TBC kudhamini ligi ya NBC hatupati value for money

Kama ni hivyo, huo ni upuuzi wa hali ya juu.
Mara nyingi wapenda mpira wa miguu huwa wanazichukia bidhaa zinazotangazwa kwa aina hii. Kuna vyombo vya kutoa huduma na Kuna vyombo vya kibiashara, TBC ni watoa huduma TU ya kuhabarisha, kufurahisha nabkuelimisha wananchi bila kujali gharama. Sio sawa kuhodhi matangazo ya mpira.
 
Mara nyingi wapenda mpira wa miguu huwa wanazichukia bidhaa zinazotangazwa kwa aina hii.
Na mimi nilitaka kusema. Wanawaharibia hao wanaowatangaza, wao wanadhani wanawasaidia kwa kuwalazimisha wasikilizaje wasikilize matangazo yao kwa nguvu.
 
sikumbuki mara ya mwisho ni lini niliwaangalia hao tbccm
 
Na mimi nilitaka kusema. Wanawaharibia hao wanaowatangaza, wao wanadhani wanawasaidia kwa kuwalazimisha wasikilizaje wasikilize matangazo yao kwa nguvu.
Wanaichonganisha bidhaa na walaji.
 
Goli limefungwa wakati tangazo la biashara linaendelea halafu mtangazaji anajishebedua kwa kusema Wacha nihadithie namna goli lilivyotokea wakati mdhamini wetu Yuko hewani. Maloon!!
 
Kwani tangazo moja linachukua muda gani kutangaza, na je, ni lazima shida ya mchezaji aliyeumia ichukue muda sawa na urefu wa tangazo, unakatisha tangazo baada ya mchezaji kuendelea kucheza, na je msikilizaji hataki kujua mchezaji aliyeumia ni nani na ameumiaje na anatibiwaje?
 
TBC kama wameamua kuhodhi ukiritimba wa matangazo ya mpira basi watenge muda kama nusu saa au dk 15 kabla ya mpira kuanza kuuzungumzia mpira na matangazo. Watu wengi watavutika kusikia uchambuzi uliotukuka unaoambatana na matangazo ya wadhamini. Half-time hivyohivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…