kuelewa.Kimsingi Mleta mada ana hoja, hata mimi nilitaka kuanzisha uzi. Kuna wakati una tune tbc usikilize mpira unakutana na mambo mengine kabisa ili hali wao ndio wamehodhi haki za matangazo wakichelewa kujiunga au hata wasipotangaza wao basi ndio imeisha hiyo.
 
We tafuta hela nunua king'amuzi. Yaani unataka uenjoy ukisikiliza TBC?
Acha utani wewe
 
Kuna magoli yanafungwa dk ya kwanza hadi Tano za kwanza ya kipindi na dk za majeruhi kabisa lakini mtangazaji Yuko bize na maokoto na upuuzi mwingine. Msikilizaji anachanganyikiwa akisubiri tangazo liishe.
 
Kuna magoli yanafungwa dk ya kwanza hadi Tano za kwanza ya kipindi na dk za majeruhi kabisa lakini mtangazaji Yuko bize na maokoto na upuuzi mwingine. Msikilizaji anachanganyikiwa akisubiri tangazo liishe.
Kama ni hivyo, huo ni upuuzi wa hali ya juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…